Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  22 Rabi' I 1446 Na: 1446/02 H
M.  Jumatano, 25 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari
Muozo wa Tabia na Maadili, Tunda la Mfumo Mbovu wa Ubepari

(Imetafsiriwa)

Kutekwa nyara kwa mwanablogu wa Mombasa Bruce John, ambaye pia alilawitiwa na kundi la wanaume kumezua kilio cha umma katika Jiji la Pwani la Mombasa na Kenya kwa jumla. Wito wa haki umekuwa mwangwi, marafiki, familia, na wanaharakati wa haki za binadamu wakikusanyika kumuunga mkono mwanablogu huyo mchanga. Sisi katika Hizb ut Tahrir / Kenya tungependa kutaja yafuatayo:

Inatia wasiwasi mkubwa kwamba muozo na tabia mbaya imefikia kiwango cha kutisha kwa katika mizani ya kimataifa. Maadili ya kiliberali ya kisekula yameunda umma kwa jumla katika kutabanni mbinu chafu kama vile unyanyasaji na kashfa kama zana za kuonyesha chuki za kisiasa.

Ulimwenguni kote, ni ukweli uliodhihirika kwamba ubakaji na ulawiti vimekuwa zana ya kisiasa na kijeshi ya kudhibiti chuki za kisiasa. Hata hivyo hii inapaswa kuwakumbusha wanadamu kwa jumla na Umma wa Kiislamu hususan kufilisika tabia na maadili ya itikadi ya kisekula ambayo haina mwelekeo na maadili. Tofauti na Uislamu, Usekula huvua maadili yake kutoka katika falsafa ya starehe (utilitarianism) ambayo hupigia debe vitendo vinavyokuza furaha au raha na kupinga vitendo vinavyosababisha kutokuwa na furaha au madhara vinapoelekezwa kwenye kufanya maamuzi ya kijamii, kiuchumi, au kisiasa. Wanadamu chini ya jamii ya kibepari isiyo na maadili wamekuwa wabaya zaidi kuliko wanyama kama ilivyoelezwa katika Quran:

[ثُمَّ رَدَدْنَاهُ أَسْفَلَ سَافِلِينَ] “Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!” [At-Tiin: 05].

Kwa zaidi ya karne 13, Uislamu tangu kuasisiwa kwa Dola mjini Madina hadi kuvunjwa kwake na Wakoloni wa Magharibi mnamo 1924, wanadamu walikuwa na viwango vya juu vya maadili. Hili lilidhihirika kwa kuegemea kwenye itikadi ya Kiislamu ambayo inalinda na kulea maadili yenye malengo na hivyo kudhamini mafanikio katika nyanja zote za maisha. Ni dhahiri, Uislamu ni hitaji la wakati sasa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ili kunyanyua maadili ya kimalengo ya jamii. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى كَثِيرٍ مِّمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلاً]

“Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba.” [Al-Isra’a: 70].

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir

Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu