Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  1 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: H 1445 / 036
M.  Alhamisi, 09 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari  
Kutokuwepo kwa Uislamu kwenye Mandhari Hutia Ujasiri Mataifa Kutushambulia Ni Khilafah Pekee Inayohifadhi Hadhi Yetu
(Imetafsiriwa)

Vyuo vikuu vya Marekani vinashuhudia maandamano makubwa ya kupinga uvamizi wa Mayahudi dhidi ya Gaza ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miezi saba. Vyuo vikuu vimeshuhudia maandamano ya wanafunzi na walimu kwa pamoja, Waislamu na wasiokuwa Waislamu, kulaani ukatili wa umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu dhidi ya Waislamu wenye msimamo thabiti huko Gaza. Wakati watu wa Magharibi wamekuwa wakiishi kwa miongo kadhaa chini ya udanganyifu wa uhuru unaounadiwa kwao na wanasiasa, maandamano haya yalifichua ubaya zaidi wa mfumo wa Kimagharibi, na uwongo wa maadili ya uhuru na haki za binadamu ya kujieleza na kuamini. Maelfu wamekamatwa na kadhaa kupigwa kwa misingi ya chuki dhidi ya Mayahudi. Siku mbili zilizopita, wasichana wanne wa Kiislamu walishambuliwa hasa katika Chuo Kikuu cha Arizona, hijabu zao zilivuliwa kwa nguvu na kutupwa gerezani huku kukiwa na shutma kali kutoka kwa wanafunzi na waliohudhuria ambao walinakili tukio hilo. Haya yalilaaniwa na Mkurugenzi Mtendaji, Azza Abu Seif, wa tawi la Arizona la Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR).

Siku zote viongozi wa Kimagharibi wamekusudia kuwaonyesha Waislamu katika sura mbili kwa watu wao na kwa ulimwengu wote: ima magaidi wenye itikadi kali wenye nia ya mauaji na kiu ya umwagaji damu na ulipuaji wa mabomu kwa watu wasio na hatia, sambamba na kuunyanyapaa Uislamu kama dini ya ghasia ambayo imeenea kwa nguvu ya upanga, katikati ya uwongo wa kihistoria na kueneza uwongo bila ya uwazi usio na upendeleo wa ukweli na maana ya jihad Au wajinga, walio nyuma, washenzi ambao hawaelewi chochote kuhusu ustaarabu, ambao wako nyuma katika utamaduni na ustaarabu, wakati Magharibi ni bora kuliko wao na inawafanyia ihsani kwa kueneza utamaduni wake kwao na kuvamia nchi zao!

Lakini miaka iliyopita, kwa rehema za Mwenyezi Mungu, na hasa baada ya Oktoba 7, 2023, sura ambayo Magharibi iliiona ya Waislamu ilibadilishwa. Kwa mara ya kwanza dunia iliwaona Waislamu katika sura ya wenye hadhi, si sura iliyofedheheshwa ambayo wanasiasa wa Magharibi waliichora kuhusu Waislamu. Katika kipindi cha miezi ya vita, umbile la Kiyahudi lilijaribu kuficha picha hii kwa makusudi, na kuficha macho ya umoja wa Waislamu, ambao kwa uthabiti wao na subira baada ya operesheni ya Oktoba 7, 2023, walidhoofisha juhudi zote za adui kwa miaka kuingiza mgawanyiko na kuimarisha kutokuwa na uwezo wa kuung'oa uvamizi. Kwa hiyo, umbile la Kiyahudi likawa la kikatili, lenye kumwaga damu, na kufanya mauaji ya kutisha kwa njia mtawalia, likionyesha chuki iliyofichika na uoga wa kweli kwa kukaribia kuangamia kwa umbile lao. Watu duniani waliasi baada ya kushangazwa na ushirikiano wa watawala wao na uungaji mkono wao kwa jinai ya umbile la Kiyahudi, kwani wao ndio ambao daima wameziona nchi zao katika dori ya shujaa anayetetea maadili ya uadilifu na uhuru.

Mwanamke wa Kiislamu, aliyelengwa moja kwa moja kama vile mwanaume, kwa kuzingatia vita vya umwagaji damu vilivyoanzishwa na nchi za Magharibi na Mashariki dhidi ya Waislamu katika nchi za India na China upande wa mashariki hadi Marekani magharibi, uwepo wake ulikuwa imara katika Gaza yenye fahari, akiwapa dada zake ulimwenguni maana ya uthabiti, fahari, subira, na utayari wa kujitolea kwa ajili ya Dini ya Mwenyezi Mungu kwa uhai, mali na watoto. Na sasa dada zake huko Amerika na Ulaya pia wamesimama na kuchukua hisa yao ya mtihani kwa ajili ya kusimamisha haki na kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu. Wanachofanyiwa wanawake wa Kiislamu katika nchi za Magharibi katika suala la ubaguzi wa rangi, unyanyasaji, na kuvuliwa hijabu vichwani mwao ni matokeo ya ushirikiano wa watawala wa Kiislamu na usaliti wa majeshi yaliyowekwa katika kambi zao.

Ingekuwa jambo tukufu kiasi gani kama maafisa katika majeshi ya Ummah wangeelewa dori yao waliyopewa, na wangejua umuhimu wa dori yao katika mabadiliko na dhambi kubwa linaloangukia mabegani mwao kwa kunyamaza kwao. Tumeliona jeshi likiiteka Amuriya kwa ajili ya mwanamke mmoja ambaye watoto wake waliuawa, hivyo akalia kuomba msaada kutoka kwa Khalifa. Sasa tunasikia vilio vya maelfu ya wanawake huko Gaza na kutazama matukio ya hijabu zikitolewa kwenye vichwa vya wanawake wa Kiislamu mbele ya watu, na picha hizi kupeperushwa hewani ili kuufikia ulimwengu wote, lakini hawapati khalifa kusonga wala jeshi linalorudisha haki na kuhifadhi heshima!

[فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى الْأَبْصَارُ وَلَكِن تَعْمَى الْقُلُوبُ الَّتِي فِي الصُّدُورِ]

“Kwani hakika si macho yanayo pofuka, lakini zinazo pofuka ni nyoyo ziliomo vifuani.” [Al-Hajj: 46]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hi.zat.one
Fax: Telefax
E-Mail: [email protected]

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu