Jumatatu, 25 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  15 Rabi' II 1446 Na: HTM 1446 / 10
M.  Ijumaa, 18 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ikiwa Sera ya Mambo ya Nje ni Kufanya Urafiki na Adui, Basi Ziara ya Adui Hakika Itakaribishwa!

(Imetafsiriwa)

Kuwasili kwa manuari mbili za China huko Penang kumezua maswali na ukosoaji unaoendelea kuelekezwa kwa serikali. Kabla ya hali hiyo kuburudi, Malaysia ilikuwa mwenyeji wa manuari ya Urusi katika jimbo hilo hilo. Ziara ya Jopo Kazi la 83 la Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA), ndani ya Meli ya Mafunzo ya Qi Jiguang na Meli ya Jinggang Shan mnamo tarehe 5 Oktoba, imeibua maswali mengi. Kuchelewa kwa serikali kujibu suala hili pamoja na maelezo yaliyotolewa na baadhi ya mawaziri si tu kwamba imeshindwa kuondoa wasiwasi bali pia imesababisha kuongezeka kwa udadisi. Mawaziri kadhaa wameeleza kuwa uwepo wa meli hizo unaashiria ziara ya kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Malaysia. Kinyume chake, serikali ya Penang ilisema kuwa meli hizo mbili zilitia nanga nchini Malaysia zikielekea Bangladesh kabla ya kuanza mazoezi yao katika Bahari Hindi.

Licha ya uthibitisho wa serikali kwamba uwepo wa meli za kivita za China ulifanywa na kuidhinishwa kupitia njia rasmi, maswali yanabaki. Kwa mfano, kwa nini Penang ilichaguliwa kuwa jimbo la kuzuru, na kwa nini viongozi wa majimbo pekee ndio walihusika katika hafla ya kukaribisha badala ya viongozi wa kitaifa? Zaidi ya hayo, kwa nini maadhimisho ya miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia yanaonekana kuhusisha zaidi ushiriki wa China wa Malaysia? Waziri wa Elimu alithibitisha kuwa ziara hiyo haikufanywa na jeshi la China bali ilihusisha makada na wahadhiri 165 kutoka Chuo Kikuu cha Wanamaji cha China. Hii inazua maswali zaidi kwa nini walitembelea shule ya kibinafsi ya China badala ya Chuo Kikuu cha Ulinzi cha Kitaifa cha Malaysia, ambayo ingefaa zaidi. Ripoti zinaonyesha kwamba manuari hizo mbili zilibeba zaidi ya wafanyikazi elfu moja, na hivyo kusababisha uvumi kuhusu utambulisho wa wale ambao hawakuwa kadeti—je, hawakuwa sehemu ya jeshi la China lenyewe? Maswali na shaka hizi zote ni halali na zinahitaji majibu ya uwazi na mantiki kutoka kwa serikali, kwani umma unatafuta ufafanuzi ikiwa hii ndio njia mwafaka kwa Malaysia na China kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi walifafanua kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa manuari za kigeni kutia nanga nchini Malaysia kama “bandari ya mapumziko ya muda.” Meli nyingi za kivita kutoka nchi mbalimbali zimeruhusiwa kutia nanga hapa kutokana na uhusiano wa kidiplomasia ulioanzishwa kati ya Malaysia na nchi hizo. Wakati serikali inajaribu kufifisha athari za ziara hizi na uwepo wa vyombo hivyo, suala hili si dogo kwa mtazamo wa Kiislamu. Katika Uislamu, uhusiano wetu na nchi nyingine, hasa zile zenye uadui na Uislamu, lazima ujengwe sio tu katika misingi ya hekima na umakini, bali muhimu zaidi, lazima uzingatie hukmu za Mwenyezi Mungu (Ahkaam Shar'iah) kuhusiana na sera ya kigeni.

Tunataka kuikumbusha serikali ya Malaysia kwamba kwa nchi zilizoainishwa kama al-Muharibah Fi'lan (nchi za vita ambazo kivitendo zinapigana na Ummah), hakuna uhusiano wa aina yoyote unaoruhusiwa isipokuwa vita, na raia wake hawaruhusiwi kuingia nchi yetu kwa hali yoyote ile. Kwa nchi zilizoainishwa kama al-Muharibah Hukman (nchi za vita ambazo kiuhalisia haziko katika vita na Ummah), lazima tuwe waangalifu. Kuanzisha uhusiano wowote wa kidiplomasia nazo hairuhusiwi. Kwa hakika, China na Urusi zinaangukia katika kundi la al-Muharibah Hukman, zikionyesha matamanio ya wazi ya kudhibiti nchi za Kiislamu na Ummah. Ingawa wawakilishi au raia kutoka nchi kama hizo wanaweza kuingia katika eneo letu kwa ruhusa (visa na pasipoti), inabakia kuwa ni marufuku (Haram) kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia nazo.

Inasikitisha kwamba Malaysia inaendelea kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na China (na pia Urusi), licha ya ukatili uliothibitishwa na ukandamizaji unaofanywa na nchi hiyo ya kikomunisti dhidi ya Waislamu wa Uighur kwa miongo kadhaa. Mbali na uhusiano wa kidiplomasia, Malaysia pia imeanzisha uhusiano mkubwa wa kibiashara na China, na kuifanya kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa nchi hiyo. Hii inaakisi sera ya kigeni ya Malaysia kuelekea China—kukuza uhusiano wa kirafiki na nchi ambayo ina chuki na Waislamu. Vile vile inaweza kuzingatiwa katika sera ya kigeni ya Malaysia kuelekea Urusi, India, Marekani, na nchi nyingine zenye vita, licha ya upinzani wao wa wazi dhidi ya Uislamu. Sawa na nchi nyingine za kibepari, mahusiano ya kimataifa ya Malaysia kimsingi yanaendeshwa na maslahi ya kiuchumi.

Hivi karibuni, Waziri Mkuu Datuk Seri Anwar Ibrahim alielezea fahari yake kwa urafiki wa Malaysia na nchi zote kuu kutoka kambi za Magharibi na Mashariki, akiangazia mafanikio ya nchi katika eneo hili. Kwa hiyo, haishangazi kwamba manuari za China hazikuruhusiwa tu kutia nanga nchini Malaysia bali pia zilipokelewa kwa ukarimu! Kwa kile kilichotokea, ni haki kwa hiyo kwa wananchi kutoa ukosoaji wao kuhusu hatua za serikali juu ya suala hili, kuakisi wasiwasi na hafu yao juu ya uingiliaji wa kigeni nchini. Walakini, kama Waislamu, ni muhimu kutambua kwamba suala hilo linaenea zaidi ya uwepo au ziara ya manuari za China. Inajumuisha uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia ambao umekuzwa kati ya Malaysia na China, nchi yenye uhasama ambayo Malaysia, tangu mwanzo, haikupaswa kujihusisha nayo. Lazima tuwe macho dhidi ya mataifa kama haya ambayo yana nia ya kudhibiti nchi yetu kwa njia mbalimbali. Zaidi ya hayo, ziara ya timu ya kadeti ya China katika taasisi za elimu katika nchi yetu haipaswi kuchukuliwa kirahisi, kwani inaakisi mbinu ya kihistoria iliyochukuliwa na wamisionari kujipenyeza katika dola ya Kiislamu (Khilafah), kwa lengo la kuhujumu na kuitawala Khilafah kupitia njia za elimu— mkakati ambao hatimaye ulionekana kuwa na ufanisi baada ya muda.

Kwa hili tunaikumbusha serikali kuachana na sera za kigeni zinazokwenda kinyume na sheria za mungu ili kuepusha nchi hii kuingia katika mawindo ya maadui ambao mara kwa mara wanatafuta fursa za kututawala. Sambamba na hilo, tunapenda kuwakumbusha Umma wa Kiislamu kwamba serikali inayopuuza sheria za Mwenyezi Mungu haitoi manufaa yoyote, na haifai tena kuongoza nchi. Malaysia itasalia kuwa dhaifu, iliyovuliwa utu wake na kujiweka mbali na rehma za Mwenyezi Mungu (swt), maadamu hukmu Zake zinapuuzwa katika utawala wa serikali.

Enyi Waislamu! Jueni kwamba Hizb ut Tahrir imekuwa ikifanya kazi kwa bidii tangu 1953, duniani kote, kuregesha Ukhalifa Ulioongoka (Khilafah Rashida) kwa Njia ya Utume. Dola hii itaasisiwa juu ya itikadi ya Kiislamu; haitalegeza msimamo, wala kuwasujudia, maadui; itaregesha sera ya kigeni ya Kiislamu ya kueneza Da’wah na Jihad kwa nchi za kivita; na itaibuka kwa mara nyengine tena kama dola kuu yenye nguvu isiyo na kifani, Insha Allah.

Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Malaysia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor
Tel: 03-8920 1614
www.mykhilafah.com
Fax: 03-8920 1614
E-Mail: htm@mykhilafah.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu