Afisi ya Habari
Kenya
H. 1 Jumada II 1445 | Na: 1445/08 H |
M. Alhamisi, 14 Disemba 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Miaka Sitini ya Uchungu na Machafuko
(Imetafsiriwa)
Kenya iliadhimisha miaka 60 ya ‘uhuru’ mnamo Jumanne, tarehe 12 Disemba 2023. Siku hiyo huadhimishwa kila mwaka mnamo Disemba 12, kuadhimisha siku ambayo mnamo 1963 Kenya ilipata uhuru wake kutoka kwa utawala wa kikoloni wa Uingereza.
Sisi katika Hizb ut Tahrir Kenya tunapenda kuangazia yafuatayo:
Neno "uhuru," baada ya Vita vya Pili vya Dunia, lilikuja kumaanisha "ukombozi" kutokana na ukoloni. Kiuhalisia, hii ni maana yake ya juu juu pekee. Ukweli ni kwamba mwenye jambo hili ni Marekani, ambayo ndiyo iliyolivumbua ili kutoa fursa ya kuyavua makoloni kutoka kwa wakoloni wengine. Uhalisia wa uongozi wa kisiasa nchini humu tangu uhuru bandia wa Kenya kutoka kwa Waingereza, ndio umekuwa mnufaika wa kweli wa kukabidhiwa huku kwani wao ndio wamiliki wa ardhi kadhaa wakiwaacha wananchi jumla wakiwa maskwota.
Mbegu za kufeli na mporomoko nchini zilipandwa na wakoloni ambao walikuuza tofauti kati ya jamii na makabila mbalimbali, na kuanzisha mapigano ambapo kila jamii ilikosa imani na nyengine na kuchochea mapigano. Viongozi wa kisiasa nchini hujitolea kwa ajili ya maslahi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ili yapatikane kupitia mamlaka ya mazungumzo ya kikanda na kikabila ambayo hutumika kama zana za mapato na mafanikio ya kisiasa. Kuregeshwa kwa Demokrasia ya vyama vingi inayochukuliwa kuwa ukombozi mpya kumeiweka nchi katika migawanyiko ya kikabila na chuki zaidi huku tabaka la kisiasa likitumiwa kuteka nyara misukumo ya umma katika kuweka ajenda zinazolenga kutoa matumaini ya upotoshaji. Kutangazwa kwa katiba mpya ya 2010 ambayo ilikuja na mfumo mpya wa utawala wa ugatuzi haujaokoa raia kutoka kwa matatizo.
Kinachoifanya Kenya ishindwe kutatua matatizo ya kimsingi ya umma ni kwa sababu ya kuegemea mfumo wa kibepari wa kikoloni ambao msingi wake ni akili ya mwanadamu na sio Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Kwa kutekelezwa kwake na tawala mtawalia, sera mbovu za kibeberu - za kikoloni kunaendelea kudhuru Kenya. Ni kupitia mikataba ya kibiashara na dola kubwa za Magharibi kama Uingereza na Marekani ambayo imeiacha Kenya na Afrika kwa jumla zikiwa zimeharibiwa na viwango vya kuzorota vya umaskini, njaa na magonjwa.
Ili kupata uhuru wa kweli, tunahitaji mfumo ambao utabadilisha jamii kwa kiasi kikubwa ambao si mwingine bali ni Uislamu. Kwa uhalisia, kwa mfumo wa kina wa Kiislamu, miaka sitini inatosha kupata mafanikio makubwa. Mafanikio makubwa zaidi yalipatikana ndani ya muda mfupi na viongozi wa kweli walioutekeleza Uislamu kupitia dola huru ya Khilafah. Kwa mfano, Khalifa Umar bin Abdul Aziz (ra) aliweza kuunda jamii isiyo na umasikini kwa muda wa miaka miwili na miezi mitano tu. Kuanzia sasa, uhuru wa kweli unaweza kupatikana tu kupitia utekelezaji kamili wa Uislamu katika nyanja zote za maisha chini ya mwavuli wa Dola ya Khilafah itakayosimamishwa tena katika mojawapo ya nchi za Kiislamu.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |