Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  11 Jumada II 1441 Na: 1441 / 05
M.  Jumatano, 05 Februari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kukataa Kuitathmini Hijab, Thibitisho kuwa Haki za Waislamu Haziwezi Kudhaminiwa Kupitia Katiba ya Kisekula

Mahakama ya Upeo imetupilia mbali ombi la kuitathmini kesi ya Hijab iliyo sajiliwa ili kubatilisha agizo kutoka Shule ya St Paul Kiwanjani la kupiwapiga marufuku wanafunzi Waislamu kutokana na kuvaa Hijab. Hukmu hiyo imeibakisha hukmu ya awali iliyotolewa mnamo Januari mwaka jana iliyoiweka kando hukmu ya mahakama ya rufaa iliyo kuwa imeruhusu uvaaji wa Hijab shuleni. Miongoni mwa mambo yaliyoibuliwa katika ombi hilo la kutathmini ilikuwa ni kwamba hukmu ya mwaka jana ya Mahakama ya Upeo ilipuuzilia mbali kadhia muhimu za kikatiba hivyo basi ilitolewa kwa msingi wa dosari za kiutaratibu. 

Kuhusiana na hili, tungependa kusema yafuatayo:

Ile inayoitwa katiba iliyo endelea ya 2010 inadhamini uhuru wa kuabudu na kujieleza lakini inapima uhuru hizo dhidi ya uhuru nyinginezo! Kwa msingi wa dosari hizo za 'kiutaratibu' mahakama imewanyima haki Waislamu na inaruhusu idara ya shule kuwanyima haki hizo. Kutokana na hukmu hii, wanafunzi Waislamu kote nchini wanakabiliana na changamoto katika mambo ya Dini yao. Baadhi ya shule zikikosa kuwapa sehemu ya kuabudu huku nyinginezo zikiwalazimisha wanafunzi Waislamu kuhudhuria ibada za kidini za imani nyinginezo. 

Hukmu hii ni shambulizi baya juu ya Uislamu kwani Hijab ni hukmu ya kidini juu ya wanawake wote Waislamu. Tunaliona hili kama sehemu ya kampeni kubwa ya kiulimwengu dhidi ya Waislamu. Ulimwengu unajua dhahiri jinsi gani mamlaka za Uchina zinavyo wahangaisha Waislamu wa Uyghur kwa kutumia mbinu katili kama vile kuwazuia kutekeleza ibada zao na kuhudhuria misikitini kupitia kuifunga pamoja na kuwazuia kutokana na kufunga saumu katika mwezi mtukufu wa Ramadhan. Vitendo hivi viovu ni ukiukaji wa wazi wa haki msingi. 

Katiba ya kisekula kamwe haitadhamini haki za Waislamu wanao wajibishwa kufuata sheria tukufu zilizo teremshwa na Muumba wao Mtukufu. Hukmu hii imefichua zaidi urongo wa uhuru na haki, ambazo hudhaniwa kuwa tukufu katika Demokrasia kama wanavyozipigia debe wakereketwa wa uhuru wa kisekula wa Kimagharibi. Kwa hakika uhuru kama hizi na zile zinazoitwa haki za kibinadamu ni urongo na uhadaifu kwa Waislamu. Tunatoa wito kwa Waislamu kwa jumla na hususan Wasomi kutopoteza juhudi zao katika kutafuta suluhisho katika mabadiliko ya kikatiba ya kisekula badala yake wanapaswa kufanya kazi kwa ajili ya Uislamu ambao ndio utakaolinda haki za Waislamu na wanadamu wote. Kwa yakini tunaudumisha Uislamu kupitia Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume ndio utakao dhamini kiukamilifu haki za raia wake.   

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu