Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  3 Jumada II 1444 Na: 1444/06
M.  Jumanne, 27 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Je, kuna Matumaini kwa Misri chini ya Mfumo wa Kirasilimali na Sheria zake?!

Je, Migogoro ya Kiuchumi ya Misri Itakwisha Lini na ni nani mwenye Masuluhisho Sahihi?!
(Imetafsiriwa)

Hakuna sauti iliyokubwa kubwa zaidi kuliko sauti ya misukosuko ya kiuchumi inayoikumba Misri na watu wake, ikiteketeza nguvu na juhudi zao, na kupoteza pamoja nao akiba zao. Mikopo na mikopo mipya ya kulipa maregesho ya mkopo, ikifuatiwa na sera na maamuzi na kufuja mabaki ya utajiri na mali ya Misri. Huu ni urasilimali ambao hautoi asali, bali unanyonya damu ya watu hadi tone la mwisho, na hivi ndivyo hasa unavyoifanyia Misri na watu wake.

Ripoti ya Wizara ya Fedha ilionyesha kuwa mapato ya deni la riba yalitawala 46.5% ya matumizi ya Misri katika robo ya kwanza ya mwaka wa sasa wa fedha Julai-Septemba 2022, ikirekodi pauni bilioni 216.940, kati ya matumizi ya jumla ya pauni bilioni 466.4, mapato ya riba ya nje ya nchi yakifika kiasi cha pauni bilioni 18.7 bilioni 197.950 bilioni katika mapato ya ndani kwa mashirika yasiyo ya kiserikali, na pauni milioni 268 kwa vitengo vya ndani (vitengo vya serikali kuu). Nakisi ya jumla ya bajeti ya Misri ilipanda hadi 2.27% ya Pato la Taifa katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha, kwa thamani ya EGP 206.77 bilioni, ikilinganishwa na nakisi ya 12.2% ya Pato la Taifa katika kipindi kama hicho cha mwaka wa fedha uliopita. Nakisi hii ilitokana na kuongezeka kwa mapato kwa asilimia 15.5 katika kipindi kilichotajwa hadi kufikia pauni bilioni 258.8, ikilinganishwa na pauni bilioni 223.9 katika kipindi sawia cha mwaka wa fedha uliopita, ikilinganishwa na ongezeko la gharama kwa 19% kufikia Pauni bilioni 466.4, ikilinganishwa na pauni bilioni 391.3 katika kipindi sawia cha mwaka jana. (Gazeti la Al-Mal 25/12/2022).

Ripoti iliyopita inahusu kile ambacho mapato ya madeni ya riba huliwa, basi vipi kuhusu madeni yenyewe na vipi kuhusu maamuzi yanayoambatana nayo ambayo yanawapa wakopeshaji utawala kamili juu ya Misri na utajiri wake, maamuzi na sera zake, na vile vile kuwafanya watu wake kuwa watumwa na kuhakikisha utiifu wake kwa Magharibi kwa miongo kadhaa ijayo?! Nakisi ya kudumu katika bajeti inashughulikiwa na mikopo mipya inayoongeza ukali wa nakisi na kuongeza kiwango cha mfumko wa bei na kiwango cha umaskini. Suluhisho bovu la kibepari kwa migogoro ambayo iliisababisha na ambayo Misri iliweza kutumiwa kwa rasilimali na utajiri wake, ikiwa tu serikali ilizitumia vyema.

Mgogoro wa halisi wa Misri hauko katika umaskini, uhaba wa rasilimali, au kukosekana kwa wale ambao wanaweza kushughulikia rasilimali hizi na kuzalisha mali kutoka kwao kwa kuwa ina wingi wa rasilimali na kawi, na inaweza, baada ya muda, kupata uzoefu, bali mgogoro wake ni katika ubepari na sheria zake zinazozuia watu kutumia rasilimali na kutoa marupurupu kwa makampuni ya Kimagharibi na kuzuia watu kulima ngano na mpunga ili makampuni ya Kimagharibi yanufaike kwa kuzileta katika nchi zetu. Inafilisi viwanda vizito ili tuweze kununua silaha, vifaa, na mitambo ya viwanda ya makampuni ya Kimagharibi, kwa ufupi, inaifanya nchi yetu kuwa soko la ustawi la bidhaa za Magharibi za kila aina, hasa zile za kimkakati, kuzinyonga shingo zetu kila tunapojaribu kutoroka kutoka kwa utumwa wa utegemezi.

Mgogoro wa Misri unatokana na kukosekana kwa mfumo unaojali watu kwa dhati, unaowahakikishia, kama watu binafsi, mahitaji yao ya kimsingi ya chakula, mavazi na vinywaji, na kuhakikishia jamii nzima usalama, elimu na huduma za afya kwa kiwango cha juu iwezekanavyo na bila malipo. Hakuna tofauti katika matunzo na utoshelevu baina ya tajiri na masikini, au baina ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu. Kila mtu ni sawa mbele ya dola katika haki na wajibu, na mfumo huu huu lazima uwezesha watu kunufaika na rasilimali na kuzitumia kikamilifu na kuzalisha mali kutoka kwao, lazima pia kuweka mkono wake kwenye vyanzo vya rasilimali za chini ya ardhi na madini na kuzalisha mali kutoka nazo na kuigawanya baina ya watu kwa mgawanyo wa haki. Haya yote yanaweza tu kuhakikishwa na Uislamu kwa mfumo wake imara na dola yake, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Hali ya watu wa Misri chini ya demokrasia ya kirasilimali ni mithili ya mtu anayezama katika bahari isiyoepukika na kushuka kuelekea shimo lake kwa ukali na mara tu Urasilimali, zana zake, na kile kinachotokana nao utakapong'olewa, watahisi tofauti kuanzia siku ya kwanza, na kwa kuutabikisha Uislamu kikamilifu, itakuwa ndio tegemeo lao kutokana na kuzama. Inatosha kwamba mkondo wa uporaji wa mali unaotiririka kwenye hazina ya Magharibi utakoma. Na upuuzaji unaoendelea wa mali za serikali zilizojengwa na kuasisiwa kwa jasho na damu ya watu utakoma, na ubadhirifu wa rasilimali na vyanzo vya mali iliyozikwa ambayo hupewa Magharibi utakoma bila ya bei. Inatosha kwamba ushuru kwa watu, ambao unazidi 74% ya rasilimali za serikali ya Misri, utaondolewa. Yote hayo yanakatwa kutokana na juhudi na akiba za watu na itawahurumia kuhusu bili za maji, umeme, na gesi pamoja na mambo mengine ambayo kiasili ni mali ya umma. Yote haya ni jambo ambalo ni Uislamu pekee pamoja na mfumo na dola yake unaweza kufanya au kuwapatia watu, basi je maisha ya watu yatakuwaje wakati huo? Bila shaka yatakuwa maisha ya staha.

Huu ndio mfumo tunaotaka kuutabikisha kwa uadilifu na rehema ya Uislamu. Mfumo unaowajali watu, kuwalisha, kuwavisha, na kuwanusuru masikini, na hauwafanyii watu fadhila au kuwafanyia biashara kwa kile kinachowapa katika haki au kuwapa matunzo na maisha ya staha. Huu ndio ulisia tunaoutaka kwa Misri na Ummah, na hilo lazima liwe lengo la kila anayeitakia mema Misri na watu wake, na hakuna njia ya kuipata isipokuwa kwa mambo matatu:

Kwanza: Kung'oa Ubepari unaotawala nchi zetu pamoja na zana, alama na watekelezaji wake wote, na kwa maumbo na sura zake zote.

Pili: Kujikomboa kutoka katika kutegemea Magharibi kwa sura zake zote na madhihirisho yake yote, na kufungwa balozi zake zinazochezea nchi zetu na kueneza sumu yake miongoni mwa watoto wa Ummah wetu.

Tatu: Utekelezaji kamili wa Uislamu katika Dola yake ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Kwa hili pekee, mageuzi ya Misri na mwamko wake utakuwa ndio mwamko wa kweli katika ngazi zote, na hii ndiyo njia na hakuna njia nyengine kwa kila mtu anayeitakia mema Misri na watu wake.

[وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ]

“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi.” [Al-A’raf 7:96]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu