Jumamosi, 23 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  10 Dhu al-Hijjah 1445 Na: H 1445 / 042
M.  Jumapili, 16 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mauaji ya Nuseirat Yanafichua Dini ya Ukafiri
Na Yanafichua Ufadhili na Uungaji Mkono wa Marekani kwa Umbile la Uhalifu
(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 8 Juni 2024, umbile la Kiyahudi lilifanya mauaji ya kutisha katika kambi ya Nuseirat katika Ukanda wa Gaza kwa usaidizi wa Marekani kwa kisingizio cha “kuwaokoa wafungwa 4” wanaozuiliwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Hamas) na kuwakomboa kutoka mikononi mwake.

Vikosi vya umbile hilo vilivyojifanya kuwa wafanyikazi wa kutoa misaada ya kibinadamu walijipenyeza kwenye kambi hiyo kupitia lori lililokuwa likitoka katika bandari ya Marekani - ambayo inadaiwa kuwa iliasisiwa ili kutoa misaada ya kibinadamu - na kuanzisha mashambulizi makali na ya vurugu ya anga, nchi kavu na baharini kwa takriban saa mbili katika eneo la soko kuu, ambalo linajaa kila siku maelfu ya wakaazi katika kambi ya Nuseirat na maeneo ya jirani, ambayo baadaye yaliathiri maeneo mengi ya katikati mwa Ukanda wa Gaza. Operesheni hii - kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha uchunguzi cha shirika la Euro-Mediterranean Observatory - ilisababisha kuuawa shahidi kwa Wapalestina zaidi ya 200 na kujeruhiwa mamia ya wengine, ambao wengi wao walikuwa wanawake na watoto, kulingana na takwimu za awali ambazo zinaweza kuongezeka shughuli za uokoaji zinaendelea. Uchunguzi wa shirika la Euro-Mediterranean Observatory ulithibitisha kwamba kujifanya kutumia vyombo vya usafiri vilivyotengwa kwa ajili ya misaada ya kibinadamu, na kuvaa nguo za wafanyikazi wa misaada ya kibinadamu kama kifiniko ni uhalifu wa uhaini.

Hivyo basi, operesheni hii ilifichua kwamba bandari hii haikuwa chochote bali ni chanzo cha kimkakati cha kijeshi kilichoundwa kuunga mkono uvamizi wa Kizayuni. Licha ya njaa ambayo watu wetu wa Gaza wanateseka nayo na hali mbaya ya kibinadamu, bandari hii, na licha ya uhitaji wa eneo hilo kwa malori 700 ya misaada, imewezesha kuingia kwa malori yasiyozidi 150 pekee, na kufanya ushiriki wa Marekani katika operesheni hii ya uhalifu kuwa wazi na kufichua kwa mara nyengine tena uungaji mkono wake na ufadhili wa umbile hili katili na usaidizi wake kwake katika uhalifu wake. Bandari hii iliasisiwa ili tu kufikia malengo ya kijeshi pekee.

Kile ambacho Marekani na umbile la Kiyahudi wanafanya kinagongana kikamilifu na kanuni muhimu zaidi za sheria za kimataifa na haki za binadamu, ambazo hazijumuishi kulenga raia, shule na hospitali. Uhalifu huu unaolenga watoto na wanawake wasio na hatia hauwezi kuhalalishwa haki kwa njia yoyote ile. Lakini wauaji hawa wawili wanafanya kazi ya kukuza tafsiri nyengine ambayo ni tofauti na fahamu za haki za binadamu, ili kupata njia za kutokea na maelezo kwa ukiukaji unaoendelea wanaoufanya.

Je, Marekani haihusiki na mauaji ya kutisha nchini Afghanistan, Iraq, Syria na Yemen? Je, siyo iliyoibua kauli mbiu ya “kupambana na ugaidi” ili kuua maelfu ya watoto na wanawake wa Kiislamu na haihojiwi kuhusu damu isiyo na hatia iliyomwaga? Je, mahakama za kimataifa, chini ya usimamizi na ufadhili wake, hazitungi sheria zinazokidhi maslahi yake na zinazoafikiana na uhalifu wake, ili waepuke adhabu na uwajibikaji? Bunge la Congress la Marekani hapo awali lilipitisha sheria za kuwalinda wanajeshi na viongozi wa kisiasa wa umbile la Kiyahudi dhidi ya taratibu za Mahakama ya Kimataifa ya Jinai. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller alitoa taarifa kuhalalisha uhalifu wa uvamizi huo dhidi ya raia katika Ukanda wa Gaza. Akitoa maoni yake juu ya mauaji yaliyotokea katika shule moja wanamoishi watu waliokimbia makaazi yao huko Nuseirat mjini Gaza, Miller alisema kuwa “wapiganaji wa Hamas walitumia eneo hilo, ambapo inaonyesha kuwa uwepo wa wanamgambo unafanya raia walio ndani yake kuwa walengwa halali.”

Marekani, ambayo wakati huo huo inasimamia mazungumzo ya “kusitisha mapigano”, haisiti kuhalalisha operesheni hii ya uhalifu, ambayo inatufanya tuwe na uhakika zaidi kwamba damu ya watu wa Gaza, watoto wao na wanawake haina umuhimu wowote kwake na iko nje ya upeo wa mahesabu na mazingatio yake, ujanja wake na mipango yake.

Kwa nini mauaji haya ya kutisha na mauaji mengine hayajaamsha ujasiri ndani ya Ummah na kujadidisha damu yake ili kutetea kila sehemu ya mwili wake inayouma na kutamani uadilifu na rehma, ili amani iweze kupatikana baina ya watu kupitia hukmu ya Shariah ya Mwenyezi Mungu na kuenea kwa Uislamu?

Kimya hiki kitadumu hadi lini huku damu za wasio na hatia zikimwagwa na mikono ya wahalifu na kukiukwa na maadui? Wako wapi wanazuoni wa Ummah? Wako wapi warithi wa manabii?

Kwa nini kuna kushindwa mbele ya ushirikiano wa makafiri na ulezi wao kwa wao? Wako wapi waumini ambao ni washirika wao kwa wao? Kwa nini wanashindwa kuwanyooshea mkono ndugu zao? Iko wapi nusra yao kwa waliodhulumiwa wanaoomba msaada wao katika Dini yao? Yuko wapi Salah ud-Din, ambaye ataikomboa Al-Aqsa kutokana na najisi ya Mayahudi? Wako wapi Al-Fatih na Baybars? Ni nani atakayezuia umbile hili la uhalifu na mshirika wake, linaloweka sheria na kuendesha ulimwengu kama linavyopenda? Ni nani atakayelishambulia kwa mkono wa chuma isipokuwa dola ya Kiislamu (Khilafah), ambayo itasimama kulinda dhidi ya yeyote atakayesubutu kushambulia shubiri moja ya eneo lake au mmoja wa raia wake?

Sisi, katika Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, tunalaani na kukemea mauaji haya, na tunayaomba majeshi ya Waislamu kuchukua hatua kali ambayo itawashangaza maadui na kuponya nyoyo za watu wetu huko Gaza, iwe ni vijana, watoto au wanawake. Tunawaomba wawanusuru na waunusuru ulinganisi wa haki, unaolingania kusimamishwa dola ya Kiislamu ambayo kwayo hukmu za Kiislamu zinatabikishwa na Waislamu, na kwa hakika watu wote wanatendewa haki.

Hebu na wafanye haraka watu wenye ikhlasi wa Ummah huu kupata heshima hii kubwa ili kumridhisha Mola wao Mlezi, na Yeye (swt) atawaridhisha kwa cheo kitukufu na Mabustani yenye Neema.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu