Jumapili, 15 Muharram 1446 | 2024/07/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  8 Jumada I 1442 Na: 016 / 1442 H
M.  Jumatano, 23 Disemba 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Hbari

Watoto wa Nigeria Watatishwa Mpaka Lini?!

(Imetafsiriwa)

Polisi wa Nigeria waliripoti mnamo Jumapili, 20 Disemba 2020, kuwa walinzi wa eneo hilo wamewaokoa makumi ya watoto wa shule ambao walitekwa nyara na watu wenye silaha katika jimbo la Katsina, kaskazini mwa Nigeria, baada ya vita vya bunduki. Msemaji wa polisi wa Jimbo hilo Gambo Isah, alisema kuwa watu wenye silaha waliwateka nyara watoto wapatao 80 Jumamosi wakati walipokuwa wakirudi katika kijiji cha Mahuta baada ya kuhudhuria sherehe. Tukio hilo lilitokea siku chache baada ya kuachiliwa kwa wanafunzi 344 ambao walitekwa nyara na watu wenye silaha kutoka shule moja ya bweni huko Kankara katika jimbo hilo hilo na kuzuiliwa kwa siku sita.

Polisi walisema watekaji nyara wenye silaha katika tukio la hivi majuzi pia waliiba ng'ombe 12 kutoka kijiji cha karibu cha Danbaure. Polisi hawakufichua zaidi juu ya vitambulisho vya washambuliaji hao au nia yao, huku wakiwataja tu kama "majambazi." Ikumbukwe kwamba wizi na mauaji ya ng'ombe na utekaji nyara vimekuwa uhalisia wa kila siku kwa watu wa kaskazini mwa Nigeria. Mashambulizi ya kijeshi na utekaji nyara yameenea kaskazini mwa Nigeria, ambapo watu wenye silaha, majambazi wasiojulikana na viongozi wa genge wanaofanya kazi katika eneo hilo aghlabu hutuhumiwa kutekeleza uhalifu huo. Makundi haya kwa weledi yanaiba ng'ombe na kuteka nyara kwa badala ya fidia, na kila wakati serikali hukataa kusalimisha kile ambacho magenge haya yanaamuru na kukubali kwao kulipa fidia, huku mgogoro ukiishia kwa kuachiliwa kwa baadhi ya wafungwa na wahalifu kukwepa uwajibikaji wowote, mashtaka au adhabu hadi wakati mgogoro unapojirudia tena na sura zake zote uchungu.

Amnesty International inasema kuwa zaidi ya watu 1,100 waliuawa na majambazi katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, kwa kuzingatia kushindwa kwa serikali kutoa amani na usalama na kushindwa kuwafikisha washambuliaji mbele ya sheria. Katika wakati ambapo watu wanatarajia kupelekwa kwa usalama zaidi na kutabanni sera za usalama za kuzuia uhalifu, serikali ya Nigeria imetabanni mkakati wa usalama kwa msingi wa kuweka vikosi katika sehemu fulani ili kuhifadhi maisha yao na kuwalinda wasitekwe nyara, ambapo imepelekea kuondolewa kwa vikosi vya jeshi kutoka maeneo ya vijijini ambayo yamekuwa hatari zaidi kwa mashambulizi, wanamgambo na majambazi.

Watu wamekuwa wavumilivu na serikali nchini Nigeria na ufisadi ambao umeharibu taasisi za serikali na kuwaacha na umasikini na kuwaacha wakitishiwa na njaa na utapiamlo. Walikuwa na subira na hali ya serikali kupuuza mambo yao na kuenea kwa magonjwa kati yao. Walikuwa na subira na ulaghai wa serikali juu yao na kueneza uongo, lakini wanawezaje kuwa na subira juu ya kutekwa nyara na kutishiwa wapendwa wao?!

Kukuza usalama, kueneza uhakikisho, na kudumisha amani na usalama ni miongoni mwa haki za kimsingi za raia na sio sahihi kuipa lakabu ya dola serikali ambayo haiwahakikishii watoto uwezo wa kwenda shule zao bila kuogopa magenge ambayo yanawahangaisha maisha yao mbele ya macho ya watawala.

Mtume (saw) amesema:                                              

«مَنْ أَصْبَحَ مِنْكُمْ آمِناً فِي سِرْبِهِ، مُعَافًى فِي جَسَدِهِ، عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ، فَكَأَنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا»

“Yeyote miongoni mwenu anayeamka, mwenye afia katika mwili wake, mwenye chakula cha siku yake, basi ni kama aliyeimiliki dunia nzima.” [Imesimuliwa na Al-Bukhari].          

Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hi.zat.one
Fax: Telefax
E-Mail: [email protected]

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu