Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  1 Muharram 1446 Na: 1446/01
M.  Jumapili, 07 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Misri Inayakusanya Makundi ya Sudan kwa Manufaa ya Marekani na Kumakinisha Mamlaka yake, Sio kwa Manufaa ya Taifa au Watu wa Sudan!
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Jumamosi, tarehe 6 Juni 2024, kongamano la vikosi vya kisiasa vya kiraia vya Sudan lilizinduliwa katika mji mkuu wa Misri, Cairo, katika jaribio jipya la Misri kumaliza vita vinavyoendelea nchini Sudan. Waangalizi wanaamini kuwa jaribio hili linaweza kuweka msingi wa mazungumzo mapana, huku wengine wakipuuza umuhimu wa mafanikio ambayo linaweza kufikia. (Al-Araby Al-Jadeed). Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ilitoa mwaliko kwa “zaidi ya viongozi 50 wa vikosi vya kisiasa, kiraia, na kijamii, pamoja na watu mashuhuri wa kitaifa, viongozi wa kidini, na wasimamizi wa jamii. Mwaliko huo - uliotolewa kwa mashirika badala ya kambi za kisiasa- ulilitenga wimbi la Kiislamu.” Kwa mujibu wa barua ya mwaliko, “kongamano hilo, litakaoandaliwa na Mji Mkuu Mpya wa Utawala huko Cairo, litasikiliza katika vikao sambamba ruwaza za vikosi vya kiraia na kisiasa kuhusu athari mbaya za mzozo wa sasa nchini Sudan, njia za kuutatua, maumbile ya mahitaji yanayohitajika kwa wale walioathirika, pamoja na kutoa mwanga juu ya viambatisho vya mazungumzo ya kisiasa ya Sudan.” (Al-Nashra)

Serikali ya Misri, kama serikali zote katika nchi zetu, haina ubwana na haufanyi kazi kwa uhuru au hata kwa maslahi ya Misri au majirani zake. Badala yake, mienendo yake inaamriwa na mabwana zake katika Ikulu ya White House ili kulinda maslahi yao na kuimarisha utawala wao. Hili linadhihirika kutokana na vitendo vya serikali hii nchini Libya, Yemen, na hata Syria na Lebanon, kuwafungia watu wetu mjini Gaza, na hivi karibuni zaidi, vitendo vyake dhidi ya watu wetu nchini Sudan. Serikali hii inajaribu kuvizima vikosi vya kiraia vinavyoungwa mkono na Uingereza na kumaliza mzozo kwa njia ambayo inadumisha ushawishi wa Marekani na kumakinisha mamlaka yake. Hili bila shaka ndilo ambalo Marekani imeipa serikali ya Misri jukumu la kukamilisha kupitia kongamano hili na njia nyenginezo. Misri inatekeleza majukumu mengi kwa ajili ya Marekani na kuyakamilisha kwa ufanisi. Tawala mtawalia nchini Misri tangu Mapinduzi ya Julai 1952 hadi sasa zote zimewatumikia mabwana zao katika Ikulu ya White House na hazijali maslahi ya nchi wanazoziita nchi jirani au hata maslahi ya Misri yenyewe. Marekani, ambayo ilisababisha Misri kujitenga na Sudan, huenda katika siku zijazo ikafanya kazi katika mgawanyiko mpya wa Sudan, na Misri inaweza kuwa chombo cha mgawanyiko huu na motisha kwa ajili yake, hata ikimaanisha kupoteza sehemu za eneo lake.

Kile ambacho Misri inapaswa kufanya sasa ni kusimama dhidi ya miradi ya Marekani na kuwakabili kwa uthabiti wapiganaji wa Sudan, kuwazuia kumwaga damu ya watu wetu huko na kuwasitisha, hata kwa nguvu, kulinda watu. Zaidi ya hayo, wajibu ni kwa Sudan, katika sehemu zake zote mbili, kuwa tena sehemu ya Misri, kama ilivyokuwa hapo awali, na hivyo kuongeza nguvu kwa Misri. Hii itaiwezesha Misri kujikomboa kutoka kwa utegemezi wa Marekani badala ya kujisalimisha kwake, kufuata mwongozo wake, na kutekeleza miradi yake.

Wajibu wa Misri ni kuuongoza Ummah kuelekea ukombozi kutoka katika utegemezi wa kafiri Magharibi, na si kuwa sehemu ya ala za kupigania madaraka miongoni mwa wezi wa ubwana na mali barani Ulaya na Amerika. Wajibu wake ni kuwa ngao inayoulinda Ummah kutokana na kafiri Magharibi, washirika wake, na zana zake. Wajibu wa Misri ni kufanya kazi kuelekea kwenye umoja wa Ummah, kuregesha mamlaka yake, na kuondosha athari za Magharibi na mipaka yake ya bandia ambayo imegawanya na kuudhoofisha Umma. Wajibu wa Misri ni kuuongoza Ummah kuelekea kuung’oa ubepari na kuutekeleza kikamilifu Uislamu katika umbo lake pana ndani ya Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Kile ambacho Misri lazima ifanye kwa ajili ya Ummah hakitafikiwa na vibaraka wa Marekani, kwani wako vitani na Ummah na ni sehemu ya njama za makafiri wa Magharibi dhidi yake. Wao ndio wa kwanza wanaopaswa kung'olewa ili Ummah uweze kuregesha mamlaka yake na kusimamisha Dola ambayo Hizb ut Tahrir inajitahidi kwa ajili yake na inaulingania Ummah kufanya kazi kuielekea na kuishi chini ya: Dola moja ya Kiislamu ambayo haitambui mipaka ya Sykes-Picot na wala haijisalimishi kwa kafiri Magharibi na athari zake; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal:24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu