Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  2 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: H 1445 / 037
M.  Ijumaa, 10 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa kuzingatia Kuenea kwa Ushoga na Utamaduni wa Uzinzi, Mitandao ya Uhalifu Inawalenga Watoto nchini Lebanon
(Imetafsiriwa)

Lebanon ilitingishwa na habari za kufichuliwa kwa mtandao potovu wa wahalifu (genge la TikTok) ambao huwarubuni watoto wadogo, kuwashambulia na kuwabaka, na kuwalangua katika karamu kubwa kubwa za chafu! Kwa mujibu wa habari za kiusalama, idadi ya wahasiriwa wadogo wa mtandao huu inaweza kufikia dazeni, na maelezo ya uhalifu huu bado yanachapishwa katika sura, kwa majina ambayo yanajulikana na maarufu katika ulimwengu wa mitandao ya kijamii, pamoja na majina mengine ambayo bado yanafichwa. Mtandao huu wa uhalifu sio wa kwanza wa aina yake na hautakuwa wa mwisho kwa kuzingatia kuenea kwa utamaduni wa upotovu na ushoga katika nchi yetu. Mnamo 2016, Lebanon pia iliibuka kashfa inayofanana na hii, ya utumizi mbaya na kutisha kwake, kwani vyombo vya usalama vilisimamisha mtandao mkubwa zaidi wa utumizi mbaya na ulanguzi wa binadamu, unaojulikana kama mtandao wa Chez Maurice, ambao uliwaweka kizuizini wasichana wapatao 75 kutoka Lebanon na Syria kwa miaka mingi ukilenga kuwasafirisha. Kuanzia 2016 hadi 2024, vikao vya kesi ya Chez Maurice bado viko katika hatua za awali katika Mahakama ya Jinai kutokana na mgomo katika sekta ya mahakama na pia udhaifu wa sekta hii kutokana na kuingiliwa kisiasa ndani yake.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Hemaya, watoto wapatao 1,932 nchini Lebanon walikabiliwa na ukatili kuanzia Januari hadi Septemba mwaka wa 2023. Uhalifu wa dhulma ya kingono, hasa dhidi ya watoto, ni mojawapo ya matatizo kadhaa ambayo yameonyesha kuporomoka kwa maadili na ufisadi wa maadili ya jamii nchini Lebanon, ambapo uraibu wa pombe na dawa za kulevya, ukahaba, kujiua, ufisadi, ubakaji wa watoto, na majanga mengine yanaharibu jamii hii na nyinginezo za kibepari za karne ya 21. Mfumo huu fisadi na wenye kufisidi wa kirasilimali haujaharibu watoto tu, bali pia umeangamiza wanadamu wote. Yeyote anayetazama uhalisia wa jamii zetu leo anaona kiwango cha changamoto na hatari zinazotukabili katika ngazi mbalimbali kutokana na kuingizwa kwa fikra za Kimagharibi na ushawishi wa fahamu hatari katika tabia za maisha yetu, jambo ambalo limesababisha uhalisia mchungu, kwa hakika, mgogoro mkubwa na changamoto halisi inayokabili vipengele vya nchi yetu ya Kiislamu. Hali yetu imefupishwa katika aya tukufu:

[وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Taha 20:124].

Hali hii inatokana na kutenganishwa dini na maisha, yaani, kukomeshwa kwa haja ya mwanadamu ya dini na sheria za kimungu, na kujitenga kwake kikamilifu nazo kwa kisingizio cha usasa na uhuru. Matokeo yakawa ni kuchanganyikiwa, hasara, na kuenea kwa utupu wa kiroho, kuchoshwa, kufazaika, unyogovu, hasara na kujiua miongoni mwa watoto na vijana, si tu nchini Lebanon bali katika ulimwengu mzima.

Uhalifu wa ulanguzi wa binadamu unashika nafasi ya tatu katika ulanguzi wa kimataifa unaoingiza faida kubwa duniani kote, ukizidiwa na biashara ya silaha, ikifuatiwa na biashara ya dawa za kulevya. Umoja wa Mataifa unakadiria idadi ya wahanga wa ulanguzi wa binadamu duniani kote kuwa takriban watu milioni 27.6.

Idadi kubwa ya uhalifu huu na idadi kubwa ya wahasiriwa inatuthibitishia kufeli kwa mikataba ya kimataifa ya haki za mtoto, ambayo haikukuzwa katika nchi yetu na haikulazimishwa kwa jamii zetu isipokuwa kueneza uasherati na uovu kwa kukosekana sheria ya kuadhibu. Kwa hiyo, balaa ilienea, vizazi vilipotea, na hata haki zote za binadamu zilipotea. Huu hapa Umoja wa Mataifa na mashirika yake, kama vile UNICEF, likiwa mbali na kutunza watoto isipokuwa ndani ya mfumo wa “taratibu, michango, kazi ya kujitolea, na Siku ya Watoto Ulimwenguni, na tusisahau kutaja kwake takwimu za kila mwaka.”

Kuzungumza juu ya “haki za watoto” ni lazima kutilia maanani utafutaji mkubwa wa vifungu na sheria zinazomhakikishia kila mtoto duniani kuishi maisha yenye heshima, bila kuruhusu mtoto aachwe kwenye vitisho au kuteseka. Hukmu na sheria kama hizo hazitatolewa na akili ya mwanadamu, bali ni hukmu za kisheria zilizoamuliwa na Muumba wa mwanadamu, ulimwengu, na uhai, zinazomhakikishia kila mwanadamu haki yake, awe ni mtu mzima au mtoto, mwanamume au mwanamke. Muumba Pekee ndiye anayejua viumbe vyake na anajua wanachohitaji na kile watakachonufaika nacho. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[أَلا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ]

“Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?” [Al-Mulk 67:14]. Moja ya haki muhimu sana za mtoto ni kuwepo kwa dola inayohifadhi haki zake na kumlinda kwa njia inayomridhisha Mwenyezi Mungu, kumchunga mambo yake, kukidhi mahitaji yake ya lazima, ya kimaadili na kimaumbile, na huduma za matibabu, na kumpa mazingira ya imani yanayomzuia kusambaratika na kupotea. Mbele ya mambo haya yote ya kutisha tuliyotaja, hatuwezi kujizuia kupiga kelele na kutahadharisha kama familia na walezi kwanza na kama wabebaji wa Dawah kwa hatua za dhati katika kupambana na fahamu zote fisidifu na fikira potovu zinazoathiri kwanza kabisa jengo muhimu la jamii zetu, ambalo ni familia, kulingana na kile mbora wa viumbe vya Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimshukie amesema:

«أَلَا كُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ؛ فَالْإِمَامُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، وَالْمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ عَلَى أَهْلِ بَيْتِ زَوْجِهَا وَوَلَدِهِ وَهِيَ مَسْئُولَةٌ عَنْهُمْ»

"Jueni! Nyote ni wachungaji na nyote mutakwenda kuulizwa mulivyovichunga: Imam (mtawala) aliye juu ya watu ni mchungaji na yeye ataulizwa kuhusu raia wake; mume ni mchungaji juu ya familia yake na utakwenda kuulizwa juu ya raia wake; mke ni mchungaji juu ya familia ya mumewe na watoto wake na atakwenda kuulizwa juu yao.” Yeye (saw) alikuwa akiwashajiisha maswahaba zake (ra) kwa kusema: «ارْجِعُوا إِلَى أَهْلِيكُمْ فَأَقِيمُوا فِيهِمْ وَعَلِّمُوهُمْ»  “Rudini kwa familia zenu, kaeni nao, na muwafunze (Imani na matendo ya Uislamu) na wahimizeni kheri.”

Ni wajibu wenu, wazazi, kuwa makini na kuwa macho kwa yale ambayo watoto wenu wanaona na tovuti wanazotembelea kwenye Mtandao na gumzo mtandaoni lisilo na lengo tovuti za gumzo ambazo zinapoteza muda bila manufaa yoyote na kuwapa silaha ya usahihi, yenye nguvu, na kitisheni Aqida (itikadi) ya Kiislamu ambayo inawafanya wapambanue kati ya kile kinachoruhusiwa na kilichoharamishwa, na ambacho kinajenga ndani yao tabia pambanuzi ya Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Wahyi Wake wa Kukatikiwa:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَاراً وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَا يَعْصُونَ اللهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa.” [At-Tahrim 66:6].

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu