Jumatatu, 13 Rajab 1446 | 2025/01/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  11 Rajab 1440 Na: 1440/024
M.  Jumatatu, 18 Machi 2019

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Janga la Watoto Wachanga Linafichua Hali Mbaya ya Sekta ya Afya Nchini Tunisia na Kudhihirisha Kufeli kwa Serikali Hiyo Katika Kuchunga na Kulinda Watu Wake!
(Imetafsiriwa)

Janga chungu liliitingisha rai jumla nchini Tunisia wiki jana! Watoto wachanga kumi na tano walikufa katika Hospitali ya Wassila Bourguiba kwa mujibu wa takwimu rasmi na idadi inazidi kuongezeka. Mnamo Ijumaa, Machi 15, msemaji wa Afisi ya Mkuu wa Mashtaka ya Ummah alisema “idadi ya watoto wachanga waliokufa katika Hospitali ya Wassila Bourguiba ilikuwa ni 15.” Janga hilo lilifuatiwa na jengine baya zaidi, kila mojawapo likiifichua dola hiyo kuwa haiangalii watu wake!

Hakuna yeyote aliyesazwa kutokana na ufisadi wa dola hii, si mzee, si kijana wala mtoto mchanga. Dola hii ya kisasa inawapiga vita watu wa Zaytoona katika itikadi yao na kutangaza chuki yake kwa baadhi ya Hukumu zinazojulikana katika Dini kwa dharura, kama vile Hukumu ya ndoa ya mwanamke Muislamu kwa mwanamume kafiri, Hukumu ya usimamizi, na hukumu za urathi. Inatekeleza hili chini ya mwito wa ukombozi kwa wanawake na kuwapa haki na ulinzi, kwa kufuata njia ya makosa ya kueneza zinaa na kushajiisha uzinzi, na kuwashajiisha wanawake kukwepa usimamizi wa wanaume. Kupitia hili ina makinisha mtazamo wa Kimagharibi katika kuangamiza familia na kuivunja vunja kupitia kuingia katika ulimwengu wa wanawake, kudunisha ufahamu wao na kufisidi fahamu zao, huku ukitelekeza uchungaji wao katika mahitaji msingi zaidi ya maisha yao.  Na kuwafanya kuteseka kutokana na umasikini, njaa na uchovu wa miili yao. Hakuna tiba wala hifadhi kutokana na maradhi. Hospitali zinakosa vifaa na huduma za matibabu, na kuna uhaba mbaya sana wa madawa. Hata baadhi ya madaktari wenye ikhlasi wametoa vilio vya hofu kwa sababu wanashuhudia vifo vya polepole kwa maelfu ya wagonjwa kutokana na uhaba huo wa madawa. Dola inayosukumiza majukumu yake yote kwa mashirika ya kimisaada na taasisi za kiraia ili kurahisisha mzigo huo na kukwepa majukumu yao. Hamu yake ya pekee ni kutabikisha maagizo ya Wamagharibi ili kudunisha sekta zote na kuzifanya kuwa mateka wa mkoloni anayeingilia mambo nchini humo na kusimamia kazi yake katika nyanja zote. 

Janga la vifo vya watoto wachanga katika Hospitali ya Al-Rabita ni mojawapo ya majanga yaliyowakumba watu wa Zaytoona chini ya serikali isiyojua njia ya mageuzi … serikali inayotawaliwa na kikundi kinacho shindania maslahi na kuzungukwa na uhasimu wa kisiasa ambao umeitupa nchi hiyo na watu wake katika shimo lenye mikasa ya kufuatana. Na kubwa ambalo laweza kufanywa na serikali hii kikaragosi ni kuwa Wizara ya Afya yaweza kuanzisha “uchunguzi wa haraka wa tukio hilo.” Ni uchunguzi upi huo wa haraka ambao Wizara ya Afya inazungumzia kuuhusu?! Je, kweli itathibitisha majukumu hayo na kutafuta ni nani aliye nyuma ya tukio hili? Je, itachunguza sababu za utepetevu huu na mhalifu halisi wa vifo hivi vya watoto wachanga?

Mipangilio inaharakishwa baina ya kumpeleka hakimu anaye chunguza na Waziri Mkuu hadi katika hospitali hiyo kwa ajili ya uchunguzi na ufuatiliaji na kujiuzulu kwa Waziri wa Afya na mwaliko wa Raisi wa Jamhuri hiyo kuitisha mkutano wa Baraza la Usalama wa Taifa … Kila mmoja yuko chonjo, lakini tunasikia maneno matupu na hatuoni kitendo! Je, watatatua tatizo hili au yote haya ni kuwafanya wajinga watu na kuzima hasira za familia za waathiriwa na watu wa Tunisia kwa jumla waliopinga uhalifu huu wa kinyama na kuituhumu serikali hiyo kushindwa kutoa huduma ya afya kwa watu!

Siku ya mkasa huu inaafikiana na tarehe Machi 8; sherehe za Siku ya Wanawake! Siku hii, ambayo serikali mtawalia nchini Tunisia zimeisherehekea, tangu Bourguiba, hadi Ben Ali na baada ya mapinduzi. Ni tukio ambalo fedha nyingi hutolewa ili kuisherehekea na tarehe yake humakinishwa na vyombo vya habari na taasisi za elimu. Yuko wapi mwanamke katika sherehe hii?

Pazia zimeinuka na mikasa mtawalia imefichua hali halisi wanazopitia wanawake nchini Tunisia. Pazia zimeinuka ili kuonyesha kuwa wanawake wanateseka kutokana na ufukara, dhuluma na kunyimwa… Wanateseka kutokana na shinikizo lililowachosha, kuwachokesha na kuwafedhehesha! Yako wapi mafanikio yaliyopatikana na wanawake kiasi ya kuonewa wivu na wanawake wengine wa nchi zengine?! Je, ni vifo wakati wa uzazi kutokana na ukosefu wa vifaa katika hospitali, au ukosefu wa madaktari wenye ujuzi wanaowapeleka katika vifo vyao wakati wanapojifungua, wakiziacha familia zao zikivunjika moyo? Au ni vifo baada ya kuanguka lori wanalosafiria kwenda makazini mwao, ambako wanafanya kazi kwa masaa mengi, na kurudi mwisho wa siku wakiwa na dinari chache zinazochangia kutoa mahitaji ya familia na mahitaji ya watoto?! Ni Siku ya Wanawake ya aina gani wanayoisherehekea, wakati wanawake hao wanaona watoto wao wakifa kwa kuchomeka, kujiua au kwa kuzama majini?! Iko wapi sherehe wakati watoto wao wanauliwa na mikono miovu, ambayo haiheshimu mkataba wowote wala nasaba kwao, na kuwazamisha katika bahari za mihadarati ambazo hakuna anayeokoka kwazo? Ni sherehe gani hii, wakati wanawake wanarudi majumbani mwao wakiwa na ukiwa wakibeba watoto wao katika “sanduku la kadi bodi” na macho yao yakijaa machozi?     

Biladi ya Uqba ibn Nafi’… Biladi ya Zaytoona… biladi iliyozongwa kwa majanga na mikasa inayofichua kuzorota kubaya katika ngazi zote! Yote haya yanatokea huku serikali hii ikitojali maumivu ya watu, na haifanyi kazi kutatua matatizo yao. Inazurura ndani ya bonde la maslahi yake huku raia wakipotea ndani ya bonde jengine, wakitafuta kile kitakacho wakomboa kutokana na matatizo yao… Serikali isiyo amka usingizini isipokuwa janga litokee, ili kuharakisha kupinga na kushutumu, na kuonyesha maslahi “yanayodaiwa”, na kuanzisha uchunguzi ambao hufunguliwa na kufungwa ili kupata malengo ya kisiasa pekee na kudumisha vyeo. Serikali ambayo watoto wasiokuwa na hatia wanauliwa, na wala haiwaadhibu wahalifu; itafanyaje hivyo wakati ndiyo ngome ya wahalifu hao?! 

Sisi katika Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunashutumu tukio hili chungu na kutoa rambi rambi zetu za dhati kwa kina mama wa watoto hawa wachanga, ambao tunaomba wawe malaika na ndege katika Pepo ya Mwenyezi Mungu, na kumuomba Mwenyezi Mungu kuwapa subra na faraja. Pia tunaitia hatiani serikali hii fisidifu inayotawala nchi hii kwa yale yaliotokea na wale wanaotekeleza sheria yake dhalimu na batil. Tunawahotubia wanawake wa Tunisia na kuwaambia: Enyi wajukuu wa Uqba! Imekuwa wazi kwenu kuwa serikali hii ni kibaraka ambayo inatabikisha pekee yale yanayoagizwa na mkoloni, na haina uwezo wa kuwachunga nyinyi na watoto wenu. Bali, ndio sababu ya moja kwa moja ya matatizo yote na hofu zinazowakumba. Ndio iliyouza utajiri wa nchi yenu na kuuwa watoto wenu. Musilinganie matakwa yasiokuwa na msingi ambayo hayatabadilisha uhalisia, wacheni lengo lenu liwe la juu zaidi kuliko kubadilisha nyuso ovu, na kuleta nyuso nyengine nyeusi na ovu zaidi, kwa sababu wote wanatabikisha maagizo ya wakoloni. Na fanyeni kazi kufikia lengo kubwa na la juu zaidi: badilisheni serikali hii na sheria na kanuni zake fisidifu zilizotungwa na binadamu na simamisheni nidhamu ya Mola wa Walimwengu, inayowabebea kheri nyinyi na wanawake wa ulimwengu.

Enyi wanawake kati ardhi ya Zaytoona! Mabadiliko yanapaswa kuwa ya kimsingi… Hivyo tunawasihi kutuunga mkono na kufanya kazi nasi katika kulingania risala ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), hadi pamoja tuunde dola halisi na sio bandia itakayo waletea izza yenu, na ya biladi hii, na kurudisha ubwana na fahari kwa Waislamu wote chini ya nidhamu ya Mola wa Walimwengu.

«خِلَافَة رَاشِدَة عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.”

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu