Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hakutakuwepo na Hadhi, Usalama na Ustawi kwa Wanawake Waislamu Bila ya Kusimamisha Khilafah Rashidah

Rajab hii inatukumbusha tukio baya mno, miaka 98 iliyopita pale Ummah wa Waislamu ulipopoteza dola yake adhimu, uongozi wake wa Kiislamu, mlinzi na ngao yake –Khilafah. Tokea wakati huo, wanawake Waislamu na familia zao wamejipata katika maangamizi ya mauaji, njaa, uvunjwaji, adhabu, kukosewa heshimu, umasikini wa kupindukia, upweke, ukandamizaji na madhila yasiyovumilika. Tumetoka kutoka kuwa chini ya dola iliyokuwa ina tawaliwa na viongozi wachamungu wakiwahudumia Ummah kwa huruma na kujali mahitaji yao kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu (swt)… kiasi kwamba Ummah upo chini ya viongozi wasiojali lolote kuwahusu, wanaoiba mali zetu kwa kujitajirisha, na kuwaadhibu Waislamu wanaoshikamana kikamilifu na Dini yao. Kutoka kuwa dola kubwa yenye kubeba Jihad kueneza Uislamu ili ikomboe miji, na iliyowafanya maadui zake kutetemeka kwa uoga kila wanapofikiria kumdhuru mwanamke Muislamu…tumekuwa wahanga wa mauaji na uvamizi.

Soma zaidi...

Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kimezindua Kurasa Mpya za Facebook: “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu”

Kufuatia mafanikio ya kampeni yetu ya kiulimwengu na kongamano la wanawake la kimataifa mnamo Oktoba 2018, “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu”, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kina furaha kutangaza uzinduzi wa kurasa zetu mpya za Facebook zinazojitolea kuangazia kadhia zinazo husiana na mgogoro wa kiulimwengu unao athiri “Kiungo cha Familia”. Kurasa hizi mpya, ambazo zitakuwa kwa Kiarabu, Kiingereza, Kituruki na Kiindonesia, zitawasilisha tena shehena ya fasihi zilizo chapishwa katika kampeni na kongamano pamoja na kutafuta mada za ziada kuhusiana na uhalisia, sababu na masuluhisho ya ukosefu wa utulivu na mfarakano unao athiri muundo wa familia katika jamii kote ulimwenguni.

Soma zaidi...

Wanawake wa Palestina Wangali Wanamsubiri Al-Mu’tassim ili Kuitikia Kilio Chao!!

Vyombo vya habari vilichapisha picha na video za majeshi vamizi ya umbile la Kiyahudi yakifurusha katika nyumba moja ya familia ya Jerusalem eneo la Aqaba Al-Khalidiya katika mji wa kale wa Jerusalem kwa kutumia nguvu za kijeshi. Vyombo hivyo vya habari vilionyesha nduru na malalamishi ya wanawake waliolalamikia shambulizi la polisi wa Kiyahudi katika nyumba hiyo, wakimpiga na kumkamata mwenye nyumba hiyo, na kuwaacha wao bila ya ulinzi na makao baada ya nyumba yao kuchukuliwa.

Soma zaidi...

Mwaelekea Wapi, Enyi Munao Simamia Muongozo wa Utoaji Fatwa wa Kiulimwengu?!!

Baadhi ya wanaume wa Al-Azhar wanaendelea kutembea juu ya barabara ya kuushambulia Uislamu na Hukmu zake pasi na maono wala hofu kwa Mwenyezi Mungu (swt). Wanaendelea kuifanya Al-Azhar Al-Sharif – ambayo ilikuwa ndio ngome dhidi ya njama za maadui wa Uislamu – jukwaa ambalo wanavishambulia vipengee vya Uislamu na Hukmu zake zinazo husiana na wanawake. Meza ya Utoaji Fatwa wa Kiulimwengu ya Jumba la Fatwa la Misri (Dar al-Ifta) zilisema kuwa, “fatwa juu ya kadhia ya ndoa kwa watoto wadogo zimeifunga ndoa kwa watoto wadogo katika mahusiano ya kijinsia pekee, na kwamba Hizb ut Tahrir imeifunga ndoa katika mahusiano ya kijinsia pekee, ikiondoa upande wa kisaikolojia, kiafya, kiakili na mambo ya kimwili, na kuweka mbali kiwango cha uvumilivu na jukumu ambalo mkataba wa ndoa unalazimisha juu ya pande zote mbili …” Hili, kwa kuanzia, linagongana na yale ambayo Quran Tukufu imeeleza kuhusu fahamu ya ndoa kama utulivu na huruma.

Soma zaidi...

Jinsi Siasa Inavyo Fanana na Zamani … Matukio Yanaendelea Kama Wanavyo Endelea Watazamaji!

Wanajeshi madhalimu wa umbile la Kiyahudi walimuua msichana kutoka Palestina kwa kummiminia risasi katika kituo cha upekuzi cha al-Za’im, mashariki mwa ardhi iliyo kaliwa Al-Quds (Jerusalem). Shahidi huyo ni mwanafunzi wa shule ya upili aliyekuwa amebeba mkoba wake wa shule wakati wa kuuwawa kwake; aliuwawa kutokana na madai ya kujaribu kutekeleza oparesheni ya kudunga kisu. Majeshi hayo vamizi yalizuia wahudumu wa ambulensi kutomfikia ili kumpa tiba. Aliachwa kuvuja damu hadi kufa.   

Soma zaidi...

Maradhi ya Utaifa Yamepelekea Kukamatwa kwa Wanawake na Watoto Wanaonyanyaswa wa Rohingya na Serikali ya Saudia

Mamia ya Waislamu wa Rohingya wanawake na watoto, waliokimbia mauwaji na ubakaji wa halaiki kutoka kwa Mabudha wenye misimamo mikali nchini Myanmar, wanaendelea kuzuiliwa pasipo kujulikana hatima yao katika Kituo cha Kizuizi cha Shumaisi nchini Saudi Arabia, baada ya kutafuta hifadhi katika dola hiyo.

Soma zaidi...

Je, Watoto wa Kambi ya Wakimbizi ya Al-Rukban Wataachwa Wafe kwa Baridi na Njaa, Huku Wakikosa Mtu Yeyote wa Kuwaokoa?!

Watoto kumi na tano wasio na makao, wengi wao wakiwa wachanga, wamekufa nchini Syria kutokana na baridi kali na ukosefu wa matibabu, kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF mnamo Jumanne 15/1/2019. Watoto, 13 kati yao walio chini ya umri wa mwaka mmoja, walifariki katika kambi ya Al-Rukban kusini mashariki mwa Syria, karibu na mpaka wa Jordan. Al-Rukban na kambi nyenginezo zinakumbwa na uhaba mkubwa sana wa misaada ya kibinadamu, pindi wakimbizi wanapowasili baada ya safari nzito baada ya kukimbia ngome ya mwisho ya ISIS mashariki mwa nchi hiyo. Geert Cappelaere, mkurugenzi wa UNICEF wa eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, alisema “Baridi kali zaidi na hali mbaya za maisha katika Al-Rukban zimesababisha maisha ya watoto kuongezeka kuwa hatarini,” aliongeza, “Kwa mwezi mmoja tu, kwa uchache watoto wanane wamekufa – wengi wao wakiwa chini ya umri wa miezi minne, na mdogo wao zaidi akiwa umri wa saa moja.”   

Soma zaidi...

Majanga Halisi Maovu Hata Bila ya Kuwepo Dhoruba za Barafu

Wakimbizi katika kambi za kinyama kadha wa kadha wameyaomba usaidizi mashirika ya misaada na wametoa wito kwa msaada wa dharura kutoka kwa mamlaka husika. Wamesema kuwa ni kiwango kidogo pekee cha msaada ndio kimewafikia wakaazi katika kambi, ambacho hakitoshi kwa asilimia 10 ya idadi jumla ya wakimbizi katika kambi, katika wakati ambapo kuna uhaba mkubwa wa mafuta na njia za kujikanza moto katika hali mbaya za anga kama hizo ambazo zimelikumba eneo zima la Ash-Sham.

Soma zaidi...

Enyi Waislamu…Waokoeni Watoto wa Yemen!

Mnamo 21/11/2018, ripoti ya Shirika la Uingereza la Okoa Watoto ilisema kuwa takribani watoto 85,000 chini ya umri wa miaka mitano wamekufa kutokana na ukosefu wa lishe bora ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya vita ndani ya Yemen.  Idadi hii pekee ni sawa na jumla ya idadi ya watoto walioko chini ya miaka mitano ndani ya Birmingham, jiji la pili kubwa ndani ya Uingereza.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia Ilikuwa Mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Wanawake “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu”

Mnamo Jumamosi 27 Oktoba, kwa Baraka za Allah, Alhamdulillah, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa ushirikiano na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kwa ufanisi kilifanya kongamano kubwa na la kuvutia la kimataifa la wanawake jijini Tunis lenye kauli mbiu, “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu” ili kuelezea sababu na suluhisho la Kiislamu juu ya mgogoro unaoathiri utulivu na umoja wa ndoa na maisha ya familia katika jamii kote ulimwenguni, ikiwemo biladi za Waislamu. Tukio hili muhimu lilihudhuriwa na zaidi ya wanawake 250 kutoka kote nchini Tunisia wakiwemo mawakili, walimu, walezi wa watoto, wahandisi, wanafunzi wa vyuo vikuu, viongozi wa jamii, na watetezi wa vijana. Hotuba zilitolewa na wanachama wa kike wa Hizb ut Tahrir kutoka Tunisia, Uturuki, Ardhi Iliyo Barikiwa – Palestina, Pakistan, Lebanon, Indonesia, Ghuba la Kiarabu. Uholanzi, na Uingereza. Kongamano hilo vile vile lilipeperushwa moja kwa moja mtandaoni kwa washiriki wa kimataifa na kutazamwa na maelfu ya watazamaji kutoka katika pembe tofauti tofauti duniani. 

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu