Ujasusi wa Ufaransa Waikanyaga Sheria na Kufichua Ukweli kuhusu Nchi ya Maarifa na Uhuru kwa Kuomba Kufanyika Sensa ya Watoro Shuleni siku ya Idd al-Fitr!!
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Gazeti la kila siku la Ufaransa la La Dépêche lilichapisha mnamo Ijumaa, Mei 19, 2023, habari iliyosema kwamba takriban shule mia moja huko Toulouse na vitongoji vyake zilipokea barua pepe kutoka kwa polisi wa Ufaransa wakiomba kiwango cha utoro wa wanafunzi mnamo Aprili 21, 2023, ambayo ilisadifu kuwa ni sikukuu ya Idd al-Fitr.