Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Kuwait

H.  12 Safar 1444 Na: 1444 / 01
M.  Alhamisi, 08 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mifumo ya Kidemokrasia Inaishi Sambamba na Matatizo na Migogoro na Haiyasuluhishi
(Imetafsiriwa)

Amri ya kifalme ilitolewa kuvunja Bunge na kuitisha tena uchaguzi. Mandhari hii imerudiwa nchini Kuwait kwa miongo kadhaa. Baada ya hali kuwa mbaya zaidi kati ya mamlaka hizo mbili, ikifuatiwa na mivutano ya wabunge na wananchi, na mkwamo wa kisiasa unaosababisha kuvurugika kwa kazi za Baraza na serikali. Na kadhalika bila ya kumalizika.

Wakati huo huo, watu wameshughulishwa na mandhari ya uchaguzi, na mazungumzo na matarajio yao ni mengi juu ya nini kitatokea kutokana nao, na nani ana uwezekano mkubwa wa kuliongoza Bunge, na kuongoza serikali na mawaziri, na wanaweka matumaini juu ya matokeo yake ili mtu anayefanya kazi ya kutatua matatizo yao atakuja.

Hata hivyo, watu wengi hawakutambua kwamba tatizo kuu sio waziri mkuu, spika wa bunge au manaibu wake, au hata mfumo wa uchaguzi wa kura moja au kitambulisho cha kiraia. Badala yake, tatizo kuu ni mfumo wa kidemokrasia uliotekelezwa kwao kwa miongo mingi. Kwa sababu imetengenezwa na mwanadamu.

Mfumo wa kidemokrasia huwapa ubwana watu, sio kwa Shariah! Ambayo inamaanisha kuzipa akili za binadamu haki ya kutunga sheria ambazo zina mapungufu, dhaifu, na zenye kikomo, na huathiriwa na mazingira na dhurufu zinazowazunguka, na sio kwa Muumba wa wanadamu! Huyafanya maoni ya walio wengi kuwa kigezo cha usahihi wakati wa kutatua matatizo, na sio hukmu za Shariah zinazotatua matatizo yote ya mwanadamu!

Kwa ajili hii, kuchunga mambo ya watu na kushughulikia matatizo yao kunakabiliwa na mkanganyiko, kutofautiana na kugongana, na kupoteza muda, juhudi na pesa kutokana na watu kushikamana na mfumo wa kidemokrasia, ambao ndio sababu ya mateso yao na chanzo cha matatizo yao.

Enyi Waislamu: Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Taha:124].

Aya hii iko wazi katika maana yake kwa wale wasiozingatia maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu kupitia kutekeleza hukmu za Shariah; ana maisha magumu! Wa mwisho wa Ummah huu hautabadilishwa ila kwa yale yale ambayo wa kwanza wake ulibadilishwa kwayo. Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume wake (saw).

Hali za nchi na watu hazitanyooka isipokuwa kwa kuukataa mfumo wa kidemokrasia na kusimamisha mfumo wa utawala kwa mujibu wa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu (swt) Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Kupitia kwayo Uislamu na Waislamu huthaminiwa, na matatizo ya watu hushughulikiwa na mambo yao kuchungwa kwa mujibu wa amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu, na ambayo kwayo watu wanaweza kuchagua mtawala wao, na ambayo kwayo Shariah ya Mwenyezi Mungu inaweza kutawala.

[إِنَّمَا كَانَ قَوْلَ الْمُؤْمِنِينَ إِذَا دُعُواْ إِلَى اللهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ أَنْ يَقُولُواْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ]

“Haiwi kauli ya Waumini wanapo itwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, ila ni kusema: Tumesikia, na tumet'ii! Na hao ndio wenye kufanikiwa.” [An-Nur:51]

Idara ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Kuwait

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Kuwait
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu