Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  2 Muharram 1442 Na: 1441 H / 001
M.  Ijumaa, 21 Agosti 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kimezindua Kampeni: "KOMESHA Vitisho kwa Wanawake WachaMungu wa Kiislamu wa Kyrgyzstan!"

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kinataka kukomeshwa muendelezo wa mateso na vitisho kwa wanawake wachaMungu wa Kiislamu wa Kyrgyzstan na serikali ya kikatili ya kisekula ya Kyrgyzstan. Serikali hii ya ukandamizaji, ambayo imezindua vita dhidi ya Uislamu chini ya madai ya uongo na muonekano wa kihadaifu ule unaoitwa vita dhidi ya ugaidi, imewakamata kwa dhulma idadi kadhaa ya wanawake wa Kiislamu kwa kuwatuhumu kuwemo ndani ya Hizb ut Tahrir ambayo inatabanni kazi ya kisiasa isiyo na vurugu kwa ajili ya kusimamisha Dola ya Kiislamu ya Khilafah.

Mnamo 27 Juni 2020 M, Kamati ya Usalama wa Kitaifa ya Dola nchini Kyrgyzstan iliwakamata wanawake wa Kiislamu 8 wasiokuwa na tishio lolote katika mji wa Naryn kwa kushukiwa kuwemo ndani ya Hizb ut Tahrir, ambayo Serikali ya Kyrgyzstan imekipiga marufuku chama hiki kwa madai ya kipuuzi kuwa ni shirika lenye misimamo mikali, licha ya kuwa kwa hakika Hizb haijashiriki katika kitendo chochote cha ghasia. Wanawake walio kamatwa ni: Arunova Erkingul ambaye ni mchunzaji wa mamake ambaye alipata kiharusi na yuko katika hali mbaya, ilhali bado angali kizuizini; na Baktybek kyzy Mahabat ambaye ana tatizo la kiafya linalo hitaji matibabu ya mara kwa mara na ni mama wa watoto wawili walio katika chekechea, ilhali bado angali kizuizini; Ajumudinova Almagul, ambaye siku ya kukamatwa kwake alikuwa anampa uangalizi mjukuu wake aliyesibiwa na maradhi ya kupooza kwa ubongo, na licha ya hivyo bado walimkamata; Ajumudinova Archagul, yeye ni mama wa watoto wanne umri wao ni miaka 16, 9, 6 na 2; Ismailova Meerim, mama wa mabinti wanne umri wao ni miaka 12, 10, 8 na 6, na ambaye yuko kifungo cha nyumbani, ; Kadyralieva Meerim, mama wa watoto wawili ambao umri wao ni miaka 9 na 5; Aytbekova Gulnur, mwenye umri wa miaka 25 na aliyeolewa; na Mamirkanova Amangul, mama wa watoto wanne umri wao ni miaka 17, 16, 10 na 4.

Licha ya kuwa nchi hii iko chini ya misingi ya karantini ya kiafya kutokana na Covid-19, watu ishirini waliivamia nyumba ya Arunova Erkengul, wala hawakumruhusu hata kujistiri uchi wake. Na wakati wa upekuzi walipandikiza madaftari yenye maandishi na maelezo ambayo hayahusiani kamwe na yeyote katika wanawake hao waliokamatwa. Vikosi hivyo vya usalama viliwapekua dada zetu hawa wa Kiislamu kwa njia ya aibu na ya kudhalilisha na kuwaweka katika baridi na njaa kwa kati ya masaa 6 hadi 12 katika kituo cha kizuizi. Na huko, afya ya Baktybek kyzy Mahabat ilidhoofika na akapelekwa hospitali. Na pamoja na hivyo, bado angali kizuizini. Maafisa hao walimhoji bila huruma Mamirkanova Amangul kuanzia saa tisa mchana hadi baada ya saa sita usiku nyumbani kwake, huku akimfanyia uangalizi mtoto wake wa kiume aliyefikia umri wa miaka 4 aliyesibiwa na maradhi ya 'Down Syndrome' na ambaye hivikaribuni alikuwa amefanyiwa upasuaji wa moyo. Waliingia nyumbani kwake wakiwa wamevalia glavu chafu na wala hawakuzingatia uwekaji umbali wa masafa. Arunova Erkingul na Baktybek kyzy Mahabat watabaki kifungoni hadi uchunguzi ukamilike Pamoja na hivyo, hawajahojiwa hata mara moja katika kipindi cha mwezi mzima uliopita kwa sababu taasi ya gereza iko katika karantini ya kiafya. Kama ambavyo hawakuruhusiwa kuonana na jamaa zao. Endapo watapatikana na hatia ya mashtaka ya serikali, huenda wakakumbwa na miaka kadhaa gerezani.                                                       

Na katika jaribio lake la kutapatapa la kuupiga vita mwamko wa Uislamu ndani ya nchi yake na kuregesha usimamishaji wa utawala wa Mwenyezi Mungu (swt), Khilafah, serikali ya Kyrgyzstan imekimbilia kuchafua sura ya wabebaji da'wah na kuwatishia wanawake watukufu wa Kiislamu kwa minajili ya kuchochea hofu kutokana na da'wah hii ya kulingania Dini ya Mwenyezi Mungu (swt). Na pamoja na hivyo, hakika kampeni inayo endeshwa na nchi hii na chini ya maelekezo ya mabwana wa serikali yake Urusi na Magharibi, ni vita visivyo weza kushindika, kwa sababu ni vita dhidi ya Mola wa Walimwengu. Ulinganizi wa Uislamu wala wanawake wachaMungu wa Kiislamu sio ambao ni tishio kwa nchi hii, bali ni utawala wa kimabavu wa serikali hii ya kisekula na nidhamu yake iliyojaa ufisadi, utapeli na kufeli kiuchumi, na kushindwa kwake vibaya kukabiliana na janga la maambukizi ya Covid-19. Na tunaiambia serikali hii ya kikatili ya Kyrgyzstan, ambayo inatawala kwa vitisho na ukandamizaji, hakika uhalifu wenu dhidi ya wanawake watukufu wachaMungu wa Kiislamu nchini Kyrgyzstan kamwe hautafichika ulimwenguni, shida yao itafichulika kimataifa! Tunataka dada zetu hawa watukufu wachaMungu wa Kiislamu waachiliwe huru mara moja na kukomeshwa mateso ya mabinti wachaMungu wa Ummah huu nchini Kyrgyzstan!     

Tafadhali fuatilia kampeni kwenye link hizi hapa chini:

http://www.hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/kampeni/1038.html

na https://www.facebook.com/womenscmoht/

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

#FreeMuslimahsKyrgyzstan     #KırgızistanlıMüslümanKadınlaraÖzgürlük

#WaacheniHuruWanawakeWaKiislamuKyrgyzstan        مسلمات_قيرغيزستان#

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu