Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  15 Muharram 1442 Na: 1442 / 08
M.  Alhamisi, 03 Septemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Modi Anabadilisha Idadi ya Watu ya Kashmir kwa Nguvu, Ilhali Serikali ya Bajwa-Imran Inazuia Majeshi ya Pakistan kwa Utiifu wa Upofu kwa Amerika

Licha ya janga maambukizi ya virusi vya Korona, serikali ya kimabavu wa Modi ilitoa vyeti vipya 430,000 vya ukaazi katika Kashmir Iliyokaliwa ili kubadilisha idadi ya watu kwa nguvu kupitia "walowezi" katika eneo hilo, kwa kuiga mipango miovu ya umbile la Kiyahudi huko Palestina na China huko Turkestan Mashariki (Xinjiang). Ili kuhakikisha kuwa vikosi vya uvamizi vya dola ya Kibaniani havikabiliwi vikwazo, serikali ya Bajwa-Imran inazuia vikosi vya jeshi la Pakistan, kwa utii wao wa upofu kwa Washington, huku ikitoa visingizio visivyo na maana, ima ni kwa kuusihi Umoja wa Mataifa na Shirika la Nchi za Kiislamu, au kwa kuandika nukuu za tweet na maneno yaliyoandikwa! Kwa mfadhaiko huu, serikali inawakatisha tamaa Waislamu huko Kashmir ili wapoteze matumaini yote ya ukombozi, inavunja harakati na hatua za jihad ambazo hapo awali zilikuwa na nguvu, na kuzinyima msaada wa vifaa katika Mstari wa Udhibiti, kwa kutumia Jopo Kazi la Fedha. Serikali  inazuia vikosi vya Pakistan vilivyo tayari, licha ya kuwa India iko katika mzozo kwenye mipaka yake na China na inakabiliwa na upinzani mkali wa Kiislamu katika Kashmir Inayokaliwa na India, na jeshi lake limepanuliwa na kugawanywa pande mbili tofauti, wakiwa na silaha za zamani, na motisha ya vikosi vyake ni dhaifu.

Uongozi wa kisiasa na kijeshi umepoteza fursa nyingi za kuikomboa Kashmir kwa sababu ya utumwa wake kwa mamlaka ya kikoloni. Licha ya ukombozi wa maeneo makubwa ya Kashmir mnamo 1948, uongozi wa kisiasa na kijeshi haukutoa magari ya kivita ili kuharibu ulinzi wa uwanja wa ndege wa Srinagar. Haukutumia fursa hiyo kuhamasisha vikosi vya jeshi kukomboa Kashmir wakati wa vita kati ya India na China mnamo 1962. Mnamo 1965, katika ukanda wa (Akhnoor), ambao inafurahiya ulinzi mwepesi wa India, serikali ilipoteza nafasi nzuri ya kuikomboa Kashmir kwa kusimamisha amali za kijeshi, ambapo iliruhusu India kuunga mkono vikosi vyake vilivyosambazwa katika maeneo tofauti tofauti. Mnamo mwaka wa 1999, utawala huo ulijisalimisha katika shinikizo la kimataifa wakati wa Mgogoro wa (Cargill). Na hii hapa leo inaitelekeza Kashmir ili kuiridhisha Amerika ... Na vivyo hivyo, kwa sababu ya utegemezi mpofu wa nguvu za kikoloni na taasisi zao za kimataifa, wasaliti katika uongozi wa kisiasa na kijeshi wamepoteza, hadi sasa, Gurdaspur, Hyderabad, Deccan, Bengal, Sachin na sehemu kubwa ya Kashmir. Basi ni nani atakayekomesha msururu huu wa khiyana?

Enyi Maafisa Wenye Ikhlasi wa Vikosi vya Jeshi La Pakistan:

Kila usaliti unaofanywa na serikali husababisha mateso makubwa kwa mamia ya maelfu ya mama zetu, dada zetu, binti zetu na wana wetu, iwe kwa kuua, kutesa, kukatakata au kubaka. Na damu ya Waislamu inamwagika kama mito, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) anasema:

«لَزَوَالُ الدُّنْيَا أَهْوَنُ عَلَى اللَّهِ مِنْ قَتْلِ مُؤْمِنٍ بِغَيْرِ حَقٍّ»

"Kuondoka kwa ulimwengu ni sahali kwa Mwenyezi Mungu kuliko kumuua muumini bila haki" (Ibn Majah), na kuonyesha huzuni pekee kamwe haitoshi. Utawala wa Bajwa-Imran unakuzuini leo, kwa agizo la Amerika. Basi komesheni khiyana hii kwa kutoa nusra yenu ili kurudisha Khilafah kwa njia ya Utume, mugeuze njia ya historia kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya kumridhisha Yeye (swt). Fursa hii inapatikana kwenu, ambapo inamsubiri kila mwenye ikhlasi miongoni mwenu kufuata nyayo za Maanswari watukufu, miongoni mwa wale 

 

waliomnusuru Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) mithili ya swahaba Saad bin Muadh (ra). Hivyo basi, jitokezeni mtoe nusra yenu kwa Hizb ut-Tahrir ili tuweze kuanzisha Khilafah kwa njia ya Utume, ili iwanusuru Waislamu wa Kashmir na kumaliza miongo mingi ya kuishi chini ya unyanyasaji wa kikatili. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْراً﴿

“Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha. Hakika Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake.” [At-Talaq :3].       

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu