Jumatano, 05 Safar 1447 | 2025/07/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  25 Muharram 1447 Na: 1447/03
M.  Jumapili, 20 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuhamishwa kwa Watu wa Arish ni Uhalifu wa Kisiasa Uliojificha kama Maendeleo
(Imetafsiriwa)

Wakati serikali ya Misri ikizungumzia "kuimarisha bandari ya Arish," kuigeuza kuwa bandari ya kimataifa na kuiunganisha na mradi mpya wa ukanda wa kiuchumi, uhalifu wa halisi unafanywa dhidi ya wakaazi wa kitongoji cha Al-Raisa huko Arish. Watu wanalazimishwa kuondoka majumbani mwao chini ya athari ya matingatinga, na nyumba zao zinabomolewa kinyume na matakwa yao kwa kisingizio cha manufaa ya umma. Wanakabiliwa na shinikizo la kisaikolojia na mazungumzo ambayo hayaendani na hadhi ya kibinadamu na yanakiuka kanuni za Kiislamu.

Tukio hili si geni katika Sinai. Kwa miaka mingi, watu wake wamezoea jinsi serikali inavyowatendea kana kwamba ni wageni katika nchi yao wenyewe. Ardhi yao inapokonywa, nyumba zao zinabomolewa, wananyimwa huduma za aina zote, wanazuiwa kupanua miji, na wanachukuliwa kama usalama badala ya raia. Wamekuja kuishi katika eneo fiche, wakinyimwa haki zao na mara kwa mara wanatuhumiwa na serikali. Malalamishi yao hayasikilizwi na manung'uniko yao hayashughulikiwi.

Kulingana na ripoti zilizo uwanjani zilizotolewa mnamo Julai 2025, serikali ya Misri ilianza awamu ya nne na ya tano ya shughuli za ubomoaji katika kitongoji cha Al-Raisa, kilicho ndani ya eneo la kijiografia la bandari ya Arish. Awamu hii ni pamoja na kubomolewa kwa nyumba zilizopo, zinazokaliwa bila idhini ya wamiliki wake, ambao walifanya kikao mbele ya nyumba zao na kukataa kusaini hati za uhamishaji. Hata hivyo, hatimaye walilazimika kuondoka kufuatia shinikizo la usalama. Wengine hata walitishwa na kuonywa dhidi ya kuongezeka kwa uhasama.

Licha ya taarifa za serikali kwamba inatoa "fidia ya ukarimu" au "badali za nyumba," fidia hii haionyeshi thamani halisi ya mali - sio katika upande bei, wala katika upande wa kuwa ni eneo la kimkakati linaloangalia bahari, wala katika upande wa maisha ya jamii ambayo wameijenga kwa miongo kadhaa.

Aidha, ilikuja baada ya vitisho, sio mazungumzo, na baada ya uamuzi wa upande mmoja, si ridhaa na kukubalika. Ripoti huru za vyombo vya habari zimefichua kuwa uondoaji huu unafanywa chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa vikosi vya jeshi, kama sehemu ya mpango wa kubadilisha bandari hiyo kuwa eneo huru la kijeshi. Hii ina maana kwamba wakaazi hawana haki ya kisheria ya kupinga, kwa kuwa eneo hilo limeainishwa kama "manufaa ya umma," na hivyo kunyang'anywa ni haki ya serikali chini ya sheria chanya.

Lakini swali muhimu zaidi hapa sio tu la kisheria, bali pia Sharia: Je, serikali ina haki ya kuwaondoa watu kwa nguvu kutoka kwenye nyumba zao? Je, inajuzu kwa Sharia kubadili mali ya mtu binafsi kuwa ya umma kwa kisingizio cha maendeleo? Je, Sharia inaruhusu uhamishaji uliopangwa kama huu?

Uislamu umeifanya mali ya kibinafsi kuwa miongoni mwa mambo matatu matakatifu ambayo hayawezi kukiukwa. Mtume (saw) amesema:

«كُلُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ حَرَامٌ؛ دَمُهُ وَمَالُهُ وَعِرْضُهُ» “Kila Muislamu kwa Mwislamu mwenzake ni mtukufu, damu yake, mali yake na heshima yake.” Mali ya kibinafsi katika Uislamu inalindwa na haiwezi kuguswa. Serikali haiwezi kumnyang'anya mtu ardhi au nyumba yake isipokuwa kwa ridhaa na chaguo lake, na kwa sababu zilizo wazi za halali.

Hakuna kitu katika sheria ya Kiislamu kama "manufaa ya umma" ambayo kwayo serikali inaweza kuwanyang'anya watu mali zao bila ridhaa yao. Hii ni fahamu kutoka kwa mifumo ya kibepari ya Kimagharibi inayoiweka serikali juu ya watu na kuipa haki ya kunyang'anya mali ikiwa itaona kuwa ni "manufaa" kwa jamii.

Ubadilishaji wa serikali wa mali ya kibinafsi kuwa ya umma ni batili kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye anayeamua aina ya mali, sio serikali. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: [وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ] “Wala msiwapunje watu vitu vyao” [Ash-Shu’ara 26:183]. Mali ya kibinafsi haiwezi kubadilishwa kuwa ya umma au ya serikali. Ukiukaji wowote wa mali hii ni shambulizi dhidi ya hukmu ya Sharia.

Uislamu unaharamisha upotoshaji wowote wa umiliki kwa kisingizio cha maslahi au manufaa ya umma. Unaweka mamlaka ya matumizi mikononi mwa sheria ya Kiislamu, sio mtawala. Mwenyezi Mungu ndiye mmiliki halisi, na watu ni wadhaminiwa wa mali zao. Hawawezi kuondolewa humo isipokuwa kwa hukmu ya kisheria. Muislamu akimiliki nyumba au ardhi kihalali, hakuna mtu, awe mtu binafsi au dola, mwenye haki ya kumpokonya haki yake ya kuimiliki, hata kwa kisingizio cha kupanua bandari au mradi wa maendeleo. Badala yake, ni wajibu wetu kuheshimu umiliki huu na kutafuta masuluhisho halali ambayo hayakiuki haki za mtu yeyote.

Kinachotokea huko Arish ni utekelezaji wa moja kwa moja wa mfumo wa kibepari katika hali yake mbovu zaidi. Ni ukiukaji wa wazi wa kanuni za Kiislamu kuhusu pesa, mali, na madaraka. Chini ya mfumo huu, serikali inawaona watu kama idadi tu, inaona ardhi kama fursa ya uwekezaji, na inatanguliza "maendeleo" badala ya utu na haki. Kuwatoa Waislamu katika nyumba zao na kubomoa mali zao bila ya ridhaa yao, huku ikionekana kuwa halali chini ya serikali ya Misri, ni haramu kidini na hata ni uhalifu wa kisiasa kwa sababu ni dhulma na hujuma dhidi ya utakatifu wa Waislamu.

Zaidi ya hayo, kubadilisha bandari ya El Arish kuwa bandari ya kimataifa chini ya ubwana wa kijeshi, na kuunganisha maeneo makubwa ya jiji la El Arish kwenye mradi huu, kunazua maswali kuhusu malengo ya halisi ya mabadiliko haya: Je, ni kwa ajili ya uchumi kweli? Au ni hatua ya maandalizi ya kuwanyonya watu wa Gaza, kama ilivyopendekezwa na miradi ya kimataifa na ruwaza ya awali ya umbile la Kiyahudi?

Watu wa Sinai wanapaswa kukataa dhulma hii, kukemea sera hii isiyo ya haki, na kudai haki zao si kwa njia ya kuomba, bali kwa kujitahidi kuubadilisha utawala huu wa dhulma kutoka kwenye mizizi yake na kuasisi mfumo unaoshikamana na dini na kuhifadhi haki zao.

Enyi watiifu wa Jeshi la Kinana: Kinachotokea Sinai chini ya ulinzi wenu ni uhalifu kamili, na Mwenyezi Mungu atakuhojini kuhusu hilo na kuhusu wanaodhulumiwa kwa sababu yake. Baada ya kuwaangusha watu wa Gaza na kutumiwa kama mkono wa serikali katika kuwazingira, Wallahi, vyeo, mishahara, mapambo, na marupurupu ambayo serikali hii inakupeni kama rushwa ili mununue kimya chenu na muhakikishe utiifu wenu wakati munautiisha Ummah kupitia kwenu, hamtanufaika navyo. Andaeni jibu lenu, kwani hesabu ni nzito, na bado hamuna kipengee isipokuwa toba ya kweli kwa Mwenyezi Mungu, ambayo kwayo mutang’oa serikali hii, mutaondoa dhulma yake kutoka kwa watu, mutakomesha mzingiro wake wa watu wa Ardhi Iliyobarikiwa, na mutawanusuru wale wanaofanya kazi ya kutabikisha Uislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hii ndiyo njia yenu ya wokovu, na hakuna njia nyengine, haijalishi munafanya nini. Ni heshima, na asikutangulieni mtu kwayo. Kimbilieni, na Mwenyezi Mungu Akukubalieni toba yenu, na afanye maregeo yenu kuwa mema, na ajaalie ushindi kupitia mikono yenu, ili mpate izza duniani na heshima kesho Akhera. Mtakumbuka tunayowaambieni, na sisi tunamkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yetu.

[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيّاً وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيراً]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.” [An-Nisa 4:75]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu