Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  23 Dhu al-Hijjah 1442 Na: 1442 / 93
M.  Jumatatu, 02 Agosti 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Iwe ni Ufungaji Kijanja au Kamilifu, Serikali ya Federali na Sindh ni Nukta za Kujishindia Alama za Kisiasa juu ya virusi vya Korona, Huku Zote Zikiwa Haziangalii Mahitaji ya Kiafya na Kiuchumi ya Waislamu

(Imetafsiriwa)

Mnamo 30 Julai 2021, Waziri Mkuu wa Sindh alitangaza kuifunga kwa ghafla Karachi kwa siku tisa, jiji kubwa zaidi la Waislamu ulimwenguni, lenye idadi ya watu inayokadiriwa kuwa zaidi ya milioni ishirini, akidai kwamba ililenga kudhibiti kuenea kwa virusi vya Korona aina ya Delta. Kufungiwa huku ni pamoja na kufungwa kwa masoko yote na biashara, na pia marufuku kupanda zaidi ya mtu mmoja kwenye pikipiki. Saa za kufungua maduka ya mikate na vyakula zimedhibitiwa, huku matembezi ya umma yamepunguzwa sana, na kuwanyima ajira mamia kwa maelfu ya vibarua wenye kupokea mshahara kila siku, ikiongezea katika idadi ya makumi ya maelfu kwa mamilioni wasio na ajira. Kufungwa huku pia kutaongeza mamilioni kwa zaidi ya asilimia ishirini ya Wapakistan ambao wanaugua utapiamlo. Ijapokuwa elegezaji kamba mwengine umefanywa baada ya shinikizo kubwa la umma, Demokrasia haikuzingatia shida ya mamilioni ya wahasiriwa wa ufungwaji, walionyimwa huduma msingi za maisha.

Kwa upande mwingine, serikali ya federali ilijibu kufungwa kwa Karachi kana kwamba yenyewe ilikuwa ikikabiliana na janga la virusi vya Korona (Covid-19) kwa njia bora zaidi, kwa mito ya maziwa na asali kutiririka nchi nzima. Je! Serikali ya federali sio iliyochelewesha uagizaji chanjo, kabla ya wimbi la tatu kuishambulia nchi? Tunauliza iwapo jukumu la serikali ni kuzuia kuenea kwa virusi vya Korona pekee au pia kuokoa watu kutokana na njaa, umaskini na mateso? Tunauliza ni mamia ya maelfu mangapi ya vipimo vya virusi vya Korona watawala hawa wanavyoweza kufanya kila siku, hata baada ya mwaka mmoja na nusu tangu mwanzo wa mkurupuko, ili kuwatenganisha wagonjwa na wazima? Baada ya mawimbi matatu, watawala lazima wawafichulie umma ni uwezo gani umeongezwa wa vifaa vya kupumua, ugavi wa oksijeni, vitanda vya hospitali, vyumba vya wagonjwa mahututi na vifaa vya kinga binafsi, ili maelfu ya wagonjwa wa virusi Korona waweze kutibiwa bila kukatisha maisha ya kila siku? Je! Watawala watajaribu kuficha uzembe wao mpaka lini nyuma ya ufungaji kijanja na kamilifu? Mpaka leo maelfu ya watu wanapanga foleni kwa masaa mengi, wakijazana kama dagaa, kwa ajili ya chanjo katika vituo vilivyojaa pomoni, pasi na hatua zozote za tahadhari. Kwa kuongezea, lazima walipe malipo ya hongo kwa utawala fisadi wa watawala, ili kufungua biashara au kuendesha usafirishaji, ili kuepuka athari za ufungwaji kikamilifu na kijanja.

Watawala wote wa mkoa pamoja na wa federali kwa uhalifu wanapuuza watu, huku wakijishindia alama za kisiasa kwa ajili ya uchaguzi ujao. Mwanzoni mwa janga hili, watawala walipuuza maagizo ya Kiislamu ya liweka karantini kamili eneo la mkurupuko, ikiruhusu virusi kuenea kote nchini, na kuzidisha hali mbaya ya janga hili. Halafu, badala ya kutafuta mwongozo kutoka kwa Uislamu, watawala waliiga kwa upofu mataifa ya Magharibi kwa kulazimisha ufungaji kamili. Lakini, lau watawala wangechukua mwongozo kutoka kwa Uislamu, wangewatenga wagonjwa kutoka kwa wazima, kupitia upimaji imara, ili kuruhusu maisha ya kawaida kuendelea. Kwa kweli, iwe ni serikali ya PTI iliyo katikati au serikali ya PPP mkoani, demokrasia inapuuza yote ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameteremsha. PTI na PPP zote hushiriki katika ugomvi wa wafuasi wasio na matunda, huku hakuna zikiwa hasimami juu ya ukweli wa Uislamu. Wanafanya hivyo ingawa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alionya,

«وَمَثَلُ الَّذِي يُعِينُ قَوْمَهُ عَلَى غَيْرِ الْحَقِّ كَمَثَلِ بَعِيرٍ رُدِّيَ فِي بِئْرٍ فَهُوَ يَنْزِعُ مِنْهَا بِذَنَبِهِ»

“Mfano wa yule anayewasaidia watu wake kwa jambo lisilo la haki (Uislamu) ni kama mfano wa ngamia mfu aliyeanguka kisimani kisha akavutwa nje kwa mkia wake. (Musnad Ahmad). Mtihani huu wa Mwenyezi Mungu (saw) umefichua kwa dhati kufeli kwa Demokrasia kote duniani. Wakati sasa umewadia kuuangaza ulimwengu kwa nuru ya Uislamu kupitia Khilafah kwa Njia ya Utume. Ni Khilafah pekee ndio itakayodhamini utoaji huduma ya afya pamoja na mahitaji msingi, kupitia utabikishaji wa hukmu za sheria za Uislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu