Jumapili, 15 Muharram 1446 | 2024/07/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  19 Muharram 1444 Na: 1444 H / 004
M.  Jumatano, 17 Agosti 2022

 

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuenea kwa Mauaji ya Wanawake
(Imetafsiriwa)

Mauaji ya wanawake wadogo yanaendelea. Watu hujishughulisha na sababu na dhurufu za uhalifu mmoja hadi uhalifu mwengine utakapotekelezwa. Matukio ya kikatili yaliwafanya watu washangae kuhusu sababu za vurugu hili la kupindukia, na kuwafanya wadai kutekelezwa kwa aina za juu zaidi za adhabu kama zuio. Wakati huo huo baadhi ya mashirika ya kiraia na haki za binadamu yalitoa taarifa ya pamoja ambapo yaliuliza: "Je, haki ya kuishi imekuwa takwa gumu kwa wanawake na wasichana katika nchi ya Misri?" na kusisitiza haja ya kuharakisha utoaji wa sheria ya unganishi ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake, ambayo ni sheria iliyoainishwa kwenye Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Ukatili Dhidi ya Wanawake 2015-2020, lakini bado ingali haijatolewa.

Ripoti za vyombo vya habari zikilaani kile walichokiita kuenea kwa unyanyasaji dhidi ya wanawake ziliendelea nchini Misri na nchi nyenginezo, huku neno "mauaji ya wanawake" likienea katika jaribio la kuangazia mawazo ya utetezi wa wanawake na kile wanachokiona kama uadui wa kiasili kati ya wanaume na wanawake. Vyombo vya habari kwa makusudi vimepuuza fahamu ambazo jamii za nchi zetu zinabeba ambazo zinatatua mzizi wa suala hilo, kiasi ya kuwa yeyote anayemuua mtu bila kosa ni kana kwamba ameua wanadamu wote bila kujali muuaji au aliyeuawa ni mwanamume au mwanamke. Wala ripoti za vyombo vya habari hazikuzungumzia ukandamizaji wa kisiasa na wa kiuchumi na ukandamizaji wa kibinadamu wa vijana wa jinsia zote katika nchi za Kiislamu.

Vyombo vya habari vinacheza dori kubwa katika kueneza na kukuuza jinai hizi na kujaribu kuzichafua jamii katika nchi za Kiislamu. Uhalifu huo ulipigwa picha na kuchapishwa kwa muda mfupi bila kuzingatia matukufu, na katika uchapishaji huu wa dhurufu za kudungwa kisu msichana mmoja kwa mapigo kumi na saba, kuchinjwa kwa mwengine mchana peupe mbele ya lango la chuo kikuu, na wa tatu kuburuzwa chini baada ya kupigwa vibaya sana. Hili linavunja kizuizi cha kisaikolojia cha mpokeaji, ambacho kinaweza kuchangia kuenea kwa uhalifu, na sio kuupunguza.

Wanawake wa Kiislamu hawajaona uadilifu wowote tangu fikra na fahamu za Kimagharibi zilipotua katika ardhi zetu. Wanawake hawaonekani tena kama kina mama, kina dada, na heshima ambayo lazima ilindwe. Badala yake, kwa mujibu wa fahamu za Kimagharibi, wamekuwa bidhaa ambayo vyombo vya habari na mabepari wanairusha huku na kule. Hii iliudhalilisha utu wake na nafasi inayomstahiki. Badala ya maisha ya ushirikiano kati ya wanaume na wanawake katika jamii ili kuijenga na kuiinua, ushindani na uhasimu ukawa tishio kwa uhusiano baina yao, na mizani ya kijamii imevurugika, na wanawake sasa sio tena dada za wanaume, kama alivyosema Mtume (saw), na kanuni ya jamii sio tena watendeeni wema “Qawareer” (wanawake).

Shina la maafa katika nchi za Kiislamu ni kukosekana kwa fahamu za Uislamu katika kudhibiti uhusiano kati ya wanaume na wanawake (au mfumo wa kijamii katika Uislamu), na haya ni matokeo ya kimaumbile ya kukosekana mifumo ya Kiislamu katika jamii na kukosekana kwa fahamu za Uislamu katika nyanja mbalimbali za maisha. Haiwezekani kwa wanawake kufurahia usalama na amani kupitia fahamu za msituni zinazofungamanishwa na fikra za mfumo wa kirasilimali wa Kimagharibi unaotawala ardhi za Waislamu. Kwa hivyo, usalama kamili kwa wanawake na wanaume utakuwa chini ya mfumo wa kifikra unaofungamanisha rehma ya Muumba wa wanadamu kwa wanadamu, mwanamume na mwanamke, inayotabikishwa na Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Hili ni rahisi kwa Mwenyezi Mungu (swt) kulifanya.

[يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالاً كَثِيراً وَنِسَاءً وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيباً]

“Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni.” [An-Nisa: 1]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hi.zat.one
Fax: Telefax
E-Mail: [email protected]

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu