Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  3 Ramadan 1440 Na: 1440 H / 10
M.  Jumatano, 08 Mei 2019

 Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Suala la Kuonekanwa kwa Mwezi Limegeuzwa kuwa la Kizalendo na Kisiasa wala Sio tena Suala la Kifiqhi

Kwa masikitiko makubwa badala ya Waislamu kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kheri na baraka kama ulivyo mwezi wenyewe, ndiyo mwanzo uhasama na chuki hutawala Waislamu katika suala la kuandama kwa mwezi.

Mkataba wa kikoloni baina ya Uingereza na Ufaransa; Sykes-Picot wa kuwagawanya Waislamu kimipaka ya kikoloni na kuwatala kupitia vibaraka (viongozi wa sasa wa nchi za Waislamu), kwa miaka yote wamekua wakijitambulisha kitaifa, kizalendo na kieneo. Hali mbaya zaidi kila nchi ikawa na mashekh na mabaraza yake ya kidini ambayo kwa bahati mbaya zaidi mabaraza haya yamekuwa yakitoa fatwa za kiajabu zinazo gongana moja kwa moja na dalili wazi za kiShari'ah. Twapenda kuzindusha kwamba saum ni ibada na siku kuu za idd pia ni ibada hivyo Waislamu hutakikana kujifunga na Shari'ah na wala sio matamanio kama inavyo shuhudiwa leo chini ya serikali za Kisekula.

Kwa uhalisia huu ndiyo licha ya kuwa ni kweli kuwa kuna rai mbili juu ya suala la mwezi; rai ya mwezi wa kiulimwengu na ile ya kimaeneo lakini kwa athari ya Sykes-Picot sasa kuna rai mpya na ngeni nayo ni mwezi wa kimapaka wa kizalendo! Kwa hivyo, hata kama baina ya nchi moja kwa nyengine zimetofautiana kwa dakika moja au tatu au hata nne Waislamu wamekuwa hawafungi pamoja kiulimwengu bali hata ndani ya nchi moja!

Twasema ni wazi kuwa kuishi ndani ya mataifa ya kisekula yamejeruhi pakubwa umoja wa Waislamu ambao umefaradhishwa na Mwenyezi Mungu (swt) aliposema: (وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا) (Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja wala msifarakiane) [Aal-e-Imran: 103]

Ayah hii inaawaamuru Waislamu mahala popote waishipo wajizingatie ni sehemu ya Ummah mmoja wa Waislamu. Haifai kwao wao kujifunga na utaifa, uzalendo na ukabila kwani zote ni fikra duni zisizofaa kuwa msingi wa kuunganisha watu. Na tunaona leo jinsi gani fikra hizi zinavyo tumbukiza Ummah katika vita leo.

Hali hii moja kwa moja tunaiona kuwa imetokamana na Waislamu kukosa Serikali halisi ya Kiislamu (Khilafah) inayoongozwa na kiongozi mmoja mwenye usemi wa mwisho. Hivyo twaendelea kukariri kwamba kusimamishwa tena Khilafah kwa njia ya Utume ndiyo kutakomesha mitafaruku baina ya Waislamu bali kuzuia uchochezi wa maadui wa Uislamu kuhujumu umoja wao. Ndani ya Khilafa kiongozi Khalifah au Imamu ana mamlaka ya kulazimisha rai ya Kiislamu kwa Waislamu ili kudumisha umoja wao. Hakika imesemwa kuwa amri ya kiongozi (Imamu) huondosha utata.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu