Jumamosi, 11 Shawwal 1445 | 2024/04/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kyrgyzstan

H.  15 Ramadan 1445 Na: 1445 H / 04
M.  Jumatatu, 25 Machi 2024

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mamlaka za Kyrgyzstan Zinayapiga Vita Maadili ya Kiislamu
(Imetafsiriwa)

Mamlaka za Kyrgyzstan zinafanya kampeni dhidi ya maadili ya Kiislamu, haswa mavazi ya Kiislamu, kwani kuna idadi kadhaa ya hatua zinazoonyesha hili. Kwa mfano, ilitajwa katika khutba za Ijumaa kwamba “niqab ya mwanamke wa Kiislamu na nguo nyeusi huwaweka watu mbali na dini.” Mnamo Machi 21, mkutano wenye kichwa “Kanuni za mavazi ya sharia ya wanawake” ulifanyika kati ya wanawake huko Kara-Suu katika eneo la Osh. Wazungumzaji katika kikao hicho walisisitiza kuwa uso wa mwanamke si 'Awra (sehemu ya mwili ya kusitiriwa), na mwanamke asiyefinika uso wake hana dhambi, na mwanamke aliyevaa nguo nyeusi na kujifinika mwili wake wote husababisha mkanganyiko kati ya watu katika jamii. Pia ilisisitizwa kwamba ni muhimu kupata elimu kutoka kwa taasisi rasmi za kidini, na kwamba elimu isiyo sahihi itasababisha kujiunga na mashirika yenye itikadi kali.

Mikutano kama hiyo pia ilifanyika katika taasisi na shule zingine za kidini katika eneo la Osh. Ilithibitisha kwamba Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu nchini Kyrgyzstan lilitoa taarifa kuhusu ulazima wa wanawake kufuata mila na desturi katika kanuni za mavazi wanapovaa nguo. Kwa ujumla, mikutano hii ilijadili hukmu za shariah zinazohusiana na kuzuia israfu, kuzuia misimamo mikali na ugaidi, kuongeza ufahamu kuhusu chanjo, na kanuni za mavazi ya sharia ya wanawake.

Hapo awali, Rais Sadyr Japarov alimpokea Mufti mpya Abdulaziz Dhakirov aliyechaguliwa hivi karibuni, na akaelezea wasiwasi wake kuhusu baadhi ya matukio ambayo hayakubaliani na maadili ya jadi ya Uislamu katika kueneza dini. Wakati wa mkutano huo, mada zilizotajwa katika mikutano hapo juu zilijadiliwa zaidi. Kabla ya hapo, Sharapatkan Majitova, mwanachama wa Baraza la Jogorku Kenesh (Bunge la Kyrgyzstan), alipendekeza rasimu ya sheria ya kupiga marufuku niqab na ndevu ndefu nchini Kyrgyzstan. Alitoa mfano wa ukweli kwamba Bunge la Uzbekistan lilipiga marufuku uvaaji wa niqab, na kubaini haja ya hatua kama hizo nchini Kyrgyzstan. Kisha, mkuu wa Kamati ya Serikali ya Usalama wa Kitaifa, Kamchibek Tashiyev, alisema kwamba niqab na ndevu ndefu zinapaswa kupigwa marufuku nchini Kyrgyzstan.

Inafahamika kuwa kampeni inayotekelezwa kusini mwa nchi yetu inatarajiwa kuendelea katika maeneo yote. Hatimaye mchakato wa kupambana na maadili ya Kiislamu kwa kisingizio cha misimamo mikali na ugaidi unawiana na maslahi ya serikali ya sasa ya kuanzisha udikteta nchini humo. Aidha, vita dhidi ya Uislamu ni hitaji la siasa za kimataifa. Kwa hiyo, vita dhidi ya Uislamu vimeenea katika nchi jirani za eneo hilo, na serikali hizi zinashindana katika suala hili. Kwa mfano, mamlaka za Turkmenistan, Tajikistan, Uzbekistan na Kazakhstan zinaendelea kupigana na Uislamu kwa kisingizio cha ndevu na niqab.

Bila shaka, vita vya mamlaka za Asia ya Kati dhidi ya Uislamu havikuanza ghafla. Mzozo huu daima ulianza baada ya kuondolewa kwa wapinzani na kuanzishwa kwa utawala wa kidikteta. Mnamo tarehe 5 Septemba mwaka jana, rasimu ya sheria iliwasilishwa kwa baraza dogo la Bunge la Uzbekistan juu ya kuweka adhabu za kiidara kwa wale wanaovaa niqab. Pia, unyama unaofanywa na dhalimu wa Tajikistan Emomali Rahmon na dhalimu wa Turkmenistan (baba na mwana) Berdimuhamedov dhidi ya Waislamu unaongezeka siku baada ya siku.

Nchini Kazakhstan, mchakato wa vita dhidi ya Uislamu unafanyika sambamba na Kyrgyzstan. Kwa mfano, katika mkutano wa kitaifa uliofanyika Atyrau mnamo Machi 15, Rais wa Kazakhstan, Kassym-Jomart Tokayev, aliwakashifu wanawake waliovaa nguo nyeusi, akitaja kuwa mwonekano kama huo haukuwa sehemu ya mila ya Kazakh. Pia, rasimu ya sheria zinazopiga marufuku ndevu na kuzuia wanafunzi wa kike kuvaa hijab (mtandio) na niqab katika shule za Kazakhstan bado lingani ni pendekezo hadi sasa.

Kwa kweli, kupiga marufuku niqab na ndevu kunakinzana na maadili ya kidemokrasia ambayo mamlaka hizo leo huyasifu. Kwa usahihi zaidi, uhuru wa dini na uhuru wa kibinafsi katika demokrasia humhakikishia mtu kuamini katika dini yoyote na kutumia sifa yoyote. “Maadili” haya ni sheria ya kikatiba ya serikali ya kisekula. Hata hivyo, Magharibi, ambayo ilikuwa chimbuko la demokrasia, tayari imeanza kuacha kanuni na maadili yake katika anga ya kimataifa. Kwa ufupi, uhuru huu unatumika tu dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ambapo, kwa mfano, uhuru wa kidini unatolewa ili kumwabudu Shetani au kutenda maovu mengine. Wasiokuwa Waislamu pia wanaruhusiwa kuvaa nguo zozote wanazotaka, na hata kwenda nje mabarabarani wakiwa uchi. Hata hivyo, linapokuja suala la maadili ya Kiislamu, suala hilo linachukuliwa kwa njia tofauti. Hili linadhihirika wazi katika marufuku ya Ufaransa ya kuvaa hijab (mtandio) shuleni mnamo 2004, kufukuzwa kwa wafanyikazi wa kike Waislamu kutoka kwa taasisi za umma, na marufuku ya kuvaa niqab katika maeneo ya umma mnamo 2010.

Mnamo 2021, Uswizi pia ilipitisha sheria ya kupinga niqab kupitia kura ya maoni. Chini ya sheria hii, wanawake wa Kiislamu wamepigwa marufuku kuvaa niqab katika maeneo ya umma. Kadhalika, wanaume hawawezi kuwalazimisha wanawake kuvaa hijab. Kwa njia hii, nchi za kibepari zinakanyaga uhuru wanaoutukuza, moja baada ya mwingine. Kutelekeza huko kwa fikra na maadili yao kunamaanisha kuwa Mfumo wao umefika ukingoni mwa shimo. Yaani, mashambulizi dhidi ya maadili ya Kiislamu yanaashiria kuwa ubepari unakabiliwa na mgogoro wa kifikra.

Nchi za Asia ya Kati zinazichukulia sheria za kidikteta za China kuwa mfano wa kuigwa, hasa katika vita vyao dhidi ya maadili ya Kiislamu. Baada ya yote, China haipaswi kukabiliana na maandamano kutoka kwa idadi ya Waislamu wa ndani wakati wa kutekeleza miradi mikubwa inayohusiana na mustakabali.

Kwa mfano, serikali ya China imepiga marufuku wanaume kufuga ndevu ndefu “kinyume na asili” na wanawake kuvaa hijab hadharani, katika Eneo linaojitawala lenyewe la Xinjiang Uyghur. Kabla ya kupitisha sheria hii, serikali ya China hapo awali ilikandamiza jamii za Waislamu kwa nguvu. Kisha ikaanza kupambana na Waislamu kwa kisingizio cha kupambana na magaidi. Mwanzoni Waislamu hawakujali miradi ya Wachina washirikina; waliamini habari iliyochapishwa na vyombo vya habari vya China na kubaki wajinga, wakiamini kwamba “baada ya kuwaondoa magaidi, Wachina wapagani watatuacha peke yetu”! Lakini haikuwa hivyo. Leo hii, serikali ya kipagani ya China imeligeuza eneo la Xinjiang kuwa gereza la wazi kwa Waislamu kwa kisingizio cha ugaidi, misimamo mikali na kujitenga.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliisifia hali yetu ya sasa, akisema:

«يُوْشِكُ أَنْ تَدَّاعَى عَلَيْكُمُ الْأُمَمُ مِنْ كُلِّ أُفُقٍ كَمَا تَدَّاعَى الْأَكَلَةُ عَلَى قَصْعَتِهَا» قَالَ: قُلْنَا يَا رَسُوْلَ اللهِ أَمِنْ قِلَّةٍ بِنَا يَوْمَئِذٍ؟ قالَ: «أَنْتُمْ يَوْمَئِذٍ كَثِيْرٌ، وَلَكِنْ تَكُوْنُوْنَ كَغُثَاءِ السَّيْلِ، يُنْتَزَعُ الْمَهَابَةُ مِنْ قُلُوْبِ عَدُوِّكُمْ وَيُجْعَلُ فِيْ قُلُوْبِكُمُ الْوَهْنُ» قُلْنَا وَمَا الْوَهْنُ؟ قَالَ: «حُبُّ الدُّنْيَا وَكَرَاهِيَّةُ الْمَوْتِ»

“Watu hivi punde wataalikana kukushambulieni kama walaji wanavyoalikana kuizunguka sahani ya chakula. Tukauliza: Je, kwani tutakuwa wachach siku hiyo? Akajibu: Hapana, bali siku hiyo mutakuwa ni wengi, lakini mutakuwa kama povu na taka zinazosombwa na mafuriko, na Mwenyezi Mungu ataondoa hofu kwenu kutoka kwa nyoyo za maadui zenu, na atajaaliya katika nyoyo zenu wahn. Tukauliza: Wahn ni nini? Akasema: ni kuipenda dunia na kuchukia mauti.” [Abu Dawud]

Kwa kumalizia, Makafiri hawapigi vita tu baadhi ya makundi ya Kiislamu au mtazamo wowote wa Kiislamu, bali wanapiga vita Uislamu na Waislamu. Kimaumbile, Ummah hauwezi kuondokana na hali hii isipokuwa kwa kurudi kwenye Uislamu wake na kutangaza tena Khilafah kwa njia ya Utume. Ama kuhusu matukio ya sasa yenye dhihirisho la chuki dhidi ya Uislamu, Waislamu wanatakiwa kujibu kila shambulizi na kujitolea mhanga kwenye njia hii.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Kyrgyzstan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kyrgyzstan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-turkiston.net
E-Mail: webmaster@hizb-turkiston.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu