Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  9 Dhu al-Hijjah 1441 Na: 1441/11
M.  Alhamisi, 30 Julai 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon inamuomboleza shahidi Ahmed Saleh Al-Ali, ambaye mauwaji yake yaliothibitika kufanywa na mikono ya serikali ya kihalifu ya familia ya Assad nchini Syria, baada ya miaka mingi ya kukosekana kwake mnamo 1980 katika magereza ya dikteta aliyefariki Hafez al-Assad.    

Shahidi huyu shujaa hakika alibeba ulinganizi wa kuregesha maisha kamili ya Kiislamu na kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume ubebaji wa kweli, kuanzia Lebanon, hadi Uturuki, kisha Syria, akiwacha nyuma yake mapambo ya maisha ya dunia, akimuelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu, mpaka akawa miongoni mwa mabwana wa mashahidi, hivi ndivyo tunavyo muhisabu, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi, kwa kusadikisha Hadith ya Mtume (saw):

«سَيِّدُ الشُّهَدَاءِ حَمْزَةُ بْنُ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، وَرَجُلٌ قَامَ إِلَى إِمَامٍ جَائِرٍ فَأَمَرَهُ وَنَهَاهُ، فَقَتَلَهُ»

“Bwana wa mashahidi ni Hamza ibn Abdul Mattalib, na mtu anayesimama mbele ya mtawala jeuri akamuamrisha mema na kumkataza maovu kisha (mtawala huyo) akamuua (kwa sababu hiyo).”

Na sisi tunapomuomboleza leo baada ya kuthibitika shahada yake, mikononi mwa madhalimu, hakika damu ya Ahmed Saleh Al-Ali, na waliomtangulia na baada yake miongoni mwa ndugu zetu, katika da'wah hii nzuri na iliyo barikiwa, haitapotea bure kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kesho iliyo karibu mno itasimama Dola ya Kiislamu, Khilafah kwa Njia ya Utume, na italipiza kisasi kikali kwa madikteta madhalimu, na itanyanyua jina la Ahmed Saleh Al-Ali na ndugu zake, wanaume katika njia ya da'wah hii, na viigizo vyema vinavyoigwa katika subira na msimamo na kujitolea katika kuregesha maisha kamili ya Kiislamu na kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume.

Mwenyezi Mungu akukubalie Ewe Abu Muhammad, na akupandishe katika Pepo ya 'Iliyeen' pamoja na mitume na wakweli na mashahidi na watu wema na hao ndio marafiki wazuri, na waliosalia nyuma katika ndugu zako miongoni mwa wabebaji da'wah, na wanaofuata nyayo zako, ni watu wema, wanaobeba bendera (liwa'a) ya ulinganizi kwa subira na msimamo na uume.

 [وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.”[Yusuf: 21]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu