Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  9 Rabi' I 1446 Na: HTM 1446 / 07
M.  Alhamisi, 12 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tunahitaji Sana Khilafah Kuilinda Bahari ya China Kusini

(Imetafsiriwa)

Mgogoro wa Bahari ya China Kusini umeibuka tena kufuatia kuvuja kwa waraka wa kidiplomasia kutoka Jamhuri ya Watu wa China (PRC) kwa Ubalozi wa Malaysia jijini Beijing, wa tarehe 18 Februari. Ujumbe huo ulifichua pingamizi ya China na kuitaka Malaysia kusitisha shughuli za utafiti wa mafuta na gesi huko Beting Raja Jarum na Beting Patinggi Ali, maeneo ya ndani ya Visiwa vya Spratly. Makala moja inayohusiana na dokezo hili ilichapishwa na chombo kimoja cha habari cha Ufilipino mnamo Agosti 29. Muda mfupi baadaye, mnamo Septemba 7, meli ya kijeshi ya China na walinzi wa pwani ilionekana ikifanya kazi ndani ya Eneo la Kiuchumi la Kipekee la Malaysia (EEZ) karibu na Sarawak. Wizara ya Mambo ya Nje, huku ikithibitisha kufahamu hali hiyo, ilijizuia kutoa maoni zaidi.

Waziri Mkuu Datuk Seri Anwar Ibrahim hivi karibuni alielezea nia yake ya kushiriki katika mazungumzo na China kuhusu mzozo unaoendelea wa eneo kuhusu Bahari ya Kusini ya China. Msimamo huu unawakilisha mabadiliko kutoka kwa msimamo wa muda mrefu wa Malaysia, ambao unakataa madai ya China katika eneo hilo. Nchi zinazohusika katika mzozo huo - Malaysia, Vietnam, Ufilipino, na Brunei - zote zina madai yanayopishana ya EEZ na rafu za bara. Licha ya “onyo” la China, serikali ya Malaysia imesisitiza dhamira yake ya kuendelea na utafiti wa mafuta na gesi katika eneo linalozozaniwa, huku pia ikisisitiza kujitolea kwake kutatua migogoro kwa njia za amani, kwa kutumia mashauriano na mazungumzo ndani ya mifumo iliyopo ya kidiplomasia ili kuepusha migogoro. Uwepo wa mara kwa mara wa manuari za China katika Bahari ya China Kusini, hasa ndani ya EEZ ya Malaysia, haujaleta mwitikio mkubwa kutoka kwa Malaysia. China inaonekana kuiona Malaysia kama nchi ndogo na iliyo hatarini, na kwa sababu hiyo, haishangazi kwamba China mara kwa mara huingilia maji ya Malaysia, hata kufikia kutoa maonyo kuhusu shughuli za Malaysia katika EEZ yake yenyewe, ambayo China inaidai.

Majibu ya Waziri Mkuu wa Malaysia katika suala hili ni ya kutatanisha. Anwar Ibrahim anataka kujadiliana na chama kinachokusudia kulivamia eneo la Malaysia! Je, mtu anawezaje kuhalalisha mazungumzo na chama ambacho hakina madai halali, hasa wakati kinakandamiza haki zetu za ubwan? Mtazamo huu unaonekana kuakisi msimamo wa Anwar kuhusu mamlaka ya ardhi, akiregelea msimamo wake kuhusu suluhisho la dola mbili la Palestina - kujadiliana na mvamizi na kusalimisha sehemu kubwa ya haki zetu. Utayari wa Anwar kushiriki katika mazungumzo na China sio tu unasisitiza udhaifu wa Malaysia lakini pia unaipa China fursa ya kusisitiza madai yake juu ya bahari ya Malaysia. Onyesho hili la mazingira magumu linaweza kusababisha kupunguzwa kwa eneo la bahari ya Malaysia kutokana na mazungumzo haya. Anwar amejaribu kuhalalisha msimamo wake kwa kuuliza swali, “Je, tunataka vita (na China) badala ya mazungumzo?” Kauli hii inasimama kinyume kabisa na matamshi yake wakati wa sherehe za hivi majuzi za Siku ya Uhuru, ambapo alikosoa uongozi uliopita kwa kupoteza kisiwa cha Batu Puteh kwenda Singapore. Anwar alisisitiza sana umuhimu wa kutetea kila shubiri ya eneo letu dhidi ya uvamizi wa kigeni, akitangaza kwamba mataifa mengi yameingia vitani ili kulinda haki zao. Swali la kusisitiza sasa ni: ni upi mtazamo wa Anwar kwa China?

Anwar anaonekana kusisitiza “tishio la vita” kutoka China, licha ya kukosekana kwa taarifa rasmi kutoka China kwa athari hiyo. Mantiki yake inaonekana kufuata kanuni ya kuchagua “la hafifu ya maovu mawili” - kuepuka madhara makubwa kwa kukubali la hafifu. Kupitia hoja hii, anaweza kuwa anajaribu kuwatayarisha watu wa Malaysia kwa ajili ya kukubali hatimaye kukabidhi baadhi ya maeneo ya bahari ya Malaysia kwa China. Iwapo wavamizi wanaendelea kukiuka haki zetu, na tukajibu kwa kufanya mazungumzo, hii haiashirii tu kusalimisha eneo bali pia kupoteza heshima na nguvu. Katika hali kama hii, uwepo wa vikosi vyetu vya jeshi unakuwa wa kutiliwa shaka, kwani kitendo chochote cha uchokozi kingekutana tu na mazungumzo!

Ni kweli kwamba China inamiliki nguvu kubwa, inayoiruhusu kufanya kutenda bila kuzingatia sheria katika Bahari ya China Kusini, mara nyingi ikipuuza haki za nchi jirani. Hata hivyo, utawala wa China hautokani na nguvu zake pekee bali pia unatokana na udhaifu na usaliti wa watawala wa Waislamu. Umma wa Kiislamu kiasili una nguvu, na jeshi la kutisha na shupavu. Hata hivyo, kundi la simba hakika haliwezi kuinuka likiongozwa na mbwa! Tangu kuanguka kwa Khilafah zaidi ya karne moja iliyopita, Ummah umekuwa bila Khalifa, ambaye Mtume Muhammad (saw) alimsifu kuwa ni ngao ambayo nyuma yake Ummah unapigana na kulindwa. Kwa sababu hiyo, ardhi za Waislamu zimekuwa hatarini kwa uvamizi wa adui.

Wakati wa utawala wa Khilafah, ilikuwa dhahiri kwamba nguvu zake za kijeshi ziliiwezesha kutawala sehemu kubwa ya bahari za dunia na njia kuu za baharini. Dola zisizokuwa za Kiislamu zilijizuia kupambana na mamlaka ya Khilafah. Kuasisiwa kwa jeshi la wanamaji la Kiislamu kulianzia zama za Makhalifa Waongofu. Chini ya Bani Umayya, Khilafah ilivunja ukuu wa jeshi la wanamaji la Kirumi, na kuwafanya Waislamu kuwa kikosi kikuu cha majini kote duniani. Utawala huu ulienea kutoka Mediterania hadi Bahari Nyekundu, Ghuba ya Uajemi, na Bahari Hindi. Urithi huu uliendelezwa na Makhalifa wa Abbas na Uthmani, ambao walidhibiti njia za biashara zinazounganisha Mashariki na Magharibi, na kuwalazimisha wafanyibiashara wa Ulaya kuvuka ardhi za Kiislamu hadi India na China.

Malaysia itasalia kuwa ndogo na dhaifu maadamu inajifunga kwenye mfumo wa dola ya kitaifa na kutawaliwa na viongozi wasio na nia ya kuuinua Uislamu duniani. Hali hiyo hiyo inapatikana kwa Umma wa Kiislamu, ambao hautaregesha hadhi yake ya kuwa taifa lenye nguvu zaidi na la kupigiwa mfano maadamu tu inaongozwa na viongozi waoga na wafisadi. Njia pekee ya kutwaa tena nafasi yetu kama dola kuu ya kimataifa na kulinda ardhi na maji yetu iko katika kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume (al-Khilafah ar-Rashidah ala Minhaj Nubuwwah). Kwa nguvu zake na kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, Khilafah itafikia ushindi mtawalia, ikitawala Mashariki na Magharibi kwa Uislamu, na hivyo basi kueneza Rehema Zake (swt) kama alivyoahidi Yeye (swt).

Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Malaysia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor
Tel: 03-8920 1614
www.mykhilafah.com
Fax: 03-8920 1614
E-Mail: htm@mykhilafah.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu