Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 19 Dhu al-Qi'dah 1442 | Na: 1442 / 86 |
M. Jumatano, 30 Juni 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Dola ya Kibaniani kwa Ujasiri Imevihamisha Vikosi Hadi Mpaka Wake na China, Ikiwa na Hakika kuwa Watawala wa Sasa wa Pakistan Kamwe Hawatapigana Kuikomboa Kashmir Iliyokaliwa
(Imetafsiriwa)
Mnamo 28 Juni 2021, Bloomberg iliripoti kwamba India imeelekeza angalau vikosi 50,000 vya ziada mpakani mwake na China, na kuongeza uwepo wa askari huko hadi 200,000, juu na zaidi ya asilimia 40 kutoka mwaka jana, katika mabadiliko ya kihistoria katika msimamo wa kijeshi wa kiushambulizi. Kwa hivyo Modi alifanyaje kile ambacho hapo awali kilifikiriwa kuwa hakiwezi kufikiriwa, tangu India kuikalia Kashmir mnamo 1947, ikichochea moto wa mpaka dhidi ya Pakistan? Baada ya kujiondoa kwa aibu kwa Amerika kutoka Afghanistan, Rais wa Amerika Joe Biden sasa anaidhibiti China kwa kupangilia upya mali za eneo, pamoja na zile za mshirika wake kipenzi, India, kama mwendelezo wa sera ya "Pivot to East Asia" ambayo alianzisha kama Makamu wa Rais wa Obama. Lakini, Modi hawezi kumtumikia Biden kwa ufanisi, isipokuwa ahakikishiwe na watawala wa Pakistan kwamba hawatapeleka vikosi wakati wa mapigano na China, kwa sababu jeshi la India lililogawanyika na lililovunjika moyo haliwezi kupigana vyema kwa upande mmoja, achilia mbali pande mbili changamfu. Kwa hivyo, kwa utiifu wa kipofu kwa mabwana zao wa Amerika, uongozi wa kijeshi na kisiasa wa Pakistan unasonga mbele kuelekea katika usawazishaji mahusiano na Dola ya Kibaniani, wakikataa katakata kupigana na India juu ya Kashmir Iliyokaliwa.
Licha ya Modi kuiambatanisha Kashmir Iliyokaliwa na mnamo 5 Agosti 2019, watawala wa Pakistan hawakuchukua hatua kwa kuvuka wazi kwa laini nyekundu. Badala ya uhamasishaji mkubwa na wa haraka wa kijeshi, Imran Khan alitangaza mnamo tarehe 18 Septemba 2019, "Ikiwa mtu yeyote kutoka Pakistan atakwenda India kupigana jihad ... atakuwa adui wa Wakashmir," jambo ambalo ilifurahikiwa sana na mabwana zake wa Amerika. Hata wakati Dola ya Mabaniani na China zilipambana juu ya Bonde la Gulwan eneo la Ladakh kwa miezi kadhaa, uongozi wa kijeshi ulizuia majeshi yetu yenye nia na uwezo, badala ya kutumia fursa nzuri ya kuikomboa Kashmir Iliyokaliwa. Kwa kuongezea, uongozi wa kijeshi ulikaa kimya cha kuidhinisha juu ya tangazo hatari la Imran Khan mnamo Juni 20, 2021 kwamba, "Pindi tu kutakapokuwa na suluhu juu ya Kashmir, majirani hao wawili wataishi kama watu wastaarabu. Hatutahitaji kuwa na vizuizi vya kinyuklia. "
Enyi Waislamu wa Pakistan, Wakiwemo Maafisa Wenye Ikhlasi wa Majeshi ya Pakistan!
Uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan unakuulizeni mkubali kuisalimisha Kashmir Iliyokaliwa kwa Modi kwa hoja kuwa Pakistan itaibuka kuwa imara zaidi, baada ya Amerika kuunda ukanda wa biashara wa "uunganishi wa kieneo." Lakini, tunadaganywa sasa kama tulivyodanganywa miaka ishirini iliyopita, wakati uongozi wa kijeshi ulioegemea upande wa Amerika wakati huo ulipodai kwamba kushirikiana na Amerika katika Vita vyake dhidi ya Ugaidi kutaimarisha Pakistan, lakini kwa kweli ilisababisha kupoteza kwa makumi ya maelfu ya maisha na makumi ya mabilioni ya dolari. Uongozi wa sasa wa kijeshi wa Pakistan unatudanganya sasa kwa sababu Amerika na Dola ya Kibaniani zimethibitishwa kuwa maadui wa Uislamu, Waislamu na Pakistan na wala hawatachukua hatua hata moja kuimarisha Pakistan. Usaliti wa uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan ni dhahiri kwa wote isipokuwa wale wanajitia upofu, huku kutofanya kazi kwetu daima kunaruhusu uharibifu usioweza kurekebishwa kwa Pakistan. Kwa hivyo, maafisa wenye ikhlasi katika vikosi vya jeshi la Pakistan lazima watoe Nussrah yao mara moja kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Ni Khilafah pekee ndiyo itakayozuia mpango wa Amerika wa kuasisi utawala wa India wa kieneo ili kuchunga dhidi ya China pamoja na mwamko wa Uislamu, kupitia kuhamasisha simba wa majeshi ya Pakistan kwa ukombozi muhimu wa Kashmir Iliyokaliwa kutokana na mshiko dhaifu wa Modi, kama hatua ya kwanza kati ya hatua nyingi za kudhibitisha utawala wa Dini tukufu ya Uislamu.
(وَقَاتِلُوۡهُمۡ حَتّٰى لَا تَكُوۡنَ فِتۡنَةٌ وَّيَكُوۡنَ الدِّيۡنُ كُلُّهٗ لِلّٰهِ)
“Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.” [Surah Al-Anfal, 8:39]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |