Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  7 Rabi' II 1444 Na: 1444 H / 017
M.  Jumanne, 01 Novemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Shambulizi juu ya Khimar (Kitambaa cha kichwa) barani Ulaya ni Vita vya Hadhara Dhidi ya Hadhara

"Jibu kwa Makala ya Jean Chichizola"
(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 11/09/2022, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kiliwasilisha mjadala kuhusu "Shambulizi dhidi ya Hijabu barani Ulaya", ambapo washiriki walizungumza kuhusu vikwazo ambavyo wanawake wa Kiislamu katika nchi za Magharibi wanakumbana navyo, ambao ulimkasirisha mwandishi wa habari Jean Chichizola kiasi kwamba aliandika makala yaliyochapishwa mnamo tarehe 19/10/2022 kwenye Gazeti la Le Figaro, yenye kichwa "Ufaransa inatuhumiwa kutaka "kuuondoa Uislamu" kwa vijana wa Kiislamu. Katika makala haya, mwandishi alikashifu mazungumzo yanayoendelea na akayakadiria yaliyomo ndani yake kama ukiukaji wa "Dola ya Voltaire", akijua kwamba mwanafalsafa na mwandishi Voltaire alikuwa maarufu kwa utetezi wake wa uhuru, haswa uhuru wa imani. Makala hayo yalionyesha kutojali kabisa maadili ya kuripoti habari na taarifa yanayoamriwa na taaluma ya mwandishi wa habari na kugonga nguzo zake muhimu - kutopendelea na usawa - kuanzia kichwa chake hadi sentensi ya mwisho ya makala hayo.

Sisi katika Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunamjibu kama ifuatavyo:

Kwanza: kwa mwandishi wa habari, uliyapa makala yako kichwa ambacho kina upendeleo na tuhma. Hii ni kwa kuwa na upendeleo kwa nchi ya Ufaransa, na kuifanya kuwa haina hatia kwa kile kilichohusishwa nayo, na kuwatuhumu washiriki wanawake, ambao wanawakilisha Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kwamba wao na chama chao walishambulia “Dola ya Voltaire” ambayo inadhamini uhuru, na walisubutu kuituhumu kuwatenga vijana wa Kiislamu kutoka katika dini yao ili kulazimisha mawazo yake ya kisekula juu yao, ili wachangamane kikamilifu na hadhara ya Kimagharibi. Je, ni kweli haina hatia kwa yale ambayo yamehusishwa nayo?

Je, Ufaransa haikupiga marufuku vazi la hijab mwaka wa 2004 katika mashule, shule za sekondari na shule za upili za umma, na kuzuia wafanyikazi wa kike katika taasisi za serikali kuivaa?! Je, haikupiga marufuku niqab katika maeneo ya umma mwaka wa 2010?! Je, nyanja haramu ya matumizi ya sheria ya mwaka 2004 haikupanuka na kujumuisha makosa mengi, kama vile kuzuia wazazi wengi wa wanafunzi wa kiume na wa kike kuingia katika taasisi za elimu na kuwazuia wanaovaa hijab kwenda kwenye baadhi ya vituo vya umma kupata huduma maalum? Je, haikufikia kiwango cha kesi za mara kwa mara za kufukuzwa shule baadhi ya wasichana wa Kiislamu wanaovaa nguo ndefu, au sketi ndefu inayofunika miguu?

Ilionekana wazi kwamba utekelezaji wa “sheria ya kupiga marufuku kuvaa alama za kidini” ulikuja kimsingi kuwawekea vikwazo Waislamu na haukuelekezwa kwa madhehebu mengine ya kidini, kama wanavyodai. Hii bila kusahau rasimu ya sheria zinazowekwa mara kwa mara za kupiga marufuku uvaaji wa hijab katika vyuo vikuu na kuzuia kina mama wanaovaa hijab kuandamana na watoto wao katika safari za shule, na kujaribu kulazimisha marufuku katika sekta ya kibinafsi, na hivi karibuni rasimu ya sheria ya kupiga marufuku hijab katika mashindano ya michezo! Hata mavazi ambayo si ya Kiislamu kwa viwango vya Sharia, kama mavazi ya michezo na burkini, walipigana nayo kama yenye kupiga vita maadili ya Kifaransa. Kwa upande mwingine, kwa kuzingatia mgogoro wa gesi nchini Ufaransa, mabwawa ya kuogelea yalilazimisha mavazi ya mwili mzima mithili ya burkini ili kupunguza dharura za afya kutokana na kuzima joto!

Hiki ndicho kidokezo cha vitendo vya "Dola ya Voltaire" kwa wanawake wa Kiislamu, ambayo yamechangia pakubwa kukua kwa chuki dhidi ya Uislamu na kuongezeka kwa idadi ya mashambulizi dhidi ya Waislamu huko, jambo lililowafanya baadhi ya watumaji wa Twitter kuitaja nchi hiyo ya uhuru kama "nchi ya taa zilizozimwa ulimwenguni." Katika taarifa yake tarehe 29/1/2021, Mkuu wa Kitengo cha Kitaifa cha Uchunguzi dhidi ya chuki kwa Uislamu nchini Ufaransa, Abdallah Zekri, alitangaza kuwa nchi hiyo ilishuhudia kesi 235 za mashambulizi dhidi ya Waislamu mwaka 2020, ikilinganishwa na kesi 154 mwaka 2019, ambayo ni ongezeko la karibu 53%.

Je, nchi ya uhuru haikufunga misikiti na jumuiya za Waislamu?! Je, haikufanya iwe vigumu kwa Waislamu kuishi?! Je, sheria ya kupambana na kile kinachoitwa "utengano wa Kiislamu" haikurasimiwa ili vijana wa Kiislamu waachane na Uislamu wao au waishi na hatia kwa sababu dini yao ni Uislamu? Licha ya hayo yote hapo juu, mwandishi huyu wa habari anakuja kusema kwamba Ufaransa inatuhumiwa, licha ya kwamba Macron alisema kwa waziwazi: kwamba sheria hii ilikuja kama "uimarishaji wa maadili ya kijamhuri" na kushughulikia ujenzi wa mfumo anaouona kuwa sambamba. Katika makala yake, mwandishi anashangaa kwa nini mazungumzo ya makundi ya Kiislamu hayakomei kwenye lahaja ya laïcité na Uislamu. Mwandishi anashangaa kuwa wanawake wanne waliovalia hijab walitangaza moja kwa moja na kulaani vikali pendekezo lililotolewa na kamati maalumu ya kupiga marufuku hijab katika shule za msingi za Denmark, kuhitimisha kwamba Ufaransa pia inalengwa na Hizb ut Tahrir. Kisha akataja misimamo ya uhasama ya hizb dhidi ya Ufaransa licha ya kupigwa marufuku kwa shughuli zake huko, na akakemea maelezo yaliyotolewa na mwanachama wa Kitengo cha Wanawake (cha Hizb ut Tahrir) kwamba sera ya Ufaransa ni udikteta na ukosoaji wake wa umbile la ufashisti la serikali hiyo ya kisekula. Mwandishi wa habari huyu anajigamba kuwa nchi yake imeizuia Hizb ut Tahrir kufanya kazi kwa sababu ya misimamo yake mikali, na wakati huo huo anafichua dhulma na kutengwa kunakotekelezwa na "Dola ya Voltaire", kama anavyoiita, dhidi ya wale wanaoipinga na kuwaona kama tishio kwa hadhara yake.

Pili: Ni wajibu wa mwandishi wa habari muadilifu kuchunguza ukweli na kufikisha habari na habari za kweli na sahihi, na wala asitoe hukumu za haraka-haraka au za dhulma au kuficha msimamo wa upendeleo humpotosha mshikaji wake kutokana na uaminifu na heshima ya taaluma yake. Mwandishi wa habari huyu aliielezea Hizb ut Tahrir - chama hiki kitukufu - kwa yale ambayo haihusiki nayo na akaikashifu. Hizb ut Tahrir kamwe haichipuzi kutoka kwa Ikhwaan Al-Muslimin, bali ni chama cha kimfumo kilichoanzishwa tangu miaka ya hamsini, na kina lengo madhubuti, ambalo ni kusimamisha dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume na kuwakusanya Waislamu chini ya bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na kwa sababu haikugeuka au kubadilika, na kwa sababu inaendelea kwa mstari madhubuti, imewaudhi wengi wa wale ambao wamekata tamaa katika kuihami hadhara ya Kimagharibi. na kuichukulia fikra yake kuwa ni yenye msimamo mkali. Wengine waichukulia kuwa shirika la kigaidi licha ya yakini yao kwamba ni chama ambacho hakikutabanni na wala hakitabanni kazi ya kisilaha, bali ni chama cha kisiasa kinacho pambana dhidi ya fikra fisidifu na kupambana na sera ovu na angamivu.

Hizb ut Tahrir pia imewatia wasiwasi wazungumzaji wengi wanaofanya kazi kwa ajili ya hadhara hii tawala ya Kimagharibi, ambayo hubadilika rangi kulingana na maslahi ya mfumo wa kisekula wa kirasilimali. Hizb ut Tahrir imemfanya mwandishi wa habari kama huyo na wale wanaosimamia utawala wake usio na nguvu kukosa usingizi, na kutekeleza viwango na kinyume chake kulingana na maagizo ya maslahi na malengo yao. Aliikashifu hizb kuwa ni miongoni mwa makundi ya Kiislamu yanayofadhiliwa na kuungwa mkono na Tume ya Ulaya; huu ni uwongo na kashfa. Hizb ut Tahrir haingii chini ya duara hili la kutia shaka. Hii ni kwa sababu ni kundi safi lililomuahidi Mwenyezi Mungu (swt) kutii na kufanya kazi ya uaminifu. Inakubali kheri pekee na haipokei msaada wa kifedha isipokuwa kutoka kwa wale wanaobeba ulinganizi wake.

Tatu: Mwanahistoria na mwanafalsafa Mfaransa Marcel Gauchet, mwandishi wa mojawapo ya utafiti muhimu zaidi juu ya hali ya kidini nchini Ufaransa, asema hivi katika kitabu chake La Religion En La Democracia [Dini katika Demokrasia]: “Usekula katika nchi za Magharibi kwa jumla umeacha kuwa na maana ya kisiasa inayokubalika,” na katika maelezo yake ya sababu za mshangao wa Waislamu wanaoishi nchini Ufaransa, na sababu za mashambulizi ya mara kwa mara ya Wafaransa na ya umma dhidi ya hijab, Gauchet anaamini kwamba yote haya yanajiri ili kutoa mwelekeo wa mapambano dhidi ya usekula na kuupa uhai ambao usekula wa Ufaransa ulikosa baada ya kupoteza vyanzo vyake vyote vya kiroho, na ukawa ni kitambulisho cha wasiwasi uliotawaliwa na kinyume chake, ukiuita na kushindana nao kila wakati. Kwa hivyo, si chochote ila ni mgongano wa hadhara. Kile anachokifanya mwandishi huyu wa habari na anachokifanya kwa kutapatapa katika kuyatetea maadili ya hadhara ya Kimagharibi na vita vyake dhidi ya Uislamu wa kisiasa ni kipengele kimoja tu cha mzozo huu wa kimaumbile na wa milele baina ya hadhara, basi kwa nini wanatushutumu kwa yale wanayoyafanya?

Kwa nini wanapigania uhai wa hadhara yao na kutushutumu kwa mapambano yetu ya kuhuisha hadhara yetu?! Wanaelekeza mishale yao yenye sumu kwa fikra zao chafu, na wanataka tuzipokee kwa vifua vilivyo wazi, vilivyo ridhika bila kuzingatia? Kwa nini wanatushutumu kwa kuhami kwetu Dini yetu na kusisitiza tuwafuate hadi kwenye mashimo yao ili watushinde?! Kwa nini tujisalimishe kwenye kampeni za kuwaoanisha watoto wa Kiislamu na fikra za kisekula na kuoanishwa kwao ndani ya hadhara ya kirasilimali?! Je, hivi sio vita kati ya hadhara kwa ajili ya kupigania kuwa hai? Dkt. Mustafa Mahmoud, Mwenyezi Mungu amrehemu, katika kitabu chake, Political Islam and the Coming Battle, alitoa mukhtasari wa ulisia wa mzozo huu wa hadhara na akaueleza kwa usahihi akisema: “Pindi wanasiasa wa nchi za Magharibi wanapotangaza kwamba wao si uadui kwa Uislamu, na kwamba wao sio dhidi ya Uislamu kama dini, wao ni wakweli kwa njia moja, kwa sababu hawana pingamizi yoyote kwa sisi kuswali, kufunga, kuhiji, kutumia usiku na mchana wetu katika ibada, utukuzaji na dua, na kutumia maisha yetu katika kutegemea (Tawakul), na tubakie nyuma kwa chochote tunachotaka misikitini (I'tikaf), na tumpwekeshe (Tawhid) Mola wetu, tumkuze na tumfanyie Tahlil, kwani wao hawapingi Uislamu wa ibada.

Uislamu wa matambiko na ibada, na wao hawana pingamizi kuwa tuwe na maisha ya akhera yote, kwani hili ni jambo ambalo hawalijali wala hawalifikirii. Bali wanaweza kuwa wamehimiza ibada na kujitenga, na wakajifungamanisha na mashekhe wa njia za Usufi na wakawatetea (nikasema: na hili limetokea), lakini uhasimu na uadui wao ni kwa Uislamu mwingine. Uislamu, ambao unapingana nao juu ya mamlaka ya kuiongoza dunia na kuijenga juu ya maadili na vima vyengine, Uislamu unaogombana nao duniani na unajitafutia uthabiti katika harakati za maisha, Uislamu unaotaka kuendeleza elimu, lakini kwa malengo mengine kando na kutawala, ufunguzi, uchokozi na udhibiti, Uislamu ambao unakwenda zaidi ya mageuzi ya mtu binafsi hadi mageuzi ya kijamii, mageuzi ya kihadhara na mabadiliko ya ulimwengu, hapa hakuna mazungumzo au ncha ya uvumilivu, bali vita vikali, hapa kila mtu itakufyatua, na risasi zinaweza kukujia kutoka kwa vikosi vya nchi yako yenyewe!”

Nne: Sisi katika Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunaendelea, Mwenyezi Mungu Akipenda, kwa mujibu wa yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu na anayoridhia; kufanya kazi ili kuhakikisha Uislamu unatawala. Tutainua risala yake na kuinua bendera yake, hatuogopi lawama ya mwenye kulaumu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na hatuzingatii kashfa ya asiyekamilika na asiye na msimamo ambaye kipimo chake pekee ni maslahi na manufaa, ambayo hubadilika kulingana na maslahi na matamanio. Tunafanya kazi ya kuchunguza habari za Waislamu wakati wote, na kuripoti kile wanachoteseka chini ya mfumo huu wa kisekula wa kilimwengu, na tutapigana nao kwa mvutano wa kifikra ambao unaziweka fikra zake potofu chini na kuonyesha ufisadi wa ufumbuzi wa matatizo ya binadamu, na kwa mapambano ya kisiasa yanayofichua uovu wake, njama na hila zake. Hapana shaka kuwa ni vita vikali, lakini tumemuahidi Mwenyezi Mungu kuung'oa mfumo wa kibepari ili tuurudishe Uislamu katika uhalisia wa maisha ili mabadiliko halisi ya kimsingi yapatikane na mageuzi sahihi ya hadhara yapatikane. Tunaendelea na njia hii kwa mwendo thabiti na tunafanya kazi kuufanya Uislamu uwe ndio hadhara inayotawala na kuongoza. Tuna yakini kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu itatimizwa kwa idhini yake, Aliyetakasika,

[وَاللَّهُ متِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ]

“… Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [As-Saff: 8].

Twamuomba Mwenyezi Mungu uthabiti na mafanikio.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu