Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 28 Jumada I 1443 | Na: 020 / 1443 H |
M. Jumamosi, 01 Januari 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wanawake Wanadhalilishwa na Kuteswa ndani ya Magereza ya Kiyahudi… Je, Yupo Mu’tasim katika Ummah Huu?!
(Imetafsiriwa)
Klabu ya Wafungwa wa Palestina ilithibitisha kuwa idara ya Gereza la Damon ilifanya operesheni za mateso mfululizo dhidi ya wafungwa wa kike, ambazo zilidumu kwa siku kadhaa na bado zinaendelea. Walipigwa sana, wakaburuzwa, na baadhi yao kujeruhiwa. Wawakilishi wa wafungwa wa kike, Shorouk Dwaikat, Marah Bakir, na mfungwa Mona Qaadan walitengwa. Klabu hiyo ya Wafungwa ilifafanua kuwa wakati wa mashambulizi hayo ya mara kwa mara, walikatiwa umeme na kuvuliwa hijab zao. Mmoja wa wafungwa hao wa kike alipoteza fahamu wakati wa mateso, na idara ya gereza inaendelea kuwatishia kwa kunyunyiza gesi ndani ya seli zao. Idara hiyo ya gereza haikuridhika na hili tu, kwani iliwapa adhabu ya pamoja dhidi yao, kuwanyima kwenda katika mkahawa wa gereza na kutembelewa, pamoja na kutoza faini za kifedha. Kwa mujibu wa Klabu ya Wafungwa, idadi ya wafungwa wa kike hadi kufikia mwisho wa Novemba ilifikia 32. Klabu hiyo ilieleza kuwa mchakato wa unyanyasaji unaofanywa na idara ya gereza ulifanyika baada ya wafungwa hao wa kike kukataa hatua mpya zilizotangazwa na idara hiyo dhidi yao.
Mashambulizi na mateso haya ya wafungwa wa kike katika magereza ya umbile la Kiyahudi yanaibua hofu juu ya mateso ya wafungwa wa kike katika jela za umbile hili la kihalifu, ambalo halitofautishi kati ya vijana na wazee, mwanamume na mwanamke katika uhalifu wake. Linawatesa wafungwa wa kike na kuwashambulia ndani na nje ya magereza. Umbile hili limevuka mipaka kiasi kwamba walinzi wake walithubutu kuwatusi wafungwa wa kike wasio na silaha na kuwavua hijabu zao, La Hawla Wa La Quwata Ila Billah (hakuna uwezo wala nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu). Uhalifu na dhuluma zote hizi zinafanyika na hatusikii sauti kutoka kwa mashirika ya wanawake na watetezi wa CEDAW. Wafungwa wa kike si miongoni mwa vipaumbele vyao, na hawako katika ajenda ya mfadhili ambaye huwaamuru kile watakachozungumza, na mipango gani ya kifisadi waitekeleze.
Mashambulizi haya yanatosha kufanya damu ichemka katika mishipa ya Umma wa Kiislamu na kuukumbusha wajibu wake kwa Masra (mahali pa Israa) ya Mtume wake (saw), na kufanyia kazi ukombozi wake na ukombozi wa wanamume na wanamke wafungwa katika magereza ya umbile la Kiyahudi. Mamlaka ya Palestina na tawala katika ardhi za Kiislamu zimeshindwa, zinafanya njama na kukimbilia kusawazisha mahusiano yao na umbile la Kiyahudi; hakuna matumaini kwao kuwakomboa au kuwasaidia wanyonge. Na tuna yakini kuwa watu wako katika kambi moja na watawala wao wako katika kambi nyengine.
Umbile la Kiyahudi lisingethubutu kufanya uhalifu huu kama Waislamu wangekuwa na dola inayotawaliwa na mtawala mithili ya Al-Mu’tasim, ambaye alitayarisha jeshi kubwa kujibu kilio cha mwanamke mmoja wa Kiislamu aliyetekwa na Warumi. Dola inayofanya kufunua uchi (awra) wa mwanamke wa Kiislamu au kuvua hijabu kuwa ni kosa lisilosameheka, na adhabu yake ni kubwa, kama alivyofanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipowafurusha Bani Qaynuqa’ kutoka Madina; dola ambayo inalinda ardhi na heshima, na haikubali kuzisalimisha.
Enyi Majeshi ya Kiislamu: Ni nani kati yenu atakayepata heshima hii kuu? Heshima ya kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu na kuwanusuru wafanyi kazi wanaotaka kuipandisha daraja ya juu kabisa, kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, kama alivyoipata Sa'ad bin Muadh, ambaye kwake kiti cha enzi (Arsh) ya Mwingi wa Rehema alitetemeka kutokana na kifo chake? Na jueni kuwa kesho mtakutana na Mwenyezi Mungu (swt), na atawahisabu kwa kufeli kwenu kuwanusuru wanyonge na kuitikia vilio vyao, basi je mmetayarisha jibu la siku hii?!
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |