Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  7 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445 H / 038
M.  Jumatano, 15 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Gaza ina Vifusi Vingi kuliko Ukraine, na Dada zetu na Watoto Wetu ndio Wengi wa Wafu Wanaozikwa Chini Yake

(Imetafsiriwa)

Shirika la Wanawake la UN lilitoa ripoti mnamo mwezi Aprili 2024, kuhusu hali ya wanawake na watoto mjini Gaza. Miezi sita ya vita hivyo, zaidi ya wanawake 10,000 wameuawa, kati yao kina mama wanaokadiriwa kufikia 6,000, na kuacha watoto 19,000 wakiwa yatima. Al Jazeera inakadiria kuwa wanawake na watoto 25,000 wameuawa. Huku zaidi ya waandishi huru wa habari 100 kuuawa na bila ya kuwepo jopo lililopangiliwa la wachunguzi kuruhusiwa kuwepo katika eneo hilo, ni vigumu sana kufuatilia idadi kamili, na ni lazima tuchukulie kwamba takwimu hizi ziko chini ya uhalisia.

Mnamo tarehe 2 Mei 2024, Charles Mungo Birch, mkuu wa Huduma ya Utekelezaji Migodi ya Umoja wa Mataifa @UNMAS nchini Palestina alitoa taarifa ya umma duniani kote. Katika taarifa yake rasmi kwa vyombo vya habari yafuatayo yalielezwa: “Gaza ina vifusi vingi zaidi kuliko Ukraine, na ili kuweka hilo katika mtazamo, mstari wa mbele wa Ukraine una urefu wa maili 600, na Gaza ni maili 25.” Aliongeza kuwa kuna zaidi ya tani milioni 37 za uchafu wa kuondolewa huko Gaza mara tu vita vya “Israel” kwenye Ukanda huo vitakapomalizika.

Kiwango cha ulipuaji wa mabomu na maangamizi hakijawahi kutokea katika historia ya ulimwengu, kwa muungano wa wasaidizi waovu wa mauaji yanayopatikana katika serikali fisadi za kikoloni za Magharibi na watumwa wao kwa sura ya watawala wote katika ardhi zetu za Kiislamu. Tunachopaswa kutambua katika kuangalia idadi kubwa ya vifo vya wanawake na watoto ni kwamba maelfu ya wanawake na watoto walioorodheshwa wamekufa wanasalia chini ya vifusi anavyozungumzia. Wengi walikufa papo hapo huku wengi wakifa polepole na vifo vya uchungu kwa siku nyingi wakisubiri kuokolewa bila mtu wa kuwaokoa. Wafanyikazi wa misaada na majirani, pamoja na wanafamilia, wameripoti kuwa waliweza kusikia mayowe ya watoto na wengine wakiwa hai, lakini kutokana na ukosefu wa vifaa au mafuta ya kuwakisha mitambo ya uokozi, iliwalazimu kuwaacha wakiwa wamenaswa na hatima yao isiyoepukika.

Hata kazi ya kuwatoa wafu, katika hali yoyote ya kupata mwili, imekabiliwa na changamoto kubwa. Mungo alieleza kuwa kifusi hicho kimechafuliwa kwa kiasi kikubwa na UXO (Unexploded Ordinance) pamoja na kemikali zinazotumika katika vita. Aliongeza kuwa zaidi ya tani 800,000 za asbesto pia ni hatari halisi na iliyoko.

Je, mipango ya uwezeshaji wanawake inawezaje kuchukuliwa kwa uzito tena!? Watetezi wa haki za wanawake na sheria za kimataifa juu ya uwezeshaji wanawake, unyanyasaji dhidi ya wanawake na haki za wanawake wote wamethibitika kuwa uongo mtupu, na sheria hizi zinatumika tu kushambulia sheria za Kiislamu na kudhibiti kuenea kwa Uislamu. Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa lilizindua Tahadhari ya hivi punde ya Jinsia kuhusu Gaza miezi sita tangu vita, na inakadiriwa kuwa kina mama 6,000 wameuawa, na kuwaacha watoto 19,000 wakiwa yatima. Wanawake ambao wamenusurika katika mashambulizi ya mabomu na operesheni za ardhini za umbile la Kiyahudi wamehamishwa, ni wajane, vilema na wanakabiliwa na njaa. Hakika hivi ni vita dhidi ya wanawake na watoto.

Kwa mwanamke yeyote wa Kiislamu ambaye anaendelea kuwa na imani au matumaini katika mifumo, sheria na taasisi za kisekula ili kuwaokoa dada zao Waislamu huko Gaza au kwengineko kutokana na mauaji na maangamizi, hakika sasa ni wakati wa kuzika matumaini yako katika vifusi na magofu ya demokrasia ya Magharibi, na badala yake waungane katika ulinganizi wa kusimamishwa kwa haraka Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt), Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itamuondoa kila mtawala kibaraka katika ardhi zetu na kuyakusanya majeshi ya Kiislamu kutimiza wajibu wao kwa Mwenyezi Mungu wa kuwalinda, kuwatetea na kuwakomboa Waislamu.

[وَمَن يُوَلِّهِمْ يَوْمَئِذٍ دُبُرَهُ إِلاَّ مُتَحَرِّفاً لِّقِتَالٍ أَوْ مُتَحَيِّزاً إِلَى فِئَةٍ فَقَدْ بَاء بِغَضَبٍ مِّنَ اللّهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ]

“Na atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo - isipo kuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi - basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahala pake ni Jahannamu, na huo ni mwisho muovu.” [Al-Anfal: 16]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu