Ijumaa, 17 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  6 Jumada II 1441 Na: 1441/ 05
M.  Ijumaa, 31 Januari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watu wa Misri Al-Kinanah, Wakijumisha Mukhlisina katika Jeshi, Kataeni Mpango wa Trump
Na Kesho Wataitakasa Al-Aqsa kutokamana na Uharibifu wa Mayahudi, Kesho iko karibu
(Imetafsiriwa)

Kutoa maoni juu ya tangazo la Trump la mpango wake wa amani kwa kinachojulikana kama Mpango wa Karne, Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Misri ilisema katika taarifa iliyochapishwa katika tovuti yake rasmi: “Misri inaona umuhimu wa kuzingatia utangulizi wa utawala wa Amerika kwa umuhimu wa kufikia kutatua suala la Palestina kwa ajili ya kuwarudishia watu wa Palestina haki zao kamili kupitia kuanzisha serikali huru yenye nguvu katika maeneo yaliyokaliwa ya Wapalestina kulingana na uhalali na maazimio ya kimataifa.” Katika taarifa yake, Misri iliziita pande mbili husika “kutilia maanani kwa umakini na kwa undani ruwaza ya Amerika ya kufikia amani na kutoa fursa za majadiliano kwa udhamini wa Amerika, kwa kurudisha tena mazungumzo.”

Katika taarifa hii iliyopotoka, Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Misri ilitanganza kuwa suala la Palestina ni suala linalohusu watu wa Palestina pekee, ilhali “inaziita pande mbili husika” kuzingatia kwa makini mpango wa Trump wa kihalifu na kufungua fursa za majadiliano, ijapokuwa inajua kuwa suala la Palestina ni suala la Ummah wa Kiislamu kulingana na sheria kwa kuwa ni ardhi ya Kiislamu iliyovamiwa na Mayahudi kwa msaada wa Makafiri Wakimagharibi na watawala madhalimu katika nchi za Kiislamu. Na kwa kuwa ni lazima kwa Ummah mzima wa Kiislamu kufanya kazi kuikomboa na kuitakasa kutokamana na machukizo ya Mayahudi na kuirudisha katika makaazi ya Uislamu, ndivyo ilivyo na ndivyo inavyopaswa kuwa.

Ummah hautarajii kutoka kwa watawala wa Waislamu, Waarabu na wasiokuwa Waarabu, harakati yoyote, kwani ni watumishi na vibaraka tu na hutekeleza wanayoamrishwa wao na mabwana zao katika koloni za Makafiri Wamagharibi, wakiamini kuwa hili litawahifadhia viti vyao ... Ndio, Ummah umeondoa mikono yao kwa watawala hawa ambao wamewaletea aibu na fedheha tu, na una wahesabu watoto wao waaminifu katika vikosi vya kijeshi ambao hawakubali kufedheheshwa na kuaibishwa, kama wanavyoona vipi serikali imehatarisha uwezo wa Ummah  na kuwasalimisha Ummah kwa maadui zake, na kuwatesa kwa adhabu mbaya zaidi. Sio jeshi la Misri lililowafukuza watu wa msalaba kutoka Bait al-Maqdis na kusitisha kuendelea kwa Matatari kusimama bila kazi kwani wanaona Mji wa Mtume (saw) unakabidhiwa kwa Mayahudi, watu wenye chuki zaidi kwa waumini.

Wacha njama hii kutoka Magharibi na Mashariki na kutoka kwa watawala waliojaa aibu na fedheha dhidi ya Ummah na Palestina iwe motisha thabiti kwa watoto wetu wa dhati katika jeshi la Misri na majeshi mengine ya Kiislamu kuziondoa serikali hizi na kusimamisha serikali ya pili ya Khilafa ya Yongofu kwa njia ya Utume, kuwarudishia Waislamu utukufu wao na nguvu zao. Na kuurudisha Ummah kama ulivyokuwa na kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyotaka uwe, taifa bora kuwahi kuinuliwa kwa wanadamu, na pia kurudisha urithi wa Ansar waliomuunga mkono Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa hivyo Mwenyezi Mungu amewahuisha wao katika Kitabu Chake Kitukufu hadi Siku ya Kiyama.

Enyi Mukhlisina katika Jeshi la Al-Kinanah: nyinyi ni, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, wenye uwezo wa kuwashinda maadui zenu. Serikali za kikafiri za kikoloni ni imara kwa mtazamo wa juu lakini dhaifu kiukweli. Wana silaha zilizoendelea lakini hawana wanaume wa kweli, na silaha bila wanaume ni dhaifu mbele ya waumini ambao wanaweza kuwa na silaha chache lakini wajuzi zaidi kwa kupigana. Serikali ya Kiyahudi ni dhaifu kuliko nyumba ya buibui mbele ya kelele za Mujahideen za Allahu Akbar, kwa sababu wanayo imani ya kweli inayowapa wao uwezo wa kupigana usiofikiwa na madhalimu. Mwenyezi Mungu yuko pamoja nanyi na Ummah wako nyuma yenu, hawatowaangusha kamwe, kwani unangojea siku ambayo mutainua bendera ya La Ilaha illa Allah, Muhammad Rasul Allah, siku hiyo Waumini watafurahi, kwa Ushindi wa Mwenyezi Mungu

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ)

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mumeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na Akhera ni chache.” [At-Taubah: 38]

                                    Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu