Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  28 Ramadan 1444 Na: 1444/09 H
M.  Jumatano, 19 Aprili 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tunawapa Pongezi kwa Idd ul-Fitr

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Kenya inapenda kutoa salamu za dhati za Idd ul-Fitr yenye baraka kwa Waislamu nchini Kenya na dunia nzima kwa jumla.

Idd hii yenye baraka inakuja huku umbile katili la Kiyahudi likiwafanyia ukatili ndugu na dada zetu wapendwa huko Al-Quds;

kibla cha kwanza cha Ummah na Ardhi ya Israa’. Cha kusikitisha ni kwamba, unyama wa waziwazi unaofanywa na majeshi ya Kiyahudi bado ungali haujachemsha nyoyo wala mishipa ya viongozi wa Kiislamu na majeshi yao! Viongozi wa Waislamu ambao kwa hakika ni Ruwaibaidha wamekuwa wakiunga mkono siku baada ya siku njama ovu za Kiyahudi kama vile kuhalalisha mahusiano yao na dola hii ya ubaguzi wa rangi ya Kizayuni. Suala la Palestina kama suala jengine lolote linaloshuhudiwa duniani kamwe halitatatuliwa kwa kufanya 'mikutano ya dharura' ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa au kauli tupu za Riyadh, Tehran, Islamabad au Istanbul. Tunahitaji Khilafah ambayo itakusanya majeshi ya Waislamu ili kuling'oa umbile la mauaji la Kiyahudi na kukomboa sio tu Palestina inayokaliwa kwa mabavu pekee bali ardhi zote za Waislamu. Khilafah pia itasuluhisha matatizo yote ya kijamii, kiuchumi na kisiasa duniani kwa suluhisho la kudumu na la kina Bi’idhnillah.

Hatimaye tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atukubalie matendo yetu mema na atuongoze kwenye Idd ya mwakani tukiwa chini ya kivuli cha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itaziunganisha nchi zote za Kiislamu duniani chini ya bendera ya 'Laa ilaha illa Allah Muhammad Rasul Allah'.

[لِلَّهِ الأمْرُ مِنْ قَبْلُ وَمِنْ بَعْدُ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ بِنَصْرِ اللَّهِ]

“Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu.” [Ar-Rum: 4]

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu