Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  14 Ramadan 1442 Na: 1442 / 67
M.  Jumatatu, 26 Aprili 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Huku Ikidhikika kati ya Pande Mbili, Dola ya Kibaniani Imepoteza Ukuu  Wake wa Kiidadi, Ilhali, Watawala wa Pakistan Wanaipa Ofa ya Amani Badala ya Kupigana kwa Ajili ya Kuikomboa Kashmir Iliyokaliwa!

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 24 Aprili 2021, Jenerali Bajwa alikuwa na mazungumzo ya masaa saba na wanahabari, akifichua diplomasia ya mlango wa nyuma kati ya maafisa wa ujasusi wa Pakistan na India. Watawala wa Pakistan wanajua vizuri kuwa India imepoteza ukuu wake wa kiidadi kwenye mpaka wa Magharibi, baada ya kudhikika kati ya Jeshi la Pakistan upande mmoja na Wachina upande wa kaskazini. Sasa, uwiano wa Pakistan na askari wa Dola ya Kibaniani kwenye Mstari wa Udhibiti umeshuka hadi mmoja kwa  mmoja, ambayo ni ya chini kabisa katika historia. Lakini, badala ya kuhamasisha simba wenye hamu ya vikosi vya jeshi la Pakistan kwa ukombozi wa Kashmir Iliyokaliwa, watawala wa Pakistan wanafuata kwa upofu maagizo ya Rais Biden wa Amerika, akitoa msaada muhimu kwa Dola ya Kibaniani, ili idumishe ukaliaji wake wa kikatili wa Kashmir.

Dola hiyo ya Kibaniani inapitia moja ya mizozo mibaya zaidi katika historia yake katika kiwango cha kistratejia. Kwa mara ya kwanza katika historia yake, India ilihamisha kikosi chao cha kwanza cha mashambulizi kutoka upande wa Pakistan hadi upande wa Wachina, na kufanya iwe vigumu kwa India kuhami upande wa Kashmir, wakati uwepo mkali wa Pakistan katika Mstari wa Udhibiti unabaki kuwa tishio kubwa. Waislamu waasi wa Kashmir wanakabiliwa na kufungiwa mara mbili, licha ya hivyo wanaasi vikali dhidi ya Dola ya Kibaniani, kiasi ya kuwa hata kikundi cha kisiasa kinachounga mkono India hakiwezi kuunga mkono India waziwazi. Janga la virusi vya Korona la India kwa sasa ni baya zaidi ulimwenguni, na Modi anakabiliwa na hasira kali ya umma kwa kusafirisha nje chanjo na oksijeni wakati watu wake wanahitaji zote mbili. Kujumuishwa kwa nguvu kwa Kashmir Iliyokaliwa imekuwa nukta ya mzozano mkali kwa Dola ya Kibaniani, huku Pakistan ikiwa na nafasi ya kidiplomasia kuingia katika eneo hili lenye mgogoro kuwakomboa Waislamu wa Kashmir kutokana na dhulma, kama ilivyo wajibu wetu mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Lakini, badala ya kupatiliza fursa hii ya dhahabu, watawala wa Pakistan wako kwenye ukurasa wa Biden. Makubaliano ya kusitisha mapigano katika Msitari wa Udhibiti hutoa msaada wa kistrategia kwa India, huku ikiwatelekeza Waislamu wa Kashmir.

Ili kuuficha udikteta wa Amerika katika lugha ya kidiplomasia, ruwaza ya Jenerali Bajwa yanaonyeshwa kama uchumi wa kijiografia, badala ya mkakati wa kieneo, ili kuimarisha uhusiano wa kikanda na India yenye uadui mkubwa. Licha ya upinzani mkali kutoka kwa watu wa Pakistan na vikosi vyake vya kijeshi, ruwaza ya Bajwa inakuuzwa, ingawa ni mpango wa zamani wa Amerika wa utawala wa India wa eneo hilo, ambapo Amerika inataka kuipunguza Pakistan kuwa serikali iliyo chini ya India, ili Dola ya Kibaniani iweze kushindana na China. Ili kufikia lengo hili, bajeti ya ulinzi ya Pakistan kwa uwiano wa Pato la Taifa inapunguzwa. Zaidi ya hayo, diplomasia ya mlango wa nyuma inaunda dhana kuwa endapo Dola ya Kibaniani itarejesha hadhi ya zamani ya Kashmir, basi usawazishaji mahusiano unaweza kuendelea. Kwa hivyo, uongozi wa sasa wa kijeshi na kisiasa wa Pakistan ni kibaraka wa ruwaza ya Amerika ya India Kuu, inayohujumu Pakistan na vikosi vyake vya jeshi.

Uadui wa Mabaniani washirikina dhidi ya Uislamu na Waislamu ni mkali sana. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

]لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ ٱلنَّاسِ عَدَٰوَةٗ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱلۡيَهُودَ وَٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْۖ]

“Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina.” [Surah Al-Maida 5:82]. Hili ndilo umbile lao, ambalo historia yetu yote inashuhudia.Uongozi wa sasa wa Pakistan umefichua waziwazi sura yake inayounga mkono Amerika. Mashaka yote yameondolewa na ni wakati muafaka sasa kwa wenye ikhlasi ndani ya vikosi vya kijeshi kuhamasika ili kuangamiza mpango huu wa Amerika, kwa kusimamisha Khilafah. Maafisa wenye ikhlasi lazima watoe Nussrah yao kwa Hizb ut Tahrir sasa, ili simba wa vikosi vya jeshi la Pakistan, ambao wanatamani kushiriki katika Ghazwa ya Hind, waikomboe Kashmir kutoka kwa makafiri wabaya zaidi, wairegeshe kwa ulinzi na Uislamu kwani ni wajibu wao wa Kiislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu