Jumanne, 04 Dhu al-Qi'dah 1442 | 2021/06/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  19 Jumada I 1442 Na: 1442 / 38
M.  Jumapili, 03 Januari 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Agizo la Kumtoa Naveed Butt Lilitolewa Mnamo 4 Januari 2018, lakini Angali Hajaonekana wala Kuskika Tangu Kutoweka Kwake kwa Kulazimishwa mnamo 11 Mei 2012

(Imetafsiriwa)

Serikali ya PTI inafanya kazi bila huruma huku mkoloni Magharibi FATF akiamuru kukamatwa kwa wale wanaopigana na vikosi vya Dola ya Kibaniani huko Kashmir Iliyokaliwa. Lakini, inajikokota wakati mamlaka ya kisheria ya Pakistan inataka afueni kwa Muislamu anayelingania kusimamishwa tena kwa Khilafah kwa Njia ya Utume. Mnamo 4 Januari 2018, Tume ya Uchunguzi ya Pakistan juu ya Kutoweka kwa Kulazimishwa ilitoa agizo la kutolewa kwa Naveed Butt, lenye nambari ya kumbukumbu ColoED ID Namba 860-P. Agizo hilo linasema kwamba "Kwa msingi wa ushahidi uliokusanywa wakati wa kesi hii, inashukiwa na Tume kwamba Mtu aliyepotea Naveed Butt ... alichukuliwa na wafanyikazi wa Taasisi ya Siri (e) na anazuiliwa katika kizuizi chao haramu." Agizo la kutolewa kisha linasema, "tume inaridhika kuamuru kwamba Naveed Butt ... aletwe mbele ya Tume ... ndani ya kipindi cha wiki tano, kinyume chake kesi hiyo itaanzishwa kulingana na sheria." Imekuwa miaka mitatu, sio wiki tano, tangu agizo hili la utolewaji lilipotolewa bila Naveed Butt kuletwa mbele ya tume au korti yoyote, na kesi bado inasubiri katika Mahakama Kuu ya Islamabad. Familia bado inasubiri uthibitisho wowote ikiwa Naveed yuko hai au aliuawa shahidi, tangu alipotekwa nyara mnamo Ijumaa tarehe 11 Mei 2012.

Tabia kama hii ya kikatili inafichua watawala wa Pakistan katika madai yao ya uongo ya kuwa watiifu kwa Jimbo la Madinah. Inamuweka mtetezi wa Khilafah ya Kiislamu katika utowekaji wa kulazimishwa, baada ya kutanua kila aina ya huduma za huruma kwa jasusi wa Dola ya Kibaniani Kulbushan Jadhav na rubani mshambulizi wa jeshi la anga, Abhinandan Varthaman. Utawala wa Bajwa-Imran unaendelea kumdhulumu Muislamu anayelingania hukmu kwa yale yote yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt), licha ya kuwa Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 (مُحَمَّدٌ رَّسُوۡلُ اللّٰهِ وَالَّذِيۡنَ مَعَهٗۤ اَشِدَّآءُ عَلَى الۡكُفَّارِ رُحَمَآءُ بَيۡنَهُمۡ)

“Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao” [Surah Al-Fath 48:29].

Enyi Waislamu wa Pakistan na haswa Mawakili wao, Wanahabari na Wanaharakati wa Haki za Binadamu!

RasulAllah (saw) amesema,

«إنَّ النَّاسَ إَذا رَأوُا الظَّالِمَ فَلمْ يَأْخُذُوا عَلى يَدَيْهِ أوْشَكَ أن يَعُمَّهُمُ اللَّهُ بعِقَاب»

“Ikiwa watu watamuona dhalimu na wasimshike mikono yake (wasimzuie kudhulumu) basi watakaribia wote kujumuishwa na Mwenyezi Mungukatika adhabu.” [Abu Dawud, Tirmidhi, ibn Majah]. Utekaji nyara unaoendelea wa Naveed Butt ni dhulma ya wazi ambayo hatuwezi kuinyamazia kimyaNi jukumu letu kuzungumza dhidi ya uhalifu huu, katika kila kikao tutakachokipata, kuitisha kuachiliwa huru kwa Naveed mara moja. Hivyo, Waislamu wote, hususan wale walio na mamlaka na ushawishi, nawatafute radhi ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa kuitisha kikomo cha mateso ya Naveed na familia yake.

RasulAllah (saw) amesema,

«مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤْمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ اَلدُّنْيَا، نَفَّسَ اَللَّهُ عَنْهُ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ يَوْمِ اَلْقِيَامَةِ»

“Yeyote atakayempa afueni Muislamu kutokana na tatizo miongoni mwa matatizo ya duniani, Mwenyezi Mungu atampa afueni kutoka na tatizo miongoni mwa matatizo ya Siku ya Kiyama” [Muslim].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-pakistan.com/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu