Afisi ya Habari
Kyrgyzstan
H. 15 Muharram 1444 | Na: 1444 H / 01 |
M. Jumamosi, 13 Agosti 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi Mmoja wa Mashababu wa Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Kyrgyzstan ina huzuni kubwa kwa watu wa Kyrgyzstan kwa kufikwa na mtihani mkubwa wa kifo cha Ustadh wetu Osanbay, ambaye aliregea kwenye rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu usiku wa kuamkia Agosti 11, siku ya Ijumaa iliyobarikiwa. Jina kamili la Ustadh lilikuwa Osanbay Soirkulov Ahmetoglu, na jina lake maarufu miongoni mwa watu lilikuwa Ustadh Osanbay.
Twamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu, Ayaondoe madhambi ya Ustadh Osanbay, na amghufirie madhambi yake, na amuingize katika mabustani yapitayo mito chini yake.
Mwalimu wetu Osanbay Soirkulov Ahmetoglu alizaliwa mnamo Januari 9, 1964 katika wilaya ya Yanjikurgan mkoa wa Namangan mashariki mwa Uzbekistan. Alisoma katika shule za Kyrgyzstan. Baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari, alihama akiwa na umri wa miaka kumi na tano ili kusoma sayansi za kidini kwa misingi ya imani na uchamungu wake. Tangu wakati huo ameboresha usomaji wake na kuongeza elimu yake, akihama kutoka darasa moja la siri hadi jengine, alielimishwa na wasomi wa kidini wa Asia ya Kati, na wakati huo huo akiwaelimisha wanafunzi wake. Mamake Ustadh Burlekan alikuwa na ushawishi mkubwa juu ya kujitolea kwa mwanawe kwa dini.
Inajulikana vyema kuwa katika miaka ya 1980, wakati dola ya Sovieti na upagani zilipofikia kilele chake, Muungano wa Sovieti uliitesa vikali dini yetu ya Kiislamu. Licha ya hayo, Ustadh huyu hakuacha kujifunza na aliendelea kujitahidi kusonga mbele. Baada ya kuanguka kwa Muungano wa Kisovieti katika miaka ya tisiini, makundi mengi yaliingia katika nchi yetu ndani ya muundo wa mfumo wa "uhuru wa imani" uliotetewa na mfumo ya kirasilimali. Ustadh Osanbei alijitahidi sana kutafuta jamii isiyo na hatia. Mnamo 1992, alichagua chama cha kisiasa cha Kiislamu, Hizb ut Tahrir, kutoka miongoni mwao.
Kuanzia siku hiyo na kuendelea, Ustadh alianza misheni yake ya kweli ya dawah na yeye na wanafunzi wake walijaribu kuupindua mfumo wa kikoloni wa kiulimwengu kupitia mapambano ya kisiasa ya kimfumo, na kuregesha tena mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu. Hivyo, Ustadh akawa mmoja wa waanzilishi katika nchi yetu, jambo ambalo lilileta usumbufu kwa mamlaka na mabwana zao wakoloni makafiri; kwa hiyo, walianza kumshinikiza na akatumia maisha yake uhamishoni hadi maadui wa dini hii wakamkamata.
Hatimaye, vibaraka hao wakatimiza lengo lao na kumtuhumu Ustadh kwa “msimamo mkali” na kumkamata mnamo Agosti 2012. Mwaka mmoja baadaye, mahakama ya Kara-Su ilimhukumu kifungo cha miaka mitano gerezani. Alipokuwa akitumikia kifungo chake gerezani, kesi hiyo ililetwa tena na Mahakama ya Jiji la Tash-Komur ikamhukumu kifungo cha miaka 16 gerezani mnamo Mei 19, 2014. Iliamuliwa kwamba hukumu hiyo ingetekelezwa katika taasisi ya kurekebisha tabia yenye utawala mkali. Baadaye, malalamiko yaliwasilishwa kwa Mahakama ya Rufaa, na hukumu ikafupishwa hadi miaka 10. Kwa hivyo, Ustadh aliachiliwa huru mnamo Mei 20 mwaka huu.
Ustadh amefariki leo, lakini ameacha wanafunzi wengi. Makafiri na watumwa wao musifanye haraka kufurahi; kwa sababu kazi ya Ustadh tayari imeshapitishwa kwa wanafunzi wa wanafunzi wake, yaani, kwa "wajukuu" wa wanafunzi na wanafanya kazi bila kuchoka bila kuacha, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Mwalimu wetu aliacha watoto saba. Tunatoa pole zetu nyingi kwa watoto wao, jamaa na wapendwa wao wengine. Pia tunamuomba Yey (swt) atupe sisi, familia yake na watu wake, subira, utulivu, na faraja njema.
Bila shaka macho yetu yanabubujika machozi, na nyoyo zetu zinahuzunika kutokana na vifo vya Waislamu, haswa kifo cha mwalimu wetu, ambaye aliubeba ulinganizi huu bila kuchoka katika maisha yake yote, lakini hatusemi ila yale tu yanayompendeza Mola wetu Mlezi (swt) pekee.
﴾إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah: 156]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kyrgyzstan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kyrgyzstan |
Address & Website Tel: http://hizb-turkiston.net |
E-Mail: [email protected] |