Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  15 Jumada I 1446 Na: HTM 1446 / 12
M.  Jumapili, 17 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Baada ya Mwaka Mmoja wa Mauaji ya Halaiki (na Miaka 76 ya Ukaliaji Kimabavu), Watawala wa Ruwaibidha Wakusanyika Tena Kuendeleza Kejeli na Usaliti wao

(Imetafsiriwa)

Ni mwaka mmoja kamili baada ya watawala wa Waarabu na Waislamu kukusanyika kujadili kadhia ya Palestina kufuatia mkasa wa Oktoba 7, wanakutana tena mahali pale pale, pamoja na mtu yule yule, wakishughulikia tatizo lile lile, na hatimaye kutoa maazimio yale yale! Zaidi ya viongozi 50 wa dola za Waislamu walihudhuria Mkutano wa Waarabu na Waislamu mnamo tarehe 11/11/2024, akiwemo Waziri Mkuu wa Malaysia. Kwa kutabiriwa, mapendekezo yaliyochakaa yaliwasilishwa, na Mkutano huo ulihitimishwa kwa maazimio yaliyochakaa vilevile. Kikubwa kinachotolewa na watawala hao ni kulaani mauaji ya halaiki ya Gaza na ‘Israel’ na kuomba Umoja wa Mataifa (UN) - shirika lile lile lililohusika na kuzaliwa kwa umbile halifu la Kiyahudi.

Tumechoshwa na maneno matupu ya watawala hawa Ruwaibidha. Wanakutana kitajiri na kifahari huku Gaza ikikabiliwa na uharibifu usio na kifani, mateso, na njaa—yanayojitokeza mbele ya macho yao. Sio kutojua suluhisho la kweli la kadhia ya Palestina ambayo inawazuia bali ni kukataa kwa makusudi kuchukua hatua. Majadiliano yao juu ya kusaidia wahasiriwa yanatumika kama kisingizio tu, kinachoonyesha kuwajali Waislamu huku wakiruhusu muindaji (Mayahudi) kuhangaisha na kuua windo lake (Waislamu). Suluhisho la Palestina liko wazi kuwa ni kuwaondoa madhalimu hao kwa njia ya Jihad Fi Sabilillah (kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu), na watawala hao wana uwezo wa kuyakusanya majeshi yao lakini wamepatwa na maradhi ya kiroho na kukosa utashi wa kutenda. Mwenyezi Mungu (swt) anaelezea hali yao:

[وَلَوْ أَرَادُوا الْخُرُوجَ لَأَعَدُّوا لَهُ عُدَّةً وَلَٰكِنْ كَرِهَ اللَّهُ انْبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ وَقِيلَ اقْعُدُوا مَعَ الْقَاعِدِينَ]

“Na ingeli kuwa kweli walitaka kutoka bila ya shaka wangeli jiandalia maandalio, lakini Mwenyezi Mungu kachukia kutoka kwao, na kwa hivyo akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanao kaa!” [At-Tawbah (9): 46].

Nguvu iko mikononi mwao; wangeweza kuhamasisha majeshi yao kwa amri moja lau wangetaka, lakini wanachagua kutotenda. Badala yake, wao hutumika kama “walinzi” wa umbile halifu la Kiyahudi, wakihakikisha hai wake. Wanazuia kwa uangalifu mwanajeshi, bomu, ndege ya kivita, kifaru au hata risasi moja iliyo chini ya udhibiti wao kufika ‘Israeli.’ Wanaepuka hata kutamka neno “Jihad” dhidi ya ‘Israeli.’ Hiki ndicho kiwango cha “ulinzi” wao kwa umbile hilo halifu.

Ni jambo lisilopingika kwamba Marekani na Umoja wa Mataifa zinalinda umbile la Kiyahudi. Hata hivyo, bila ya “huduma kubwa” ya watawala Ruwaibidha, umbile hili halifu lingekuwa limetoweka kwa muda mrefu kwenye ramani ya dunia. Kama msomi mmoja alivyosema, ‘Israel’ ni kivuli cha tawala za Kiarabu; kifo chake kimefungwa kwao. Leo, ‘Israel’ sio tu kivuli cha tawala za Waarabu bali pia watawala wote wa Waislamu! Watawala hawa Ruwaibidha ndio “kuba la chuma” halisi la ‘Israel’! Mikusanyiko yao, ambayo kamwe haina lengo la kuikomboa Palestina, ni khiyana za waziwazi kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw), waumini, na Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, zinazofanywa bila haya. Maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) yanaendana na ukweli: «إِذَا لَمْ تَسْتَحْيِ فَاصْنَعْ مَا شِئْتَ» “Ikiwa hauoni haya, basi fanya upendavyo” [Al-Bukhari].

Enyi Waislamu! Watawala wenu wanajifanya kutetea Palestina, lakini wakati huo huo wanalinda ‘Israel’. Kwa hakika, hakuna kheri katika watawala kama hawa. Kwa hili tunapenda kusisitiza tena kwa mara ya kumi na moja, kwamba njia pekee ya kuwasaidia ndugu na dada zetu huko Gaza na kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ni kupitia uhamasishaji wa majeshi ya Waislamu, ya karibu na ya mbali, kuitikia amri za Mwenyezi Mungu (swt); kuandamana kwa Takbir na Tahmid; kubeba bendera ya Mtume (saw); kwa lengo na sababu moja ambayo ni kupigana na Mayahudi na kuiregesha ardhi ya Isra' na Mi'raj kwa mmiliki wake halali. Hili ndilo suluhisho la pekee kwa Palestina—si kwa mikutano ya kilele, ususiaji, kusitisha mapigano, usaidizi wa Umoja wa Mataifa, achilia mbali matamshi matupu ya watawala Ruwaibidha.

Enyi majeshi ya Waislamu! Wajibu wenu kwa Palestina ni mkubwa sana, na kadhalika thawabu na dhambi zinazohusika. Mnajua watawala wenu hawatakuongozeni kuchukua hatua. Mkiwatii na kujitenga na amri ya Mwenyezi Mungu ya kufanya Jihad, mtabeba dhambi kubwa na udhalilifu. Lakini mkijiepusha na watawala hawa na kumtii Mwenyezi Mungu, malipo yenu na utukufu wenu ni mkubwa. Tunakuombeni mara kwa mara na hatutaacha kulingania - toeni Nusrah yenu (msaada wa kimada) kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Khalifa atakuhamasisheni na kukuongozeni kwa ujasiri wa kuwashinda Mayahudi, kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, na kufikia moja ya izza mbili zilizoahidiwa - ushindi au kifo cha shahada.

[قُلْ هَلْ تَرَبَّصُونَ بِنَا إِلَّا إِحْدَى الْحُسْنَيَيْنِ وَنَحْنُ نَتَرَبَّصُ بِكُمْ أَنْ يُصِيبَكُمُ اللهُ بِعَذَابٍ مِنْ عِنْدِهِ أَوْ بِأَيْدِينَا فَتَرَبَّصُوا إِنَّا مَعَكُمْ مُتَرَبِّصُونَ]

“Sema: Hivyo mnatutazamia litupate lolote isipo kuwa moja katika mema mawili? Na sisi tunakutazamieni kuwa Mwenyezi Mungu akufikishieni adhabu itokayo kwake, au kutokana na mikono yetu. Basi ngojeni, nasi tunangoja pamoja nanyi.” [At-Tawbah (9): 52].

Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Malaysia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor
Tel: 03-8920 1614
www.mykhilafah.com
Fax: 03-8920 1614
E-Mail: htm@mykhilafah.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu