Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  4 Rabi' I 1444 Na: 1444 H / 010
M.  Ijumaa, 30 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kipindupindu Kinawaua Watu wa Syria, Hivyo Iko Wapi Dola ya Kuwanusuru?!
(Imetafsiriwa)

Wizara ya Afya ya Utawala wa Syria ilitangaza mnamo Jumatatu kuwa mkurupuko wa kipindupindu katika maeneo kadhaa umewauwa watu 29, vifo na majeruhi vilikolea katika jimbo la kaskazini la Aleppo, ambapo watu 25 walithibitishwa kufariki, na maelfu kadhaa ya visa vinavyoshukiwa kuripotiwa kote nchini kuanzia Septemba 19, kulingana na data iliyopatikana na chama cha misaada kutoka Kitengo cha Afya cha Serikali ya Syria (GoS), Idara ya Kibinafsi ya Mamlaka ya Afya ya Mitaa, Kaskazini na Mashariki mwa Syria. Haya yametokea baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza, mwezi huu, kwamba mkurupuko huo unaaminika kuhusishwa na kumwagilia mimea maji machafu na kunywa maji yasiyo salama kutoka Mto Furat, unaovuka Syria kutoka kaskazini hadi mashariki.

Maafa na mateso yaliyosababishwa na vita vya Syria ni mengi, kwani viliharibu karibu nusu ya vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu, uliosababisha uhaba wa rasilimali za maji katika maeneo mengi yaliyoathiriwa. Jambo hili limewasukuma watu wengi kutegemea maji yasiyo salama jambo ambalo liliharakisha kuenea kwa magonjwa na majanga ya maambukizi, na hilii ni dhahiri kupitia ugonjwa wa kipindupindu ambao umewaambukiza hasa watu wa Aleppo, ambayo ni ngome kubwa zaidi ya wapinzani wa utawala huo. Haya bila kusahau uhalifu unaolenga maeneo ya watu wengi, ambapo maelfu ya watoto, wanawake, vijana na wazee waliuawa, na kuwanyima maelfu ya wanafunzi kuendelea na masomo yao, kutokana na kulengwa kwa shule zao au kuhamishwa kutoka kwa makaazi yao, ikiongezewa na kusababisha ukosefu wa usalama wa chakula na kuenea kwa njaa na utapiamlo miongoni mwa maelfu ya watoto.

Madai ya mashirika, yanayojiita ya kibinadamu, kushughulikia hali ya kibinadamu nchini Syria siyo ya kweli. Hayakusudii kupunguza mateso ya watu wake, kama ambavyo hayakusudii kupunguza jukumu la moja kwa moja kutoka kwa utawala wa kihalifu wa Baath na kutoka kwa wale ambao mikono yao pia ilitiwa doa na vita hivi vya kinyama ambavyo dola kubwa zilivitangaza dhidi ya watu wa Ash-Sham walioasi dhidi ukandamizaji na dhulma. Ni wazi kuwa nchi za kibepari hazina nia ya dhati ya kuwaokoa Waislamu nchini Syria, hali kadhalika hazina nia ya kuwaokoa Waislamu wa Yemen, Myanmar, Palestina, Kashmir na nyenginezo kwani kwa mujibu wa vipimo vyao vibovu vya kirasilimali, hakuna faida ya kisiasa wala ya kiuchumi itakayopatikana kutokana na kusitisha au kukomesha mauaji ya watoto na raia wasio na ulinzi.

Enyi Waislamu: Kama mjuavyo, hivi sasa kuna janga la kibinadamu linaloundwa na watu linaloathiri watu wetu nchini Syria, kwani maji yanaweza kuchafuliwa na watu kutokana na nyenzo zinazotumika katika viwanda na kilimo, kama vile vyuma vizito mithili ya risasi na zebaki, na kemikali na misombo hatari kama vile dawa za wadudu na mbolea. Yanaweza pia kuchafuliwa kutokana na nyenzo za kiasilia, kama vile madini ya arseniki au pathojeni kama vile bakteria, virusi na vimelea kama vile viumbe vyenye seli moja na funza. Ikiachwa bila kutibiwa, uchafuzi huu unaweza kusababisha magonjwa mbalimbali, ambayo yataleta madhara makubwa kwa afya ya binadamu. Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, zaidi ya watu bilioni moja kote ulimwenguni wanakosa maji safi ya kunywa, na angalau watu milioni nne, wengi wao wakiwa watoto, hufa kila mwaka kutokana na magonjwa yanayotokana na maji machafu ya kunywa, kama vile homa ya matumbo, kipindupindu, kichocho, kuhara damu na magonjwa mengine ya kuharisha.

Hivyo basi, kwa mujibu wa kanuni (qaida) pana ya kisheria inayosema kuwa kusiwe na madhara, na kwa mujibu wa Hadith zinazoharamisha kuchafua maji ya umma ambayo ni mali ya Waislamu wote, ni wajibu wa dola kutunza usafi wa vyanzo vya maji na kufuatilia ubora wa maji ya kunywa na kuhakikisha kuwa hayana vichafuzi. Lakini iko wapi hiyo dola yenye kunusuru kwa haki?!

Ndio, hii ndiyo hali ya Umma wa Kiislamu kwa kukosekana dola inayochunga na kutetea mambo yake, na Ummah huu utaendelea kubakia katika mporomoko wake mpaka ujue kuwa wokovu wake ni kwa kupitia kuifahamu dini yake na kwa kupitia kuitekeleza maishani, kupitia kusimamisha dola yake inayotabikisha hukmu na kanuni za imani yake, Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

(وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ)

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum:4-5]

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu