Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  20 Muharram 1445 Na: 1445 / 03
M.  Jumatatu, 07 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Chini ya Uchumi wa Sasa wa Kibepari, ni Kipote cha Wacheche tu ndio Hufaidika na Miradi ya Maendeleo. Ni Chini ya Kivuli cha Khilafah Pekee, ndipo Miradi Italeta Ustawi kwa Maisha ya Watu

(Imetafsiriwa)

Mnamo 1 Agosti, 2023, Mkutano wa Madini wa Pakistan 2023 uliandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Petroli na shirika la Barrack Gold Corporation. Katika hotuba yake, Waziri wa Kawi, Idara ya Petroli, Dkt. Musadik Malik aliwaalika wawekezaji wa kigeni kuwekeza katika sekta mbali mbali za Pakistan, haswa madini na uchimbaji madini. Alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kuongeza uwekezaji wa moja kwa moja nchini na kusonga zaidi ya "vumbi la maendeleo."

Katika miaka ya sitini ya karne iliyopita, Pakistan ilifanya maendeleo katika baadhi ya sekta za viwanda na kilimo. Iliitwa 'Muongo wa Maendeleo.' Walakini, baadaye ikawa wazi kuwa sehemu kubwa ya matunda ya maendeleo haya yalikuwa tu kwa familia ishirini na mbili za kibwenyenye pekee. Halafu katika miaka ya themanini na tisini ya karne iliyopita, uchumi wa soko huria, ukombozi wa biashara, ubinafsishaji wa taasisi za umma na ujenzi wa barabara, zilitangazwa kuwa msingi wa maendeleo. Walakini, faida ya sera na miradi hii pia ilifungika tu kwa sehemu ndogo ya idadi ya watu na wawekezaji wa kigeni. Nchi na watu walibaki masikini.

Vivyo hivyo, katika muongo wa kwanza wa karne ya sasa, ukuaji wa mawasiliano ya simu, na kisha Ukanda wa Kiuchumi wa China-Pakistan (CPEC), katika muongo wa pili, yalitangazwa kama mdhamini wa maendeleo ya nchi. Hata hivyo, kwa mara nyingine tena, faida zake nyingi zilivunwa na mashirika ya kimataifa na kampuni za Kichina. Watu na Serikali walibakia na umaskini, na walizama zaidi katika deni.

Hivi sasa watu wanapewa pipi mpya. Inaelezwa kuwa kwa kuwa Pakistan ina utajiri wa mali ya madini, madini yenye thamani ya matrilioni ya dolari yapo nchini Pakistan, ikiwa tutafanya kazi kwa bidii katika sekta hii, hatima ya Pakistan na watu wake itabadilika. Swali ni lipi jipya katika hili? Pakistan ilitia saini makubaliano na kampuni moja ya Kichina karibu miaka ishirini iliyopita ili kuchimba shaba na dhahabu kutoka kwa migodi ya Saindak huko Baluchistan, ambayo yameongezwa hadi 2037. Pakistan na watu wake hawajapata chochote kutoka kwa mradi huu. Badala yake, eneo ambalo madini haya yanatoka bado lingali linaumia kutokana na umaskini na mateso.

Ikiwa yaliyopitiwa miaka sitini iliyopita yatakumbukwa, haitakuwa vibaya kusema kwamba kwa mara nyingine tena wawekezaji wadogo wa ndani na wawekezaji wa kigeni wanaunyonya utajiri huu wa madini. Ni wazi kutoka kwa waandazi wa mkutano huo kampuni moja kubwa ya kimataifa, na pia washiriki wa mkutano huu. Kwa hivyo, kwanza kabisa, swali linapaswa kujibiwa kuwa licha ya uwepo wa mambo yote ya maendeleo, kwa nini Pakistan na watu wake wanatamani ufanisi?

Sababu kuu ya hali hii ni mfumo wa uchumi wa kibepari unaotabikishwa nchini Pakistan. Daima unatabikishwa, iwe kuna demokrasia, udikteta wa kijeshi au serikali ya mseto. Mfumo wa uchumi wa kibepari unapeana karibu rasilimali zote katika jamii kwa sekta ya kibinafsi. Faida halisi ya rasilimali hizi huenda kwa makundi yanayotawala sekta ya kibinafsi. Kampuni hizi za hisa hukusanya mabilioni ya dolari kupitia muundo wa ufadhili wa kibepari. Benki, masoko ya hisa, masoko ya mitaji na wawekezaji wa kitaasisi wanapata udhibiti wa rasilimali hizi. Hii ni licha ya kuwa faida za utajiri wa nchi zinapaswa kufikia watu wote. Mfumo wa kibepari huhakikisha mkusanyiko wa utajiri katika mikono michache.

Urasilimali huzingatia utajiri mikononi mwa kipote kidogo cha mabepari katika nchi "zilizoendelea" vilevile. Katika robo ya kwanza ya 2023, asilimia 69 ya utajiri wote nchini Marekani ulikuwa unamilikiwa na asilimia 10 ya wachumaji. Kwa kulinganisha, asilimia 50 ya wachumaji walikuwa na asilimia 2.4 pekee ya utajiri jumla. Rasilimali nyingi za Pakistan zitawanufaisha watu tu katika mfumo kiuchumi wa Kiislamu pekee chini ya kivuli cha Khilafah kwa njia ya Utume. Mfumo wa uchumi wa Uislamu huzingatia madini kuwa ni mali ya umma. Kwa hivyo, dola inahitajika kusimamia hatua zote za uchimbaji madini, kusafisha na kuuza madini haya yenyewe. Lazima itumie mapato juu ya mahitaji ya watu, kwa sababu Dola ya Khilafah ni dola ya usimamizi, kuchunga mambo ya watu. Kwa njia hii, watu na dola hufanikiwa, kwa sababu ya utabikishaji wa amri hii moja ya mfumo wa kiuchumi wa Uislamu.

Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[وَلَوۡ اَنَّ اَهۡلَ الۡقُرٰٓى اٰمَنُوۡا وَاتَّقَوۡا لَـفَتَحۡنَا عَلَيۡهِمۡ بَرَكٰتٍ مِّنَ السَّمَآءِ وَالۡاَرۡضِ]

“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi.” [Al-A’raf 7:96].

Ni lazima kwa watu wenye nguvu kutoa Nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, bila kupoteza zaidi, muda, nguvu na pesa, juu ya maagizo ya kibepari yaliyofeli.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu