Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 22 Sha'aban 1444 | Na: 1444 H / 032 |
M. Jumanne, 14 Machi 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kupunguzwa kwa Bajeti ya India Kwaongeza Hasara kwa Wanawake wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)
Mwishoni mwa Februari 2023, Waziri wa Masuala ya Wachache wa India Smriti Irani alipunguza kwa kiasi kikubwa bajeti ili kuunga mkono ujumuishwaji wa kijamii na kisiasa wa vikundi vilivyo na uwakilishi mdogo nchini India. Hii imewaacha wanawake wengi wa Kiislamu katika hatari ya kupoteza ufadhili wa masomo na usaidizi wa kuwaruhusu kufanya maendeleo katika elimu na malengo ya kitaaluma. Bajeti ya mwaka jana ilikuwa dolari milioni 304 na sasa imepunguzwa hadi dolari milioni 204. Upungufu huo wa dolari milioni umesababisha mgao wa uimarishaji ujuzi na machumo kupunguzwa kwa asilimia 99. Wakati huo huo, vishajiisho kwa mafunzo ya bure na mipango mengine shirikishi ilipunguzwa kwa karibu asilimia 60.
Hatua hizi mpya zimeongeza sera za kibaguzi za mwaka jana zinazowakabili wanawake wa Kiislamu huko Karnataka ambao walikabiliwa na marufuku ya mavazi ya Kiislamu. Walimu wa Kiislamu ilibidi wavue sitara zao kabla ya kuingia shuleni, na wanafunzi Waislamu waliokataa kufanya hivyo walirudishwa nyumbani; mwanamke pekee aliyeruhusiwa kuonyesha itikadi ya kidini alikuwa mwalimu anayeweka "nidhamu". Alivaa sari na bindi, inayochukuliwa kuwa sura inayokubalika ya mwanamke "Mhindi".
Urithi wa unyanyasaji, wa kimwili na wa kilugha, ni maudhui ya kihistoria ya India kwa wanawake wa Kiislamu. Wanawake wa Kiislamu wanaojidhihirisha wanaishi katika hali ya hofu na ukosefu wa usalama mara kwa mara, na sheria hizi mpya zinathibitisha ukweli kwamba hili halitabadilika hivi karibuni. Kampeni ya Waziri Mkuu Modi ya mahusiano ya umma kujionyesha kama mwokozi wa wanawake kutoka kwa ukandamizaji na vikwazo vya maisha ni batili na jaribio la juu juu la kucheza dori ya shujaa wakati yeye ni dhalimu wa aina mbaya zaidi. Mateso ya wanawake wa Kiislamu katika hali ya kimwili na msongo wa kisaikolojia wa kukabiliwa na unyanyasaji yanahusiana moja kwa moja na mipango ya kimfumo inayoungwa mkono na BJP na sera zao za ubaguzi wa rangi / chuki dhidi ya Uislamu. Wakati ufadhili wa haki za wanawake wa Kiislamu unapokuwa mikononi mwa wale ambao wana chuki kwa Uislamu, tunaweza kutarajia hatua hizi zenye madhara zinazowatesa Waislamu na kuwaweka katika hali ya udhaifu.
Kwa ukomo huu wa wazi na dhahiri juu ya maendeleo ya wanawake wa Kiislamu, hatuoni jibu au hatua kutoka kwa mashirika ya kimataifa au viongozi kubadilisha simulizi iliyochakaa kwamba wanawake wanakandamizwa na wanaume wa Kiislamu au ni watu wenye msimamo mkali ambao wanachochea moto wa mvutano wa kidini. Wanawake wa Kiislamu wanatelekezwa na jumuiya ya kimataifa wakati hawawezi kufaidika na kile kinachoitwa uhuru wa demokrasia kubwa zaidi duniani. Maadili huria hayatumiki kwa kusudi lolote kwao. Sera za uanuwai na ujumuishi vilevile ziliwaweka ukingoni mwa jamii kama watu waliotengwa na kukataliwa.
Uwezeshaji wa kweli wa wanawake unaweza tu kuja kutoka kwa Khilafah kwa njia ya Utume ambayo inatumikia mahitaji ya raia wote kwa namna ambayo ni ya haki na isiyo na upendeleo wa kisiasa. Mwenyezi Mungu (swt) aliiteremsha Quran na Sunnah kwa wanadamu ili kutoa mizani na masuluhisho ambayo ni kwa maslahi ya wanadamu bila kujali utaifa, rangi, jinsia au imani.
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاءَ لِلَّهِ وَلَوْ عَلَى أَنْفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ إِنْ يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقِيرًا فَاللَّهُ أَوْلَى بِهِمَا فَلَا تَتَّبِعُوا الْهَوَىٰ أَنْ تَعْدِلُوا وَإِنْ تَلْوُوا أَوْ تُعْرِضُوا فَإِنَّ اللَّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيراً)
“Enyi mlio amini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au masikini Mwenyezi Mungu anawastahikia zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkajitenga nao basi Mwenyezi Mungu anajua vyema mnayo yatenda.” [An-Nisa: 135]
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |