Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  17 Muharram 1444 Na: H.T.L 1444 / 01
M.  Jumatatu, 15 Agosti 2022

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

(مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا)

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon inamuomboleza kaka mbeba dawah, Jamal Suleiman Abu Khaled, aliyefariki alfajiri ya leo, Jumatatu, 17 Muharram 1444 H, sawia na 15/08/2022, akiwa na umri wa miaka 59.

Abu Khaled Suleiman, mmoja wa watu wa mwanzo wa ulinganizi huu katika miji ya Sidon na Tiro na viunga vyake, aliibeba dawah kwa uaminifu na ikhlasi. Sisi tunamchukulia vivyo hivyo, na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye hesabu yake, na hatumsifu yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu, katika siku zake ngumu na dhurufu zenye kiza kikubwa, na dawah ilimjua tu kama mtu mwenye tabia njema, mshikamano mwema, makini na mvumilivu ndani yake, akiipenda dawah na kizazi chake kichanga.

Abu Khaled alikuwa mwenye utambuzi wa kifikra, mwenye maoni yaliyo wazi, sahihi, na ufahamu sawasawa. Kijana mmoja alimuuliza siku moja: Ulinganizi huu tutaubeba kwa muda gani? Akajibu: “Mpaka kufa, na akasoma maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

(وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّى يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ)

 “Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.” [Al-Hijr:99]” na ndivyo alivyokuwa. Hakubweteka katika wajibu au kazi yoyote, hata iwe nyingi kiasi gani, hadi siku za mwisho za uhai wake, Mwenyezi Mungu (swt) amrehemu.

Abu Khaled alifanya kazi ya kusimamisha Khilafah, na aliiona imesimama mbele yake, akiwa na yakini na ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na bishara njema ya Mtume Wake, rehema na amani zimshukie yeye na jamaa zake.

Jicho linatokwa na machozi, moyo unahuzunika, na sisi tumehuzunishwa na kutengana nawe, na hatusemi ila tu yanayompendeza Mola wetu.

(إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ)

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara:156].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu