Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  14 Safar 1444 Na: 1444 / 06
M.  Jumamosi, 10 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Huzuni ya Watawala wa Waislamu juu ya Kifo cha Malkia wa Uingereza, Inatokana na Kujitolea kwao kwa Ukoloni wa Magharibi

(Imetafsiriwa)

Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, aliandika kwenye anwani yake rasmi ya Twitter mnamo 8 Septemba 2022, “Nimehuzunishwa sana na kifo cha Mtukufu Malkia Elizabeth II. Pakistan inaungana na Uingereza na mataifa mengine ya Jumuiya ya Madola kuomboleza kifo chake.” Watawala wa Ulimwengu wa Kiislamu, miongoni mwa Waarabu na wasiokuwa Waarabu, wametangaza huzuni kubwa kwa kuaga dunia Malkia wa Uingereza, kana kwamba ni Khalifah mwadilifu amefariki, akitawala kwa uadilifu na kuwapa wanadamu uongozi wenye huruma. Kabla ya umati wa Waislamu kushiriki katika maombolezo ya watawala, uhalisia wa utawala wa kifalme wa Uingereza, ukiwemo uongozi wake, familia ya kifalme ya Uingereza, lazima uzingatiwe kwa makini.

Utawala wa kifalme wa Uingereza ndio unaoongoza mambo ya dola ya kikoloni, Uingereza, kupitia mtandao mpana wa ushawishi. Ushawishi wa ufalme wa Uingereza unaenea zaidi ya Nyaraka za Whitehall, zilizotayarishwa na mawakili wa Afisi ya Baraza la Mawaziri, ambazo zinaonyesha kuwa miswada ya bunge iko chini ya mamlaka ya wakuu wa familia ya kifalme kuidhinisha au kuzuia sheria mpya. Utawala wa kifalme wa Uingereza hudumisha ushawishi kupitia majukwaa kama vile bunge la House of Lords, House of Commons, Afisi ya Baraza la Mawaziri, Kanisa la Uingereza, Jiji la London, Whitehall, Huduma ya Ujasusi ya Kisiri (MI6), Sandhurst na Oxbridge.

Utawala wa kifalme wa Uingereza ni mchangiaji mbunifu wa mpangilio wa kiuchumi wa wakoloni hivi leo, ambao umeitumbukiza sehemu kubwa ya ulimwengu katika deni kubwa, ili wawekezaji wa Magharibi katika mikopo, wanufaike na malipo ya riba. Viongozi wake wa viwanda wanatumia rasilimali tajiri na nguvukazi tele ndani ya Ulimwengu wa Kiislamu, ikiwemo eneo la Ghuba na kuenea zaidi ya hilo, huku kwa wivu wakizuia maendeleo yake ya viwanda. Ujasusi wake unazua matatizo ndani ya maeneo ya Umma wa Kiislamu, kwa kutumia vibaraka wa kisiasa na kijeshi iliyo waajiri, katika taasisi kama vile Oxbridge na Sandhurst. Hakika, vibaraka hawa ndio wanaofanya kazi kulingana na muundo wa Lawrence wa Uarabuni, ili kuwatumia wenyeji katika maeneo ya mbali, kwa ajili ya Ufalme huu.

Ama kuhusu watawala wa Pakistan, wanazungumza kana kwamba wanaishi Windsor, badala ya kutoka Bara Hindi, ambalo ni mandhari ya uhalifu wa ufalme wa Uingereza, kwa zaidi ya karne tatu. Chini ya Uislamu, kabla ya uvamizi wa Waingereza, hisa ya Bara Hindi dogo ya uchumi wa dunia ilikuwa asilimia 23, kubwa kama ya Ulaya yote ikijumuishwa pamoja, ikipanda hadi asilimia 27 mnamo 1700, wakati wa zama za Aurangzeb Alamgir. Baada ya kukaliwa na Waingereza, ilishuka hadi chini ya 4%, huku mamia kwa maelfu wakiteseka kwa baa la njaa. Waingereza walilipora eneo hili kwa miaka 173, na kulikamata eneo la sasa ambalo ni sawa na dolari trilioni 45!

Kwa hakika, Waislamu lazima wautambue utawala wa kifalme wa Uingereza jinsi ulivyo na wajibu kifo cha mfalme wake ipasavyo. Katika zama za dola ya Uingereza iliyodorora sana duniani, ni fursa mwafaka kwa Ulimwengu wa Kiislamu kuepuka minyororo ya mafungamano yanayoendelea ya Uingereza, ikiwemo Jumuiya yake ya Madola na mtego wake wa minyororo ya kijeshi na kiuchumi. Waislamu lazima sasa waamiliane na watawala wa Waislamu kama walivyo, mashabiki na vibaraka wa ukoloni. Na Waislamu lazima wafanye kazi ya kusimamisha tena Dini yao, kama Khilafah kwa Njia ya Utume, ili hatimaye ulimwengu uweze kuondolewa dhulma ya ukoloni wa Amerika na Ulaya. Wakati huo ulimwengu hautaomboleza tena kifo cha wahalifu wa kivita na madhalimu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

(فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ)  

“La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula.” [Surah Ad-Dhukan 44:29].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu