Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  29 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: 1442 H / 042
M.  Jumamosi, 10 Julai 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 Ulengaji wa Raia ni Kuwatiisha Wanamapinduzi kwa Masuluhisho ya Mhalifu
(Imetafsiriwa)

Vikosi vya serikali vimeanzisha tena upya umwagaji wao wa mabomu viunga vya Hama na Idlib, Syria. Alfajiri ya Jumanne, walipiga mabomu maeneo ya Fleifel, Benin, viunga vya Kansafra, Al-Bara na Al-Fatirah huko Jabal Al-Zawiya, na maeneo ya jirani ya Qalidain na Al-Ankawi katika Uwanda wa Al-Ghab ulio kaskazini magharibi mwa kijiji cha Hama, huku ndege za uchunguzi za Urusi zikiruka juu ya eneo hilo.

Mnamo Jumamosi, 3/7/2021, mwanahabari mmoja wa Al-Jazeera nchini Syria pia aliripoti kwamba raia 9 - wakiwemo watoto 6 na watu wa familia nzima - waliuawa na wanachama 5 wa Ulinzi wa Raia walijeruhiwa kutokana na ulipuaji mabomu wa serikali na vikosi vya Urusi kwenye vitongoji vya makaazi katika vijiji na miji ya Jabal Al-Zawiya viungani mwa Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria.

Mauaji na uhalifu unaofanywa na serikali ya Syria na washirika wake, Urusi na Iran, hautakoma dhidi ya wale wanaokataa kufuata nyayo zao, hata ikiwa watawadhuru watoto, wazee na wanawake. Ulengaji huu wa mara kwa mara wa raia wasio na hatia hakuna uzito kwa hesabu za kibinadamu - hata kama unapatikana katika mipango yao ya kihalifu - lakini kila wakati unakusudiwa kupitisha makubaliano, mikataba na miradi inayotumikia serikali na mabwana zake, ili kufikia mafanikio ya kisiasa kwa gharama ya Mapinduzi ya Syria, ambayo inahitaji kukubalika kwa suluhisho la kisiasa la Amerika kwa msingi wa maridhiano na serikali na kurudi mikononi mwake huku ikiwalinda wauaji na kuwazuia kuhesabiwa kutokana na uhalifu wao wa kikatili.

Uhalifu huu unaoendelea dhidi ya watu wanaoasi wa Ash-Sham unathibitisha kwamba "jamii ya kimataifa" inayoongozwa na Amerika - ambayo inagawanya dori zake za kishetani kwa vyombo vyake na vibaraka wake - inahalalisha uwepo na umakinishaji wa serikali ya mhalifu Assad na kuipatia uhai, ili kuwaongoza watu wa Syria katika hali ya kukata tamaa na kukata tamaa hivi kwamba wakubali masuluhisho ya kikoloni yanayoamrishwa kwetu na maadui zetu.

Mauaji haya ni ushahidi wa hatari inayouzunguka Umma wa Kiislamu isipokuwa tu upate tena mamlaka yake kutoka kwa wanyakuzi wake. Nchi za Kiislamu lazima zitoe zitoe habari kuyahusu ili kuondoa dhulma hii na uvamizi kutoka kwa wasio na hatia na wanamapinduzi, ambao walitaka mapinduzi yawe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na walijitolea muhanga sana ili kuishi kwa heshima.

Umma wa Kiislamu, ambao ulilipia na bado ungali unalipia gharama nzito ili kuishi kwa usalama na amani, lazima ujue kwamba ushindi na fahari viko katika ukombozi wake kutoka kwa utawala wa Magharibi kafiri na kurudi kwenye sheria ya Mola wake na kuifanya kuwa ndio nukta maregeleo katika mambo mbali mbali ya maisha yake ili kumridhisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake; na kupelekea mabadiliko ya hali na mabadiliko katika mchezo wa kisiasa ambao utaregesha uongozi kwa Uislamu ili kurekebisha hali za wanadamu wote.

Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu