Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  20 Muharram 1443 Na: 1443 H / 003
M.  Jumamosi, 28 Agosti 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Musktakbali Mwema kwa Wanawake wa Afghanistan Utapatikana tu Chini ya Kivuli cha Nidhamu ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Kuchukuliwa tena kwa Afghanistan na Taliban kutabiriwa kufuatiwa na wimbi la madai na mafuriko ya utiaji hofu kutoka kwa serikali za Magharibi, watetezi wa usawa wa kijinsia na vyombo vya habari vya kiulimwengu kuhusu kile ambacho utekelezwaji wa hukmu za Shariah za Kiislamu kitamaanishwa kwa mustakbali wa wanawake katika nchi hii. Uongo na uvumi ni mwingi dhidi ya sheria ya Kiisilamu na madai kwamba ingeunda dola ambayo unyanyasaji dhidi ya wanawake ungeenea, wasichana kunyimwa elimu, na wanawake kunyimwa haki ya kufanya kazi na kujihusisha katika maisha ya kisiasa ya jamii yao. Kujibu desturi hii ya muda mrefu na mashuhuri ya ksekula ya Kiagharibi ya kubuni uwongo juu ya ukandamizaji wa wanawake chini ya Shariah, tunaangazia hoja zifuatazo:

1. Ni wazi kabisa kwamba serikali za Kimagharibi na sekta mbali mbali za vyombo vya habari vya kisekula hazijali lolote kuhusu ustawi na haki za wanawake na wasichana nchini Afghanistan, na kihakika hata wanawake wa Kiislamu katika nchi zote ulimwenguni. Kujali huku kulikuwa wapi wakati maelfu ya wanawake na wasichana wa Afghanistan walipokuwa wakiuawa, mamia ya maelfu zaidi walipokuwa wakifa kwa njaa na maradhi na wakitolewa makaazi yao, au kufanywa wajane wa vita waliolazimika kujitahidi kwa ajili ya maisha ya kila siku katika nchi ambayo uchumi, miundombinu, elimu na mfumo wa huduma ya afya yaliharibiwa kutokana na vita na uvamizi huu wa kikoloni wa Kimagharibi wa miongo miwili?! Na kujali huku kulikuwa wapi wakati serikali za Kimagharibi zilipokuwa zikiusaidia Muungano wa Kaskazini kuingia madarakani - genge la wababe wa kivita na rekodi mbaya ya uhalifu dhidi ya wanawake? Na je! Kujali huku kulikuwa wapi juu ya haki za wanawake wakati wasichana wa Kiislamu katika dola za kisekula kama Ufaransa, Ubelgiji, Denmark, na Uholanzi wanaponyimwa haki ya kupata elimu kutokana na marufuku ya hijab na niqab; au wakati wanawake wa Kiislamu katika tawala zinazoungwa mkono na Magharibi kama vile Kyrgyzstan, Uzbekistan na Bangladesh wanateswa, kufungwa na kunyanyaswa kwa kuzungumza dhidi ya ukandamizaji wa watawala wao au kwa kulingania tu Uislamu? Wanawake wa Kiislamu wanajua vyema rekodi ya kihistoria ya serikali za kisekula za Kimagharibi na vyombo vya habari vinavyotumia kadi ya haki za wanawake kuhalalisha uingiliaji wa kikoloni na kueneza maadili ya kiliberali ya kisekula katika nchi za Waislamu ili kupambana na kurudi kwa mfumo bora wa Kiislamu wa utawala, kwa lengo la kudumisha utawala wa Kimagharibi juu ya siasa na uchumi wa eneo hilo.

2. Wazo kwamba Afghanistan ilikuwa hadithi ya mafanikio kwa wanawake chini ya utawala na mfumo wa kisekula uliowekwa na Magharibi, na kwamba wanawake na wasichana sasa wana hatari ya kupoteza haki zao zile zinazoitwa "zilizopatikana kwa taabu" ni upuuzi! Mnamo mwaka wa 2011, utafiti uliofanywa na TrustLaw, huduma ya habari inayoendeshwa na wakfu wa Thomson Reuters Foundation, ambayo iliwahoji "wataalam wa jinsia" zaidi ya 200 ulimwenguni, iliiorodhesha Afghanistan kuwa nchi hatari zaidi ulimwenguni kwa wanawake kutokana na kiwango cha unyanyasaji, utoaji mbaya wa huduma za afya na viwango vya kikatili vya umaskini. Leo, Afghanistan inashika nafasi ya pili hadi ya mwisho katika ustawi wa wanawake kulingana na takwimu za 2019 zilizokusanywa na Taasisi ya Wanawake, Amani na Usalama ya Georgetown jijini Washington na Taasisi ya Utafiti wa Amani jijini Oslo. Kulingana na tarakimu za serikali ya Afghanistan za 2017, zaidi ya asilimia 50 ya wanawake wajawazito hawakupata huduma muhimu za afya. Ripoti ya 2019 ya UNICEF iligundua kuwa watoto 3.7 milioni hawakuenda shule nchini Afghanistan, na asilimia 60 yao ni wasichana. Shirika la Human Rights Watch limeripoti kuwa theluthi mbili ya wasichana nchini bado hawaendi shule na zaidi ya asilimia 40 ya shule zote hazina majengo. Na baada ya miaka 20 ya uvamizi wa Magharibi, zaidi ya asilimia 80 ya wanawake wamebaki hawajui kusoma na kuandika nchini, wakiongezeka hadi asilimia 90 katika maeneo mengine ya vijijini (UNESCO). Mangati ya kuondoa unyanyasaji wa wanawake chini ya uongozi na mfumo wa kisekula yameshindwa kabisa, sambamba na maisha ya wanawake wa Afghanistan, Iraq na nchi zengine ambazo zimeteseka na uingiliaji wa Magharibi.

3. Serikali za kisekula za Kimagharibi hazistahiki kufundisha juu ya haki za wanawake, wakati zinasimamia janga la ghasia, unyanyasaji wa kijinsia, unyonyaji, ulanguzi, umaskini na dhulma zengine na unyanyasaji dhidi ya wanawake ndani ya nchi zao kwa sababu ya maadili na nidhamu zao fisidifu na mbovu za huria za kirasilimali, ambazo zimeshusha hadhi ya wanawake, zimeidhinisha uendekezaji ngono wao na kuifanya kuwa chombo cha kujipatia faida, na kujenga fikra kwa wanaume wengi kwamba inakubalika kuwatendea wanawake vile wapendavyo. Nchini Amerika, wanawake 3 wanauawa kila siku kutokana na unyanyasaji wa kinyumbani (Afisi ya Sheria), na 1 kati ya wanawake 5 wamebakwa katika maisha yao (Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa). Thuluthi moja ya wanawake wote katika Muungano wa Ulaya wamepitia unyanyasaji tangu umri wa miaka 15 (Shirika la Muungano wa Ulaya la Haki za Msingi). Nchini Australia, mwanamke mmoja hulazwa hospitalini kila masaa 3 kwa sababu ya unyanyasaji wa kinyumbani (Taasisi ya Afya na Ustawi ya Australia). Na nchini Uingereza na Wales, wanawake 85,000 ni wahasiriwa wa ubakaji au jaribio la ubakaji kila mwaka (Afisi ya Takwimu za Kitaifa).

4. Taswira inayoundwa kuwa umati wa wanawake nchini Afghanistan wanaogopa utabikishwaji wa Shariah na wanataka mustakbali wa kisekula kwa ardhi yao ni upuuzi wa uwongo ulioundwa na wakoloni wa Kimagharibi. Ni mwendelezo wa ruwaza ya kiulimwengu ya watu wa mashariki na imani ya hadaifu kwamba Waislamu wa nchi za Waislamu wanapenda kuachana na Uislamu na kukumbatia maisha huria ya kisekula, na huitazama demokrasia ya kisekula ya Kimagharibi kama njia ya kuwakomboa kutokana na dhulma - uonevu ambao Waislamu ulimwenguni wanauona umesababishwa kimsingi na tawala na nidhamu za kisekula zilizoundwa na wanadamu zilizopandikizwa na kufadhiliwa na Magharibi, na sio kwa utawala wa Uislamu au utabikishaji wa Shariah. Wanawake wa Kiislamu wa Afghanistan na katika ulimwengu wote wa Kiislamu wana mshikamano mkubwa na imani, matendo na sheria zao za Kiislamu kama walivyokuwa kwa karne nyingi. Ripoti ya 2017 ya Waislamu - wanaume na wanawake - katika nchi 39 ya Shirika la Utafiti la PEW, iligundua kuwa asilimia 99 ya Waislamu nchini Afghanistan wanapendelea kuifanya Shariah ya Kiislamu kuwa ndio sheria rasmi katika nchi yao. Idadi kubwa zaidi katika nchi zengine za Kiislamu zikiwemo Pakistan, Bangladesh, Iraq, Misri, Indonesia, Palestina na Jordan pia iliunga mkono kutawala kwa Shariah ya Kiislamu. Hili ni la kutarajiwa, kwani Waislamu wanatambua kuwa ni Mola wa walimwengu (swt) Peke Yake ndiye anajua zaidi jinsi ya kuendesha jamii na dola ili kuhakikisha haki za wote - wanamume na wanamke - zinapatikana katika haki na usawa na kwa namna ya utulivu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 [أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ] “Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?” [Al-Mulk: 14].

5. Ni jambo linalojulikana vyema kuwa Uislamu uliongoza ulimwengu katika kuinua hadhi na utu wa wanawake na kuwalinda kutokana na unyanyasaji, pingamizi na unyonyaji hivi kwamba kitendo chochote cha kuwadhuru wanawake kimeainishwa kama jinai kubwa inayostahili adhabu kali. Kwa kuongezea, Uislamu ulikuwa mwanzilishi wa haki za wanawake kisiasa, kielimu, kiuchumi na kimahakama karne nyingi kabla Magharibi hata haijatambua kuwa wanawake walikuwa na roho na akili sawa na thamani sawa na wanaume. Hii ni pamoja na kuwapa wanawake haki ya kuchagua mtawala wao, kuwa mwakilishi aliyechaguliwa wa watu wao, na kuwahesabu wale wanaotawala bila hofu ya athari yoyote. Uislamu ulihimiza wanawake kutafuta maarifa na utaalamu katika nyanja zote za maisha, ikizalisha maelfu ya wasomi wa kike na wataalamu katika taaluma za Kiislamu, sayansi na tiba chini ya utawala wake. Uislamu pia uliwapa wanawake fursa ya kupatiwa mahitaji ya kila siku na waume zao, ndugu zao wa kiume au serikali, huku ikiwaruhusu pia kutafuta ajira yenye hadhi, kuanzisha biashara na kusimamia utajiri wao na mambo ya kisheria kwa uhuru na vile vile kutafuta suluhu ya kimahakama kwa ukiukaji wowote wa haki zao. Lakini, hadhi isiyo na kifani ya Uislamu, fadhila na haki ambayo huwapa wanawake hazitapatikana chini ya dola ya Kiislamu jina pekee, au ambayo inatabikisha sehemu tu Uislamu huku ikitembea katika njia ya kufeli iliyotandazwa vizuri ya kuchanganya Uislamu na sheria za kafiri au kugawanya mamlaka na wale watetezi wa ruwaza ya kisekula kwa nchi hii. Badala yake, ni utabikishaji kamili wa Shariah kupitia mfumo wa kweli wa Kiislam, Khilafah kwa njia ya Utume ndiyo itakayounda mustakbali mzuri, salama na ustawi kwa wanawake wa Afghanistan na katika nchi zote za Waislamu, kuwapatia haki zao walizopewa na Mungu, kama ilivyokuwa kwa karne nyingi, kama inavyothibitishwa na vitabu vya sheria na rekodi za kimahakama za dola ya Khilafah.

Kwa hivyo tunawasihi ndugu zetu katika Taliban na ndugu na dada zetu Waislamu nchini Afghanistan kujifunza kutoka kwa historia na kuzingatia maneno ya Mwenyezi Mungu (swt), kwamba mafanikio hapa duniani na kesho Akhera yanaweza kuwepo tu kupitia utabikishaji kamili wa Sheria za Mwenyezi Mungu (swt), chini ya mfumo wake yaani nidhamu ya Khilafah. Yeye (swt) asema:

 [فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى * وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

“Akasema: Ondokeni humu nyote, hali ya kuwa ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika. Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Ta-Ha: 123-124].

Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut Tahrir

#أفغانستان#Afganistan                      #Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu