Alhamisi, 09 Rajab 1446 | 2025/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  11 Dhu al-Qi'dah 1444 Na: 1444 H / 039
M.  Jumatano, 31 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ujasusi wa Ufaransa Waikanyaga Sheria na Kufichua Ukweli kuhusu Nchi ya Maarifa na Uhuru kwa Kuomba Kufanyika Sensa ya Watoro Shuleni siku ya Idd al-Fitr!!
(Imetafsiriwa)

Gazeti la kila siku la Ufaransa la La Dépêche lilichapisha mnamo Ijumaa, Mei 19, 2023, habari iliyosema kwamba takriban shule mia moja huko Toulouse na vitongoji vyake zilipokea barua pepe kutoka kwa polisi wa Ufaransa wakiomba kiwango cha utoro wa wanafunzi mnamo Aprili 21, 2023, ambayo ilisadifu kuwa ni sikukuu ya Idd al-Fitr. Makala hayo yalijumuisha ushuhuda kutoka kwa mwalimu mkuu mmoja wa shule ambaye alishtushwa na ombi hili.

Kama ilivyotajwa kwenye gazeti hilo, maombi kama hayo yalipokelewa pia na shule za Hérault, ambapo zilitakiwa kiwango cha kutohudhuria siku ya Idd na hata katika mwezi mzima wa Ramadhan.

Mkuu wa Chuo cha Toulouse, Mustafa Forar, alikanusha kuwa hatua hii iliombwa na Wizara ya Elimu ya Kitaifa. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya gazeti hilo, maafisa wa polisi waliotuma barua pepe hiyo walifanya hivyo kutokana na maagizo ya idara ya upelelezi ya Ufaransa.

Habari hizo kwa hakika zilizua sintofahamu kubwa nchini Ufaransa, na kulikuwa na msururu wa shutma kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu na watu mashuhuri wa umma. Suala hilo limezua mjadala mkubwa. Awali, serikali ilikaa kimya, lakini baada ya kuongezeka kwa maandamano na tuhma, Wizara ya Mambo ya Ndani ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari siku mbili na nusu baadaye, Jumapili jioni. Katika taarifa hiyo, wizara ilikiri kwamba iliomba baadhi ya shule "kutathmini kiwango cha utoro kilichoonekana wakati wa Idd al-Fitr." Hata hivyo, ilikanusha vikali kuitisha sensa ya watoro.

Katika taarifa yake siku hiyo hiyo, Waziri wa Uraia, Sonia Backès, pia alikanusha kuwa kuna data yoyote iliyoombwa kwa jina au takwimu yoyote wakati wowote. Alisisitiza kuwa mpango huo haukuhusisha hamu ya "kukusanya faili" za wanafunzi kulingana na dini zao. Alihusisha suala hilo na tathmini ya mara kwa mara iliyofanywa na "Wizara ya Mambo ya Ndani na Nje ya Nchi" ambayo "hutafiti mara kwa mara athari za sikukuu fulani za kidini katika utekelezaji wa huduma za umma, na haswa katika nyanja ya shule".

Wanaharakati wa haki za binadamu na wengi waliokemea tukio hilo walikubaliana kuwa lililenga Waislamu, na hatari iko katika kuhusisha mila ya watoto wa Kiislamu na suala la usalama wa ndani. Wamekosoa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiiona kuwa ni ghiliba za watu, na kuitaka wizara hiyo kutoa taarifa mara moja kwa umma kuhusu sababu na matokeo ya kilichotokea. Lakini bila shaka, serikali iliziba masikio kwa madai haya na kupiga kichwa chake kama mbuni kwenye uchafu, ikitumai kulificha tukio hilo chini ya zulia.

Kile ambacho ujasusi wa Ufaransa ulifanya inathibitisha tu ukweli uliothibitishwa ambao tumefichua kwa muda mrefu. Inafichua kuwa Ufaransa ni dola ya kijasusi ambayo kwa hila inalenga Uislamu na Waislamu mchana na usiku. Haisiti kuonesha uadui wake kwa uwazi kwa jambo lolote linalohusiana na Uislamu wakati wowote fursa inapojitokeza. Jambo hili halihitaji tena maelezo, kwani historia yake imejaa matukio ambayo bila shaka yanaonyesha uhalisia huu.

Hakika, walichokifanya wakati huu pia kinafichua kwa uwazi uwongo wao wa dhahiri kwa walimwengu kuhusiana na kustahi kwao heshima ya usekula na fikra ya uhuru. Kupitia matendo yao, wamezikanyaga sheria zao wenyewe zinazokataza "ukusanyaji wa data ya watu binafsi ambayo moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja inafichua asili ya rangi au kabila, maoni ya kisiasa, kifalsafa, au kidini" (Kifungu cha 8 cha Sheria ya Julai 6, 1978). Hii ni pamoja na waraka uliotolewa Mei 15, 2004, na Wizara ya Elimu, unaotaka "kuruhusu wanafunzi kutohudhuria shuleni wakati wa sherehe za kidini." Hii ni mbali na kutaja mikataba yote ya kimataifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, ubaguzi wa rangi, na kanuni za msingi za usekula ambazo wamezitangaza kwa sauti kubwa.

Ndio, ujasusi wa Ufaransa umefichua ukweli mara hii na kufichua udanganyifu wa siasa za Ufaransa, kufichua udhalilishaji wao na ukiukaji wa taswira nzuri waliyoichora ya nchi yenye nuru, haki, na uhuru. Hiyo ndio maana mashirika mengi yamepiga kelele na kulichukulia suala hilo kuwa ni kuhujumu usekula, kulenga uhuru, na kushiriki katika ubaguzi wa rangi dhidi ya Waislamu.

Majibu dhaifu ya Wizara ya Mambo ya Ndani yanadhihirisha zaidi jaribio lao la kuchezea akili za watu na uhalisia wa fahamu ya ubwana wa watu. Wananchi hadi leo hawajapata majibu ya maswali yao ambayo serikali haikujishughulisha kuyashughulikia.

Changamoto zinazowakabili Waislamu nchini Ufaransa zinaongezeka kwa kasi ya kutisha hasa baada ya kupitishwa sheria ya kupinga utenganishaji inayotaka Waislamu waoanishwe ndani ya chungu cha uyeyushaji cha usekula. Sheria hii iliidhinishwa mnamo 2021.

Kulengwa kwa Uislamu kumedhihirika, na kuuchukulia Uislamu kuwa ni adui wa kistratejia sasa kumefichuliwa wazi, hasa kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya Waislamu nchini Ufaransa katika miaka ya hivi karibuni, iwe ni wahajiri au wazawa wa Ufaransa waliosilimu.

Mkanganyiko wa serikali na sera yake ya kuwalenga Waislamu unatokana na utambuzi wa wanasiasa wa Ufaransa kwamba mfumo wao unayumba, na Uislamu ndio badali pekee ya kihadhara na tishio la kweli kwa maadili yao. Kwa hivyo, ni muhimu kwa Waislamu nchini Ufaransa kutambua maumbile ya mzozo wanaokabiliana nao na wale walio madarakani na kutambua ubatili wa hadhara ya Kimagharibi na kauli mbiu zake za kidanganyifu. Wanapaswa kushikilia kwa uthabiti Dini yao na wasilegee dhidi ya njama zenye lengo la kuwatia hofu na kuwaoanisha.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu