Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  9 Muharram 1442 Na: 1442 / 05
M.  Ijumaa, 28 Agosti 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Msiba wa Karbala ni Ukumbusho Kwetu kwamba Utawala Pasi na Bay'ah ya Kisheria Haukubaliki katika Zama Zozote Zile

Imam Hussein alikufa Shahid katika njia ya kulinda utawala kwa Uislamu ambapo alipambana na mnyakuzi wa utawala, yazid, aliyetaka kusimamisha utawala wa nasaba. Msiba wa Karbala ni ukumbusho wa wajibu wa kuuhesabu vilivyo utawala kwa Uislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«وَاللَّه لَتَأْمُرُنَّ بالْمعْرُوفِ، وَلَتَنْهوُنَّ عَنِ الْمُنْكَرِ، ولَتَأْخُذُنَّ عَلَى يَدِ الظَّالِمِ، ولَتَأْطِرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ أَطْراً، ولَتقْصُرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ قَصْراً، أَوْ لَيَضْرِبَنَّ اللَّه بقُلُوبِ بَعْضِكُمْ عَلَى بَعْضٍ، ثُمَّ لَيَلْعَنكُمْ كَمَا لَعَنَهُمْ»

“Naapa kwa Mwenyezi Mungu, kwa yakini hamtaacha kulingania mema na hamtaacha kukataza maovu, wala hamtaacha kuukamata mkono wa dhalimu na mumuweke katika haki, na kumfanya ashikamane na haki, isipokuwa Mwenyezi Mungu atazigonganisha nyoyo zenu nyinyi kwa nyinyi kisha atawalaani kama alivyo walaani wao (Banu Israel) (Abu Dawood, Tirmidhi). Hivyo, leo, vipi tusiwahesabu watawala wa Pakistan, walioijaza dhulma ardhi na mbingu; wakiusalimisha uchumi wetu kwa taasisi za kikoloni, IMF na Benki ya Dunia, wakitoza kodi nzito ili kupata malipo ya riba kwa warasilimali wa ndani ya nchi na wa kimataifa, wakilitelekeza jiji la Karachi lililozama katika mafuriko huku Waislamu wake watukufu wakikabiliwa na hasara ya mamilioni ya Rupia na kuyazuia majeshi yetu yaliyo tayari na yenye uwezo huku Ardhi za Waislamu zikichafuliwa na umbile la Kiyahudi na Dola ya Kibaniani?

Hatuwezi kuonyesha unyonge mbele ya madhalimu kwa sababu kutimiza faradhi ya kuamrisha mema na kukataza maovu, kumhisabu dhalimu, yanaipa nguvu Dini hii na kuilinda jamii kutokana na Kumuasi Mwenyezi Mungu (swt). Ingawa Imam Hussein (ra) na wafuasi wake wachache watiifu hawakuweza kufaulu dhidi ya jeshi lililotumwa na Yazid, mapambano yao makali kwa utawala haramu wa Yazid yalizipiga muhuri nyoyo za vizazi vya baadaye vya Waislamu kuwa hakuna nafasi ya utawala wa kifalme au wa kurithishana. Upinzani huu unathibitisha kuwa muumini hawezi kukubali ukiukwaji wa hata sheria moja ya utawala na usimamizi. Hakika, kumpa Ba'yah mtawala ili atabikishe Uislamu ni haki ya Ummah pekee, ambayo ni lazima waitekeleze kwa kuridhia na hiari.  

Lakini, leo, watawala wanalazimishwa juu ya Waislamu ambapo hawajakiuka sheria moja tu ya Kiislamu pekee, bali wameitelekeza sheria yote ya Kiislamu na nidhamu yake ya utawala, Khilafah. Ni wajib juu ya kila muumini anayempenda Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw), familia yake tukufu (ra) na Maswahaba wake (saw) watukufu kujiunga na mapambano ya kuwang'oa madhalimu wa leo, ili Bay'ah kwa Khilafah Rashida iweze kurudishwa na hukmu kwa yale yote yaliyo teremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) iweze kuregea.

Msiba wa Karbala unawakumbusha Waislamu wote wenye ikhlasi wanaopambana dhidi ya watawala waliolazimisha na Magharibi juu ya ulimwengu wa Kiislamu, kutokuwa dhaifu mbele ya dhulma wala kuchoka kutokana na mfadhaiko. Muislamu mwenye ikhlasi daima husonga mbele dhidi ya dhulma, kwa Kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt), bila ya kuogopa hasara yoyote ya kimada hata kama atakikumbatia kifo cha shahada. Mwenyezi Mungu (swt) asema,                                                          

(وَالۡعَاقِبَةُ لِلۡمُتَّقِيۡنَ)

 “Na mwisho mwema ni wa wachamngu.” [Surah Al-Qasas, 28:83].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu