Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  14 Sha'aban 1438 Na: PR17031
M.  Alhamisi, 11 Mei 2017

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mwacheni Huru Naveed Butt, Mtetezi wa Khilafah Utekaji Nyara wa Miaka Mitano Hautazuia Kurudi kwa Khilafah kwa Njia ya Utume

 (Imetafsiriwa)

Ni miaka mitano sasa tangu Ijumaa tarehe 11 Mei 2012, wakati majambazi wa watawala wa Pakistan walipomteka nyara Naveed Butt, Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan. Kile kinachoitwa "uhalifu" wa Naveed Butt ni kwamba alikuwa ni sauti yenye ushawishi mkubwa nchini Pakistan kwa ajili ya kusimamishwa tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Wito wake wenye nguvu ulikuwa pambano la moja kwa moja kwa vibaraka wa Amerika na ulidhoofisha mipango ya mabwana wao wa Washington. Naveed bila hofu aliwaonya Waislamu juu ya uwepo wa wakoloni wa Amerika unaodhoofisha eneo hili, na vile vile mpango wa Amerika wa "Akhand Bharat" (India Kuu) wa kuinyanyua India kama dola kubwa ya kanda hii. Lakini, badala ya kusimama kando ili kutoa nafasi kwa Haki kama toba, watawala wasaliti waliongeza dhambi zao nyingi, kwa kuwapiga vita watetezi wote wa Khilafah, kwa njia ya vitisho, mateso, ukamataji, utekaji nyara na kuteswa vikali ambako kulijumuisha utiaji shoti ya umeme. Hadi leo wasaliti hawa wanangali wanamzuilia Naveed katika utekaji nyara, ingawa katika Hadith Qudsi,

قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ «إِنَّ اللَّهَ قَالَ مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ»

“Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, hakika Mwenyezi Mungu amesema: 'Yeyote atakayemdhuru Walii wangu basi nimekwisha tangaza vita naye...” [Bukhari].

Na wahalifu hawa hutumia nguvu dhidi ya Mashababu wa Hizb ut Tahrir ingawa Mwenyezi Mungu (swt) ameteremsha katika Quran,

 (إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ)

“Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.” [Surah Al-Buruj 85:10].

Lakini, utawala wa Bajwa-Nawaz umefadhaishwa na ukweli kwamba Hizb ut Tahrir haijaachana na mapambano yake, licha ya kukandamizwa kwa nguvu. Ukweli ni kuwa, ushawishi wa Hizb ut Tahrir umeongezeka ndani ya Waislamu kwa jumla na haswa majeshi, kwani Waislamu huwaheshimu wale wanaovumilia shida kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw).

Enyi Waislamu wa Pakistan! Uvumilivu wa Naveed haswa na Mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa jumla una funzo muhimu kwetu sote. Nguvu kama hiyo ndani ya muumini haitokani na njia za kimwili mbele ya dhalimu mwenye nyezo, bali hutokamana na Imaan yenye nguvu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Imaan hii ndio mwamba ambao kwao ubabe huvunjwa vunjwa. Hili ndilo somo ambalo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alilifikisha kwa Ummah wake wakati alipotuarifu juu ya haja ya kukaidi mbele ya mtawala dhalimu na matokeo mema ya kufanya hivyo. Imesimuliwa kutoka kwa Khabab bin Aratt (ra) ambaye alisema:

شكونا إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم وهو يومئذ متوسد بردة في ظل الكعبة، فقلنا: ألا تستنصر لنا؟ ألا تدعوَ لنا؟ فقال: «قد كان الرجل فيمن كان قبلكم يؤخذ فيحفر له في الأرض، فيجاء بالمنشار على رأسه فيجعل بنصفين فما يصده ذلك عن دينه، ويمشط بأمشاط الحديد ما دون عظمه من لحم وعصب فما يصده ذلك، والله ليتمنَّ الله عز وجل هذا الأمر حتى يسير الراكب من صنعاء إلى حضرموت لا يخاف إلا الله تعالى، والذئب على غنمه، ولكنكم تستعجلون»

"Siku moja tulimshitakia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipokuwa amejipumzisha chini ya kivuli cha Kaaba, tukamwambia: Mbona usituombee nusra (kwa Mwenyezi Mungu)? Mbona usituombee Dua (kwa Mwenyezi Mungu)? Akasema (saw): 'Alikuwa mtu katika wale waliokuja kabla yenu, akichimbiwa shimo ardhini akiingizwa humo, kisha ukiletwa msumeno na kuwekwa juu ya kichwa chake, akikatwa vipande viwili; lakini hilo halingemfanya aachane na dini yake; na akichanwa nyama za mwili wake kwa kichana cha chuma mpaka ikibakia mifupa, lakini hilo halikumfanya aachane nayo. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwa yakini Mwenyezi Mungu Mtukufu ataitimiza amri (dini) hii mpaka mtu aliyepanda kipando atatoka Sanaa hadi Hadhramout akiwa haogopi chochote isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt), na mbwa mwitu kwa mbuzi wake, lakini nyinyi ni watu mulio na pupa." [Imesimuliwa na Ahmad].

Kwa hivyo msiwaogope watawala madhalimu na simameni imara pamoja na Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika jukumu la kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume.

Enyi Maafisa wanyofu wa Jeshi la Pakistan! Ni kupitia nguvu ya Imaan yao, ndipo wanasiasa wenye uwezo na wakweli wa Hizb ut Tahrir wanaweza kushikamana na Haki mbele ya madhalimu. Kwa hivyo, ni kitu gani kinachotarajiwa kwa maafisa wa jeshi wenye uwezo na wakweli, walio na uwezo wa kumsitisha dhalimu na kusimamisha Haki kupitia nguvu zao, ndani ya masaa? Jiepusheni na minong'ono ya mashetani wa serikali hii wanaotafuta kutia hofu ndani yenu na jikirimuni kwa kusimama na Ummah katika wakati wa mahitaji yao dhidi ya madhalimu wa leo. itikieni wito wa Hizb ut Tahrir na mutimize wajibu wenu kwa kutoa Nussrah kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, kwa kuwasitisha watawala madhalimu kileleni mwa usaliti wao na kuponya nyoyo za waumini.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu