Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  21 Rabi' II 1442 Na: 1442 / 32
M.  Jumapili, 06 Disemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watawala wa Pakistan Wanaisaidia Amerika katika Kuasisi Serikali ya Kidemokrasia ya Kisekula Nchini Afghanistan, kwa Vazi la Kiislamu

Mnamo 2 Disemba 2020, ilitangazwa kuwa serikali ya Afghanistan na Taliban wamekubaliana juu ya sheria za mazungumzo. Mjumbe maalum wa Washington kwa Afghanistan alikaribisha tangazo hili kama "hatua muhimu". Afisi ya Mambo ya Nje ya Pakistan ilitangaza kwa shauku kwamba, "ni maendeleo muhimu yanayochangia kufikia mafanikio ya mazungumzo ya kindani ya Afghanistan. Pakistan itaendelea kuunga mkono mazungumzo ya ndani ya Afghanistan, ambayo yatafikia suluhisho jumuishi, pana na kamilifu la kisiasa lenye kutoa njia ya amani, utulivu na ustawi wa Afghanistan."

Kulingana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Amerika na Taliban ya Afghanistan mnamo 29 Februari 2020, mazungumzo ya kindani ya Afghanistan, na serikali kibaraka wa Amerika ya Afghanistan, yalipangwa kuanza kutoka 10 Machi 2020, kuamua juu ya usitishaji mapigano kamili na muundo wa kisiasa. Lakini katika miezi kumi iliyopita, maendeleo yalikwama, na kuongeza hatari ya Taliban kurudi kwenye vita kamili, ambavyo vingevunja mbavu za vikosi vya Amerika vilivyo kosa shajaa na vyenye uoga. Mazungumzo ya kindani ya Afghanistan ni muhimu kwa Washington, ili kuinasa Taliban ndani ya mfumo wa katiba ya kisekula ya Afghanistan, na mageuzi bandia ya Kiislamu. Amerika inazidisha utumiaji wa vibaraka wake ili kupata maslahi yake ng'ambo kwa sababu ya udhaifu wake unaokuwa. Kwa hivyo, Amerika imeupa jukumu uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan kuipeleka Taliban ndani ya mtego wa kisekula. Mtego huu wa Amerika utalinda maslahi ya Amerika, kwa msaada wa majeshi kidogo ya karibu vikosi 2500 hadi 4000, vilivyoko ndani ya kambi chache za jeshi.

Kwa maagizo ya Amerika, serikali ya Bajwa-Imran unajitahidi sana kufikia malengo ya Amerika ya kieneo. Ili kufungua njia ya makubaliano ya Disemba, mjumbe maalum wa Amerika wa Afghanistan, Zalmay Khalilzad, alitembelea makao makuu ya jeshi huko Rawalpindi mnamo 3 Novemba 2020, kukutana na mkuu wa jeshi, Qamar Javed Bajwa. Halafu mnamo 19 Novemba 2020, siku ambayo Imran Khan alifika Kabul, mwanadiplomasia wa Amerika, Angela Aggeler, alikutana na mkuu wa jeshi huko Rawalpindi. Kulingana na taarifa iliyotolewa na ISPR, katika mikutano yote miwili, mchakato wa amani wa Afghanistan na usalama wa eneo hilo ulijadiliwa. Wakati wa ziara yake ya Kabul, Imran Khan alisema kuwa Pakistan itaendelea kuunga mkono juhudi za kupata makaazi ndani ya Afghanistan, ikipokea sifa kutoka kwa Amerika.

Enyi Waislamu katika Jeshi la Pakistan! Zingatieni ruwaza fisidifu ya uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan. Inadai kwamba tutapata faida za kiuchumi kutoka kwa mashirika ya kifedha ya kimataifa, ikiwa tutafuata kwa uttiifu amri za Amerika, kupata maslahi yake katika eneo letu. Serikali hii inadhoofisha usalama wa Pakistan kwa ajili ya dolari zilizochumwa kwa kulinda utawala wa wakoloni wa Amerika. Inafanya hivyo ingawa nguvu ya vikosi vyake vya kijeshi na ujasusi ni kwa ajili ya kutimiza maslahi ya Uislamu na Waislamu, ikiwemo kupangua mipango haribifu ya Amerika. Kila mtu mwenye akili timamu anajua kuwa Pakistan ndio nguvu kubwa zaidi nchini Afghanistan, inayoamua mwelekeo wake wa kisiasa pamoja na muundo wa usalama. Lazima mutoe Nussrah kwa ajili ya kusimamisha Khilafah nchini Pakistan, ambayo itaweza kuambatanisha kwa urahisi Afghanistan na Asia ya Kati ili kuimarisha Ummah kwa umoja, na kuilazimisha Amerika kutoka eneo hilo, kisiasa, kiuchumi na kijeshi. Huu ndio ushindi wa kweli ambao Waislamu lazima wautafute. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَن يَشَاء وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu