Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 12 Muharram 1444 | Na: 1444 H / 003 |
M. Jumatano, 10 Agosti 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Gaza iko Peke Yake Huku Kukiwa na Mashambulizi, Njama na Usaliti
(Imetafsiriwa)
Matokeo ya mashambulizi ya umbile la Kiyahudi kwenye Ukanda wa Gaza wakati wa mashambulizi yaliyopita yalikuwa ni mashahidi 45 na mamia ya waliojeruhiwa, wakiwemo watoto 15 na wanawake 6.
Matukio ya mashambulizi, upigaji mabomu, mauaji na uharibifu yanarudiwa rudiwa katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa kwa zaidi ya miaka 16, na ulimwengu unatazama hili kwa ukimya wa bubu na usaliti kutoka kwa wale walio karibu na mbali.
Shambulizi hili linajiri katikati ya uungaji mkono wa Magharibi, haswa kutoka Marekani, na njama na mapuuza ya Waarabu kupitia kukimbilia kwao kuhalalisha mahusiano na Mayahudi katika sura na nyanja zake zote, pamoja na utiifu wa mamlaka katika uratibu wake wa usalama na kuridhika na kauli za kioga na kuomba (uingiliaji kati wa) Umoja wa Mataifa na Baraza lake la Usalama.
Watawala makhaini, vibaraka wa Magharibi na watumwa wa viti vyao (viti vya utawala), wanawatazama wahasiriwa, wakiwemo wanawake na watoto, wasio na uhalifu wowote isipokuwa tu kwamba wako Gaza bila ya mlinzi, msimamizi, au kiongozi anayemcha Mwenyezi Mungu ndani yao. Bali, baadhi yao hujifanya kuwa na hofu kwa wahasiriwa na kujadili "kusitishwa kwa mapigano" kana kwamba kuna mapambano sawa kati ya vikosi viwili na sio mashambulizi ya kikatili na dhulma dhidi ya watu wasio na ulinzi wowote.
Enyi Majeshi ya Waislamu: Hatutaacha wala hatutachoka kuwalingania muwanusuru dada zenu na watoto wenu nchini Palestina. Matumaini yetu ya mwitikio wenu kwa wito wa kina mama wanao omboleza hayatafifia, kwa hiyo msiyazibe masikio yenu kwa kilio cha dhulma, huzuni na hofu wanacholia watoto, wanawake na hata wanaume huku wakikabiliana na zimwi hili halifu peke yao; lenye huhisi kinga kutokana na dhidi ya adhabu ya watawala na viongozi wenu, na kuongeza mauaji yenu.
Enyi Maafisa na Askari wa Majeshi: Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Kitabu chake Kitukufu:
[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]
“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal: 72]. Al-Aqsa, Iliyobarikiwa, Al-Quds, wanawake na watoto wa Gaza na Palestina yote wanaomba msaada na kulilia heshima kwenu, basi musiwaangushe na kutoa kafara damu yao kwa ajili ya viti vya enzi vya watawala na viongozi vibaraka wenu.
Mwenyezi Mungu (swt) pekee ndiye atakunusuruni, na Mwenyezi Mungu (swt) pekee ndiye atakuhisabuni, atalipa wema kwa wema na adhabu kwa makosa. (Watawala na viongozi) hawa waliomkhini Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, Dini na Ummah hawatakunufaisheni wala kukunusuruni.
[إِن يَنصُرْكُمُ اللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُم وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ]
“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Al-i-Imran: 160] Hivyo, je mutaitika?
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |