Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
| H. 23 Jumada II 1447 | Na: 17 / 1447 |
| M. Jumapili, 14 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je, Vikosi vya Kiislamu vya Jeshi la Pakistan Sasa, Chini ya Uongozi wa Jenerali wa Marekani, Vitawalinda Mayahudi na Kuupokonya Silaha Upinzani wa Palestina?
(Imetafsiriwa)
Gazeti la Dawn liliripoti kwenye tovuti yake mnamo tarehe 13 Disemba, 2025 kwamba majeshi ya Waislamu huenda yakatumwa kuanzia mwezi ujao kwa ajili ya “Kikosi cha Kimataifa cha kuleta Utulivu” mjini Gaza. Hapo awali, mtawala kibaraka wa Marekani Shehbaz Sharif alikuwa tayari ametoa idhini “ya kikanuni” kwa kutumwa kwa vikosi vya Pakistan huko Gaza. Hata hivyo, wakiogopa upinzani mkali wa umma, watawala wa Waislamu mmoja baada ya mwengine wamekuwa wakionyesha kutokuwa na msaada kwao mbele ya Amerika. Hivyo sasa shetani Trump na wafuasi wake, watawala wa Waislamu, wanaunda njama mpya za kutumia vikosi vyetu vya Waislamu vya mujahid kuwalinda Mayahudi na kuwanyang'anya silaha Hamas na vikosi vyengine vya upinzani vya Palestina. Ripoti hiyo inathibitisha kwamba, mbali na vyombo vya habari, maelezo yanakamilika kwa kutumwa kwa vikosi vya Waislamu. Utawala wa Trump pia umesema kwamba kituo cha utoaji amri za kijeshi huko Gaza kitaongozwa na jenerali mmoja au wawili wa Marekani. Kwa hivyo ni wazi kwamba vikosi vya Waislamu vitatumika chini ya uongozi wa jenerali wa vita vya msalaba wa Marekani kutekeleza dhamira ile ile chafu ambayo Amerika na umbile la Kizayuni kwa pamoja hazingeweza kukamilisha!
Enyi Maafisa wa Vikosi vya Jeshi la Pakistan!
Amri za Uislamu ziko wazi na dhahiri. Hakuna utiifu kwa mtu yeyote katika yaliyo haramu na uvunjaji wa sheria. Mtumwa hawajibiki kwa bwana wake, mke kwa mumewe, watoto kwa wazazi wao, wala jeshi kwa uongozi wao katika mambo ya dhambi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«إِنَّمَا الطَّاعَةُ فِي الْمَعْرُوفِ» “Hakika, utiifu ni katika mambo mema tu (ma‘ruf).” [Bukhari, Muslim]. Na akasema (saw):
«السَّمْعُ وَالطَّاعَةُ عَلَى الْمَرْءِ الْمُسْلِمِ فِيمَا أَحَبَّ وَكَرِهَ، مَا لَمْ يُؤْمَرْ بِمَعْصِيَةٍ» “Kusikiza na kutii ni wajib kwa Muislamu kwa yale anayoyapenda na anayoyachukia, maadamu hajaamrishwa kutenda dhambi.” [Bukhari, Muslim].
Matokeo ya kukiuka amri hizi ni kwamba tangu zama za Musharraf kauli mbiu yenu ya “imani, uchamungu, na jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu” imezikwa kwa uthabiti, na mukageuzwa kuwa jeshi la kisekula la kitaifa ambalo kisha likageuka kuwa jeshi la mamluki. Uongozi mtawalia wa kijeshi uliiweka Kashmir kwa urahisi kwenye mapaja ya Hindu Baniya, Kashmir ile ile ambayo mulitoa maelfu ya uhai kwa ajili yake. Hata hivyo uongozi wenu ulijibu kwa kutoa amri ya kusitisha mapigano katika Mstari wa Udhibiti. Kutokana na uoga wa uongozi wenu, dola ya Kibaniani ilichukua udhibiti wa mito ya Pakistan. Iwe ni uongozi wa kiraia au wa kijeshi, wote wamezama katika upanuzi, marupurupu, ufisadi, idhini ya mabwana Wamarekani, na sasa kinga; na jeshi lenye nguvu zaidi la Ummah wa Kiislamu linaendelea kugeuzwa kutoka kwenye misheni yake hadi kutumikia ubeberu wa Marekani. Na sasa mambo yamefikia hatua kwamba vikosi vyetu vya Kiislamu vyenye uwezo na ari vitatekeleza mkataba wa kuwalinda “wale ambao ghadhabu imewashukia” (Mayahudi) na kuunyang'anya silaha upinzani wa Palestina?!
Enyi Maafisa wa Vikosi vya Jeshi la Pakistan!
Msidanganyike na uwongo wa watawala hawa kwamba vikosi vyetu vya jeshi havitawanyang'anya silaha Hamas. Agizo la kikosi wanachotumwa kujiunga nacho tayari limewekwa katika azimio la Umoja wa Mataifa, ambalo linajumuisha kuwanyang'anya silaha Hamas. Vikosi hivi vitatekeleza majukumu chini ya kituo cha amri cha Marekani kinachoongozwa na jenerali wa Marekani, kilichoanzishwa haswa ili kuwapa Mayahudi udhibiti katika ardhi hii iliyobarikiwa. Kituo hiki cha amri kipo ili kukamilisha ajenda ile ile ambayo haijakamilika ya Mayahudi na Amerika: kuondoa upinzani wa silaha kwa Waislamu na kuwalazimisha kujisalimisha kikamilifu mbele ya Mayahudi. Kwa hivyo, Enyi Maafisa wa Vikosi vya Jeshi la Pakistan, kimya hiki kitaendelea hadi lini? Kila siku inapopita, kimya chenu kinakuwa sababu ya uhalilifu wenu, gharama ambayo Ummah mzima lazima ulipe. Toeni ahadi ya utiifu mara moja: hakuna zaidi!
Enyi Maafisa wa Vikosi vya Jeshi la Pakistan!
Nyinyi ndio vikosi vya jeshi vyenye nguvu zaidi vya Ummah wa Kiislamu. Nyinyi ndio walinzi wa nguvu na heshima ya Ummah huu. Jitengeni na kushindwa huku na minyororo ya utaifa. Amri za uongozi kibaraka wa Marekani sio takatifu, bali amri za Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saw). Utakatifu hauko katika mistari iliyochorwa na Waingereza, bali katika uhai, utajiri, heshima, na imani ya Waislamu. Adui si Waislamu, bali ni mfumo wa kilimwengu wa kibeberu wa kikrusedi, umbile la Kizayuni, na dola ya Kibaniani. Watawala wenu ni manaibu wa mfumo huu wa kilimwengu wa kibeberu, wakitupilia mbali nguvu za Ummah, ikimaanisha nyinyi, miguuni mwa mfumo huu wa kibeberu wa kikrusedi na Wazayuni.
Wokovu wa Ummah huu upo katika kusimamisha Khilafah Rashida na kujikomboa kutoka kwa watawala hawa, na njia hii itapatikana kupitia ujasiri na azma yenu kwa kutoa nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida na kuvunja mpangilio huu wa kibeberu. Hizb ut Tahrir inakulinganieni, katika hatua ya mwisho ya mpango wake mpana, kujiunga katika jukumu hili. Je, mutajibu?
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surah Al-Anfal, 8:24]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: +(92)333-561-3813 http://www.hizb-pakistan.com/ |
Fax: +(92)21-520-6479 E-Mail: htmediapak@gmail.com |



