Afisi ya Habari
Wilayah Misri
H. 3 Dhu al-Qi'dah 1445 | Na: 1445/24 |
M. Jumamosi, 11 Mei 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je! Uhalifu Uliopita Haukutosha Kukomesha Makubaliano ya Khiyana? Au Kukomeshwa kwake Kunahitaji Mauaji Makubwa Zaidi?
(Imetafsiriwa)
Operesheni "ndogo" ya kijeshi iliyofanywa na jeshi la umbile la Kiyahudi huko Rafah ya Palestina hivi karibuni ilifanya mazungumzo mapya juu ya hali ya Misri ya kuamiliana na mpango wa umbile la Kiyahudi endapo kutatokea "uvamizi kamili wa Rafah," kwa kuzingatia maonyo ya mara kwa mara ya Misri kuhusu "madhara ya uvamizi wa mji huo kwa Wapalestina,” na hakikisho kutoka kwa umbile la Kiyahudi la "kuendelea kwa operesheni hiyo." Kwa mujibu wa mkuu wa zamani wa Kikosi cha Upelelezi cha Jeshi la Misri, mtaalamu wa mikakati, Meja Jenerali Nasr Salem, "Misri itafanya kazi ndani ya mfumo wa machaguo ya kidiplomasia ikiwa Rafah itavamiwa," akibainisha katika taarifa kwa Al-sharq Al-Awsat “Machaguo machache ya Misri katika kukabiliana na msimamo wa “Israel” hasa kwa kuzingatia umakinifu wa Cairo wa kupeleka misaada katika Ukanda wa Gaza, na kuchukua dori ya mpatanishi katika mazungumzo kati ya pande hizo mbili ili kufikia mwafaka katika Ukanda wa Gaza.” Kwa mujibu wa mkuu wa zamani wa Kikosi cha Upelelezi cha Jeshi la Misri, mtaalam wa kimkakati, Meja Jenerali Nasr Salem alisema, "Misri itafanya kazi ndani ya mfumo wa machaguo ya kidiplomasia endapo utatokea uvamizi wa Rafah." Mtaalamu wa Misri wa masuala ya "Israel" katika Kituo cha Al-Ahram cha Mafunzo ya Kisiasa na Kistratejia, Dkt. Saeed Okasha, alisema kuwa kukataa kabisa kwa Misri kuwafukuza Wapalestina na kuwaondoa katika ardhi zao "ni jambo ambalo Misri haija na haitakata tamaa”, akionyesha kwamba “ikiwa Israel itadhuru usalama wa taifa la Misri, Misri inaweza kuikimbilia Marekani kama mdhamini wa makubaliano ya amani, au kusimamisha utekelezaji wa mkataba wa (amani) iwapo kutatokea ‘uvamizi kamili wa Rafah.” Lakini Okasha aliieleza Al-sharq Al-Awsat kwamba "Israel ina nia ya kuhifadhi makubaliano ya (amani) na Misri, na licha ya hali katika ukanda wa mpaka, Tel Aviv bado inaweka amani na Cairo kama kipaumbele, ambayo itasukuma Tel Aviv kukaribia, ikiwa itazingatia kuvamia Rafah ya Palestina, kupitia operesheni ndogo katika kila kitongoji cha mji kibinafsi, ambayo inamaanisha kuwa vita vitaendelea kwa muda mrefu." (Al-sharq Al-Awsat, 10/5/2024)
Utawala wa Misri haujali damu ya watu wa Palestina na kwa kweli hausongei kuwanusuru, bali kutekeleza mipango ya mabwana zake katika Ikulu ya White House. Ikiwa utawala wa Misri ungekuwa na wasiwasi kuhusu watu wetu huko Gaza, ungetenda tofauti. Una chaguo halisi ambalo husuluhisha suala hilo, lakini haujalichukua na hautalichukua. Badala yake, ungali unajiambatanisha na Mkataba wa kisaliti wa Camp David, ambao ulihitimishwa miongo kadhaa iliyopita na kuhakikisha usalama na amani ya umbile la Kiyahudi.
Kinachopaswa kufanywa na Misri sio tu kutishia kusitisha makubaliano hayo yenye hatima mbaya, au hata kuonya juu ya kuyabatilisha, lakini lazima uyabatilishe mara moja, kuondoa mipaka na ardhi yetu iliyobarikiwa, na kuhamasisha jeshi la Misri kuwanusuru watu wake na kuikomboa ardhi yake kikamilifu, kuling'oa umbile la Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake na kuitakasa ardhi ya Uislamu na matukufu yake.
Je, ni mauaji kiasi gani zaidi tunayosubiri, zaidi ya mauaji yanayofanywa na Mayahudi na jinai nyingi zaidi walizofanya dhidi ya Ummah ili majeshi yasonge kwa hasira kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na matukufu yake na ukiukaji wa sheria zake?! Kusonga kwa majeshi kulikuwa ni faradhi tangu siku ya kwanza Mayahudi walipokanyaga Ardhi yetu Iliyobarikiwa. Sasa ni kitendo cha faradhi zaidi, kuwanusuru watu hawa wanaodhulumiwa, ni wajibu zaidi juu ya Misri na jeshi lake, kwani wao ndio walio karibu zaidi, wenye nguvu zaidi, na wanaostahiki zaidi, na wao ndio wanaojigamba kuwa ni wanajeshi bora zaidi ambao Mtume wetu (saw) aliwasifu. Kuwa bora ni sifa inayostahiki kwa mwenye kutekeleza aliyomuamrisha Mwenyezi Mungu ili kuuhifadhi Ummah, Dini yake na matukufu yake. Basi je, wanajeshi wa Misri watafanya hivyo, au wamewaangusha watu wetu katika ardhi iliyobarikiwa na kuwatii watawala waliomsaliti Mwenyezi Mungu na Mtume wake?
Enyi Wanajeshi wa Kinana (Misri): Huku watu wetu wakiuawa nchini Palestina ilhali wao wako masafa ya pua na mdomo tu kutoka kwenu, haijuzu kuketi. Bali, wajibu wenu ni kuikomboa Palestina yote, kuwanusuru watu wake wanaodhulumiwa, kuondoa dhulma dhidi yao, na kung'oa kila kitu kinachokuzuieni kutokana na wajibu huu, kama vile tawala na watawala waovu. Kwa hiyo, mutafanya nini?! Naapa kwa Mwenyezi Mungu, watawala hawatokufaeni, wala hawatabeba dhambi zenu, na kubwa zaidi ni dhambi la kuwatelekeza ndugu zenu wanaolilia msaada wenu, mchana na usiku. Je, hamjasikia maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):
«مَا مِنْ امْرِئٍ يَخْذُلُ امْرَأً مُسْلِماً فِي مَوْضِعٍ تُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ وَيُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ إِلَّا خَذَلَهُ اللهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ، وَمَا مِنْ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِماً فِي مَوْضِعٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ إِلَّا نَصَرَهُ اللهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ نُصْرَتَهُ»
“Hakuna mtu (Muislamu) atakayemtelekeza Muislamu mwengine mahali ambapo utakatifu wake unakiukwa na heshima yake inavunjwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamtelekeza mahali ambapo angependa msaada wake; na hakuna mtu (Muislamu) ambaye atamsaidia Muislamu mwengine mahali ambapo heshima yake inavunjiwa na utakatifu wake unakiukwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsaidia mahali ambapo ungependa msaada wake”.
Hivi muko wapi na majibu yenu ni nini kwa hawa watu wanaodhulumiwa wanaoomba msaada wenu?! Je, munasimama wapi kuhusiana na kitendo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambaye alitangaza wito wa kupigana na akaelekea kuifungua Makka na akasema: «لَا نَصَرَنِي اللهُ إِنْ لَمْ أَنْصُرْ بَنِي كَعْبٍ» “Hatoninusuru Mwenyezi Mungu mpaka niwanusuru Banu Ka'b”?! Muko wapi kuhusiana na Al-Muutasim, ambaye aliombwa msaada na mwanamke mmoja, akaja kumsaidia na kuifungulia Amuriya ili amnusuru? Ni upi msimamo wenu kuhusu maelfu ya wanawake wanaotafuta msaada wenu na wazee wanaotafuta msaada wenu?!
Enyi Askari wa Kinana, Enyi Wanajeshi bora zaidi: Sifa ya kuwa bora zaidi si nishani ya heshima, bali ni haki ya ufaradhi inayostahiki kupewa mwenye kubeba bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika haki yake, na ambaye ni tegemeo la Ummah na ngao yake, mwenye kuwahifadhi watu wake na matukufu yake, na wala haachani na haki zake kwa kisingizio cha makubaliano ya khiyana yaliyofungwa na watawala waovu. Kwa hakika sifa ya kuwa bora zaidi inawataka askari bora zaidi duniani waachane na watawala hawa na ahadi zote za uongo walizoweka, na kwamba wawe ni nusra kwa Ummah kupitia kusimamisha dola yake; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, hali inayowasukuma kunusuru Uislamu na watu wake, kuuhifadhi na kuhifadhi matukufu yake. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba sifa hii italetwa na nyinyi na iko ndani yenu, enyi Wanajeshi wa Kinana.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Misri |
Address & Website Tel: |