Jumanne, 06 Dhu al-Hijjah 1443 | 2022/07/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  12 Jumada I 1438 Na: 17008
M.  Jumatano, 08 Februari 2017

Ni Wajibu kwa Waislamu Kuwahesabu Watawala kwa Uislamu

Maandamano ya Kudai Kuachiliwa Huru kwa Naveed Butt, Mtetezi wa Uislamu na Khilafah Yake

 (Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan ilifanya maandamano kote nchini, ikitaka kuachiliwa huru kwa Naveed Butt, msemaji wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Waandamanaji walikuwa wamebeba bendera iliyotangaza: "Mwachilieni Huru Naveed Butt, Mtetezi wa Khilafah". Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan inalaani vikali unafiki wa utawala linapokuja suala la Uislamu na sura yake ya kisiasa.

Hivyo basi, kwa upande mmoja, tuliwaona maafisa wa serikali na wasemaji wao wakizingatia kupotezwa kwa nguvu kwa wanabloga huru, hadi walipoachiliwa huru ndani ya miezi kadhaa.

Hata hivyo, linapokuja suala la Naveed Butt, serikali inadumisha kimya cha jiwe ingawa amepotezwa kwa nguvu kwa miaka minne na miezi tisa, baada ya kutekwa nyara na asasi za serikali mnamo tarehe 11 Mei 2012!

Ni wazi kutokana na msimamo wa serikali kuwa imejisalimisha kikamilifu kwa Washington kuhusiana na unafiki wake juu ya kujieleza kisiasa. Amerika inavumilia tu kujieleza kisiasa ndani ya Ulimwengu wa Kiislamu wakati kunapojengwa juu ya msingi Demokrasia ya kikafiri na uhuru wa kiliberali, ambayo ndio chimbuko la dhulma kote duniani leo.

Hata hivyo, pindi Muislamu yeyote anapoufunga usemi wake wa kisiasa kwenye Quran na Sunnah, anakuwa mlengwa wa serikali. Hapo ndipo Washington hufumbia macho huku vibaraka wake katika Ulimwengu wa Kiislamu wakitoa adhabu na mateso kwa Waislamu wanyofu, jambo ambalo hata wanyama wa msituni wangeliepuka. Zaidi ya hayo, Muislamu yeyote anayefanya kazi ya kuuregesha Uislamu kama mfumo kamili wa maisha anaonekana kuwa mtu duni na Amerika na vibaraka wake, na hana haki hata ya kuhukumiwa mbele ya mahakama kwa kujieleza kwake kisiasa. Ni nani aliyeipa Amerikan haki ya kuamua aina ya kujieleza kisiasa ndani ya Ulimwengu wa Kiislamu? Hivyo basi, vibaraka wake wanathubutuje kushiriki katika upumbavu wa kujaribu kutengua kipindi cha zaidi ya milenia moja ya kushikamana na Uislamu, Dini ya Haki! Na wanathubutuje kutumia nguvu kuwazuia Waislamu wasimhesabu mtawala kwa Uislamu, jambo ambalo sio haki tu, bali ni wajibu ambao kwao watahesabiwa na Mwenyezi Mungu (swt).

Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan inatoa wito kwa watu wanyoofu ndani ya vyombo vya habari, wanasiasa, Maulamaa, wasomi, mawakili na wanaharakati wa haki za binadamu, ambao wanauheshimu sana Uislamu na Waislamu, kupaza sauti kwa ajili ya kuachiliwa huru Naveed Butt. Kama ibada ya kweli kwa Mwenyezi Mungu (swt) ni lazima wasiache juhudi yoyote ya kukomesha dhulma kubwa dhidi ya Naveed, inayofanywa katika nchi iliyoasisiwa kwa jina la Uislamu. Hivyo basi kwa ajili yetu wenyewe tupaze sauti zetu dhidi ya madhalimu na tuondoe dhulma. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«إنَّ النَّاسَ إَذا رَأوُا الظَّالِمَ فَلمْ يَأْخُذُوا عَلى يَدَيْهِ أوْشَكَ أن يَعُمَّهُمُ اللَّهُ بعِقَاب»

“Pindi watu wanapomuona dhalimu na wasimzuie mikono yake basi watakaribia kujumuishwa katika adhabu na Mwenyezi Mungu.” [Abu Dawud, Tirmidhi, ibn Majah].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu