Jumamosi, 09 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  5 Sha'aban 1445 Na: 1445 H / 024
M.  Alhamisi, 15 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Watoto mjini Gaza Wanakula Chakula cha Wanyama ili Kuishi!

(Imetafsiriwa)

BBC imeripoti juu ya watu wanaoishi katika eneo lililotengwa la kaskazini mwa Gaza na wameandika kwamba watoto hukosa chakula kwa siku kadhaa. Misafara ya misaada inazidi kunyimwa vibali vya kuingia na umbile la Kiyahudi. Umoja wa Mataifa umeonya kwamba utapiamlo mkali miongoni mwa watoto wadogo kaskazini umeongezeka kwa kasi na sasa uko juu ya kikomo hatari cha 15%. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, linasema zaidi ya nusu ya misheni za misaada kaskazini mwa Gaza zilinyimwa njia ya kuingia mwezi uliopita na kwamba kuna ongezeko la uingiliwaji na majeshi ya Kiyahudi katika jinsi na wapi misaada inatolewa.

Baadhi ya wakaazi wameamua kusaga chakula cha mifugo kuwa unga ili kuishi, lakini hata akiba ya nafaka hizo sasa inapungua, wanasema. Watu pia wameelezea kuchimba kwenye mchanga ili kupata mabomba ya maji ya kunywa na kuoga.

Takriban watu 300,000 wanaripotiwa kuishi katika maeneo ya kaskazini mwa Gaza, na wanakaribia kukatiwa kabisa msaada. Matokeo yake, sasa kuna hatari ya njaa inayoongezeka.

Mfanyikazi mmoja wa kituo cha msaada wa matibabu, Mahmoud Shalabi huko Beit Lahia, alisema watu wamekuwa wakisaga nafaka zinazotumika kwa chakula cha mifugo kuwa unga, lakini hata hiyo sasa zinaisha alisema; "Watu hawazipati sokoni. Hazipatikani siku hizi kaskazini mwa Gaza na Mji wa Gaza. Tulichokuwa nacho ni kutoka kwa siku sita au saba za usitishaji vita [mnamo Novemba], na msaada wowote ulioruhusiwa kaskazini mwa Gaza kufikia sasa watu washautumia. Kile watu wanachokula hivi sasa ni wali, na wali pekee."

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) liliifahamisha BBC kwamba vikosi vya jeshi la Kiyahudi vimesimamisha misafara minne kati ya mitano ya mwisho ya misaada kuelekea kaskazini, na kusababisha pengo la wiki mbili kati ya usafirishaji hadi Mji wa Gaza. Katika kitendo cha utaratibu wa uongo na propaganda msemaji wa shirika la kijeshi la Kiyahudi lililopewa jukumu la kuratibu upatikanaji wa misaada huko Gaza alisema katika mkutano wa mwezi uliopita kwamba "hakuna njaa mjini Gaza. Kwisha." Shirika hilo, Cogat, limesema mara kwa mara haliwekei kikomo misaada ya kibinadamu inayotumwa Gaza.

Tunajua kwamba ukweli mkali na uhalisia wa kutisha wa hali ya Gaza unafichwa na vyanzo vya habari uwanjani vinathibitisha vyenginevyo.

Watoto wetu wapendwa, safi, wa Gaza wanawezaje kutendewa kama wanyama kwa namna hii! Kwa hakika, watawala wa nchi za Kiislamu lazima wawajibike kwa usaidizi wao katika jinai hizi kwani wanayazuia majeshi ya Waislamu. Sisi kama Umma wa Kiislamu hatuwezi kamwe kuukubali uovu unaojitokeza unaotolewa kwa jina la ulinzi feki na uhuru wa kupambana na Mwenyezi Mungu (swt). Enyi Umma wa Kiislamu, tangazeni ukimya wa tawala hizi na mujitenge na historia inayoandikwa katika kuendeleza mipango ya Shetani. Ili Mwenyezi Mungu aturehemu Siku ya Kiyama kutokana na adhabu yake kali.

[أَلَيْسَ اللَّهُ بِكَافٍ عَبْدَهُ وَيُخَوِّفُونَكَ بِالَّذِينَ مِن دُونِهِ وَمَن يُضْلِلِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ * وَمَن يَهْدِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِن مُّضِلٍّ أَلَيْسَ اللَّهُ بِعَزِيزٍ ذِي انتِقَامٍ * وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّهُ قُلْ أَفَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّهِ إِنْ أَرَادَنِيَ اللَّهُ بِضُرٍّ هَلْ هُنَّ كَاشِفَاتُ ضُرِّهِ أَوْ أَرَادَنِي بِرَحْمَةٍ هَلْ هُنَّ مُمْسِكَاتُ رَحْمَتِهِ قُلْ حَسْبِيَ اللَّهُ عَلَيْهِ يَتَوَكَّلُ الْمُتَوَكِّلُونَ * قُلْ يَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَى مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ * مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيْهِ عَذَابٌ مُّقِيمٌ]

“Je! Mwenyezi Mungu si wa kumtosheleza mja wake? Na ati wanakutishia kwa hao wenginewe wasio kuwa Yeye! Na aliye hukumiwa na Mwenyezi Mungu kupotea hana wa kumwongoa. Na ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa hana wa kumpotoa. Je! Mwenyezi Mungu si Mwenye nguvu anaye weza kulipiza? Na ukiwauliza: Ni nani aliye ziumba mbingu na ardhi. Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu. Sema: Je! Mnawaonaje wale mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu akitaka kunidhuru, wao wanaweza kuniondolea dhara yake? Au akitaka kunirehemu, je, wao wanaweza kuzuia rehema yake? Sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Kwake Yeye wategemee wanao tegemea. Enyi watu wangu! Fanyeni mwezavyo, mimi pia nafanya. Basi mtakuja ona. Ni nani itakaye mfikia adhabu ya kumhizi, na itakaye mshukia adhabu ya daima.” [Az-Zumar: 36-40]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu