Jumanne, 06 Dhu al-Hijjah 1443 | 2022/07/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  17 Dhu al-Qi'dah 1443 Na: 1443 H / 037
M.  Alhamisi, 16 Juni 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Onyo la Njaa Kubwa Barani Afrika na Uingizaji Siasa Mateso ya Wanawake na Watoto
(Imetafsiriwa)

Rais wa Muungano wa Afrika, Rais wa Senegal Macky Sall alisema katika taarifa kwa Radio France International kwamba Afrika itakabiliwa na njaa mbaya sana, ikiwa usafirishaji wa ngano kutoka Ukraine hadi barani hautaregelewa. Sall alisema, wakati wa taarifa zake kwamba njaa "inaweza kuyumbisha bara." Akizungumzia mkutano wake wa wiki iliyopita na Rais wa Urusi Putin jijini Moscow, alisema alimwomba Putin kuisaidia Afrika kupata mbolea na nafaka. Matamshi haya yalitanguliwa na kauli kadhaa za wanasiasa wa nchi za Magharibi wakihusisha vita vya Ukraine na msukosuko wa chakula barani humo, hasa kauli za Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) kwamba “kusema kwa ufupi, vita barani Ulaya, Ukraine, vinatafsiriwa kuwa njaa barani Afrika,” na kauli ya rais wa Ufaransa, “Tunatarajia njaa barani Afrika kwa sababu ya vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.” Kauli hizi, kwa ujumla wake, hazikuwa chochote ila chombo cha propaganda kati ya Urusi na Magharibi. Urusi ilikutana na taarifa hizi za kushangaza za nchi za Magharibi kwa shutma za moja kwa moja kwamba vikwazo vya Magharibi vilizidisha janga la chakula na kufunga maduka ya nafaka na mbolea.

Wakati wanasiasa wakilaumiana wao kwa wao kwa kupatiliza mateso ya binadamu kama silaha ya vita, taswira ya miili ya Waafrika iliyodhoofika na kina mama walio na huzuni imeregea katika vichwa vya habari, kama vile matukio ya watoto wenye utapiamlo katika pwani ya Afrika au Afrika Mashariki, kana kwamba picha ilikuwa haijabadilika na wakati ulikuwa umesimama katika mandhari ile ile ya kusikitisha miongo kadhaa iliyopita. Nyuso ni zile zile, na ulimwengu unasimama bila hatua yoyote mbele ya kambi za njaa na msaada zinazotarajiwa ambazo wengine huzifikia baada ya safari ndefu kwa miguu, huku wakizika watoto na wazee wao waliokufa. Hii inafanywa ndani ya muundo wa uangaziaji wa vyombo vya habari ambao unaingizwa siasa katika umbo na maudhui na hauna uhusiano wowote na wanadamu. Licha ya uzito wa hali hiyo na taarifa nyingi zinazosikika, kuna upungufu mkubwa wa ufadhili wa mpango wa dharura wa Umoja wa Mataifa kwa nchi zilizoathirika. Taarifa ya pamoja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa (WFP, FAO, na UNICEF) ilisema kwamba "asilimia 18 tu ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana na hali ya kibinadamu nchini Somalia kwa mwaka 2022 ndio umefadhiliwa."

Mbali na milipuko ya kisiasa, Oxfam na Save the Children wameielezea hali ya Afrika Mashariki kuwa ni ya janga, na kubainisha kuwa mtu mmoja hufariki kwa njaa kila baada ya sekunde 48, na njaa hiyo inadhihirisha kufeli mara kwa mara kwa duniani kuepusha majanga yanayoweza kuzuilika.

Tunasimama tena mbele ya uhalisia mchungu ambapo watu wa Bara lenye rutuba la Afrika, tajiri kwa maliasili yake na hali ya hewa ya hali ya juu, hawawezi kupata riziki yao ya kila siku, na kadhia zao nyeti zinatumiwa katika mikataba duni, na wanalipa thamani ya vita vya kirasilimali ambavyo hawana mkono ndani yake.

Suala la usalama wa chakula barani Afrika na kwingineko halitengani na kufikia usalama kwa watu, na haliwezi kuachwa mikononi mwa nchi nyingine, zikilitishia wakati mmoja na kujadiliana nalo wakati mwingine. Wala isiachwe mikononi mwa mashirika ya kimataifa ambayo yanahesabiwa kuwa sehemu kuu ya tatizo, kwani yamefuata sera zilizoharibu uchumi wa nchi na kuweka utiifu na utegemezi kwa wengine. Hizi ni sera zinazowataka wananchi kutumia na kuagiza bidhaa kutoka nje badala ya kuzalisha na kufufua ardhi na kuelekeza kilimo ovyo ovyo katika kutafuta faida ya haraka hivyo kuuchosha udongo bila mafanikio yoyote. Chanzo cha ugonjwa huu sio bei ya juu na ngano ya Urusi wa Ukraine, lakini ni sera hizo zenye kupuuza ardhi na mazao ya ndani, kuzinasibisha riziki za watu na maeneo ya ng’ambo, kuzalisha mazao maalum na kuwalazimisha watu kuagiza ngano kutoka nje, huku tukipuuza kilimo cha kienyeji.

Kwa miongo kadhaa, Afrika imekuwa ikikabiliwa na umaskini wa fikra, akili na utashi wa kisiasa. Ardhi yake imedhulumiwa kinyama, na watu wake wanakufa kikatili kwa njaa. Afrika haina njia ya kutoka isipokuwa kwa kuifurusha Magharibi na mashirika yake yaliyoifukarisha nchi na kuanzisha majanga matatu, umasikini, ujinga na maradhi. Na haina njia ya kutokea isipokuwa ikiwa watu wake watalima ardhi yao yenye rutuba na kula kile inachokiotesha na kuachana na masuluhisho hadaifu yatokayo nje yaliyoifukarisha nchi na watu. Lakini haiwezekani kwa hili kutokea, isipokuwa kwa kukabiliana na mgogoro wa utawala na kutambua uhalisia wa ukhalifa ardhini.

 [أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ خُلَفَاءَ الْأَرْضِ أَإِلَـهٌ مَّعَ اللَّـهِ قَلِيلاً مَّا تَذَكَّرُون]

Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayo yazingatia.” [An-Naml: 62]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu